KINGAZI BLOG: June 2016

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, June 30, 2016

Waziri Mkuu Awataka Wanufaika wa Mikopo ya Elimu Juu Kurejesha mikopo waliyopewa.


Wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya Juu ambao tayari wapo katika ajira wametakiwa kurejesha marejesho ya mikopo waliyopewa kutokana na mfuko wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kutegemea fedha hizo kuendelea kuwakopesha wanafunzi wengine.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha hotuba ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja.

“Uwezo wa Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu kuwahudumia walengwa unajengwa na fedha zinazotengwa kila mwaka katika mipango na Bajeti pamoja na marejesho ya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika,”alisisitiza Mhe. Majaliwa.

Aliendelea  kusema kuwa Serikali inaendelea kufanya maboresho ya kimfumo na kisheria ili kuimarisha urejeshwaji wa mikopo. 

Aidha amewaagiza waajiri wote Nchini kutekeleza wajibu wao wa kuingiza makato ya marejesho wa mikopo ya wanufaika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa baada ya kuwasiliana na Bodi ya Mikopo.

Vile vile Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu sambamba na kushughulikia changamoto mbalimbali zilizopo katika Bodi ya mikopo ili kuhakikisha utoaji wa mikopo unafanyika kwa ufanisi.

Pia Serikali inategemea kubadilisha utaratibu wa kutoa mikopo ili kuwafikia wanafunzi wote wenye uhitaji zaidi wakiwemo yatima na wenye uwezo mdogo kiuchumi bila kujali aina gani ya program wanazozisomea.

Wednesday, June 29, 2016

BOFYA HAPA HAPA KU APPLY ONLINE MKOPO WA ELIMU YA JUU

HIGHER EDUCATION STUDENTS' LOANS BOARD

Online Loan Application and Management System





>>>>>>BOFYA HAPA KUAPPLY MKOPO WA ELIMU YA JUU ONLINE <<<<<<<<<

Rais Magufuli asema haya kuhusu ugunduzi wa gesi ya Helium nchini Tanzania


June 28 2016 ziliripotiwa taarifa kuwa watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalamu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Leo June 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kupitia account yake ya tweeter amepost akizungumzia ugunduzi huo huku akitoa wito kujipanga katika eneo la mikataba……..
>>>Tunamshukuru Mungu Tanzania tumegundua gesi aina ya Helium(He),wito wangu kwa wachumi,wanasheria na watanzania wote kwa ujumla tujipange
>>>Ugunduzi huu utuelekeze kujipanga hasa ktk eneo la mikataba yetu ili rasilimali hii adimu isaidie kuujenga uchumi wetu

Mbunge Chadema Avuliwa Ubunge!


Ole+Nangole
Aliyekuwa Mbunge wa Longido, Mhe. ONESMO NANGOLE.
Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika Mahakama Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii.
Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea Ubunge wa CCM, Jimbo la Longido, Dk. KIRUSWA alifikisha mahakamani shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya Mbunge wa Longido, Mhe. ONESMO NANGOLE.
Onesmo-Ole-Nangole
Akisoma hukumu hiyo, Jaji MWAGESI alisema kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili Dk. Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.
Katika shauri hilo, dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikuwa ni;
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa Mhe. Onesmo Nangole
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mhe. Nangole
3.Kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura
4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo
Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni, sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili, Jaji kutoka Mahakama Kuu Bukoba Mh. Jaji Mwagesi alisema;
“Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria, Natamka kwamba;
Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki.”

Rais ‘Aruhusu’ Watu Kwenda Kazini Uchi


naked5
Mkazi wa Belarusia akiwa ofisini.

BAADHI ya wananchi wa Belarusia wamekuwa wakienda makazini wakiwa uchi, na baadhi yao wakitupia picha mtandaoni zikiwaonyesha wakiwa uchi kutimiza kauli ya rais wao aliyoitoa siku za hivi karibuni.
Lukashenko-Aleksandr1
Alexander Lukashenko (61).
Kiongozi wa taifa hilo, Alexander Lukashenko (61), anatajwa kama dikteta pekee barani Ulaya ambapo amekuwa rais wa Belarusia toka mwaka 1994 hadi sasa. Lukashenko analaumiwa na watetezi wengi wa haki za binadamu kwa kuminya uhuru wa wananchi wake. Anahesabika kama mtawala dikteta aliyebakia barani Ulaya. Nchi ya belarusia inapakana na Russia, Ukraine, Poland, Lithuania and Latvia.
NAKED..
Lukashenko aliteleza wakati akifungua mkutano wa uwekezaji ambapo alitamka: “Kuwekeza katika tenknolojia ya kisasa, kuruhusu ubinafshaji na kukaribisha wawekezaji, vyote vitatusaidia kama taifa tusonge mbele. Na tayari teknolojia imetupa urahisi wa kutekeleza mahitaji yetu kiufasaha na sasa mtu anaweza kufanya kazi akiwa ‘undressed’ huru”.
Matumizi ya neno ‘undressed’ ndilo lililowababaisha baadhi ya waliolisikia ambapo kwa maana ya kinahau linamaanisha ‘kutovaa nguo au kuwa uchi’, wakati kwa maana halisi linamaanisha ‘kuwa huru’.
Akihojiwa na kituo cha gazeti la Observer, Doroshenko Kostyantyn alisema: “Hatuwezi kupingana na kauli ya rais, lazima twende kazini tukiwa uchi, kutimiza matakwa ya mkuu wetu wa nchi”.
naked 88
Wananchi wa Belarusia wakiwa utupu.
Wananchi wengi wa Belarusia wamechoshwa na vitendo vya matumizi ya mabavu katika utawala vya Lukashenko. Kwa kauli yake hiyo wananchi walio wengi wanatumia mitandao ya kijamii kujipiga picha wakiwa uchi huku wakitamka bayana wanafanya hivyo kutimiza matakwa ya rais wao.
Wananchi wengi wanamwona rais wao kama kituko akiwa kama kiongozi mkuu wa taifa, huku akiteleza mara kwa mara kutamka maneno mazito. Lukashenko aliwahi kutamka ‘ni bora kuwa dikteta kuliko kuwa shoga au kusapoti ushoga’. Kwa Wabelarusia hakuna atakayeisahau kauli hiyo na tayari wameanza kuitekeleza kwa kasi.
nake
Wachambuzi mbalimbali wa kimataifa wanamwona kiongozi huyo kama mtu aliyeanza kupoteza umakini wa kuzungumza mbele ya raia wake, hali inayosababisha kukosea mara kwa mara au kutamka vitu visivyo na mantiki katika jamii.
Wananchi wengi wanatekeleza suala hili ambapo lengo lao kuu ni kumfikishia ujumbe rais wao kwamba amechoka na anahitaji kuachia nafasi kwa wengine waongoze

HATUA TANO ZA KURUDISHA NGUVU ZA KIUME KATIKA NDOA YAKO


Napenda kukukaribisha tena katika jukwaa langu la afya yako, leo hii napenda nizungumzie tatizo ambalo limekuwa ni kubwa sana kupita kiasi kwa kila m, tatizo ambalo linayumbisha na kuweka ndoa matatani, usiwe miongoni mwa watu wenye upungufu wa nguvu za kiume, yote hayo utayaepuka kwa kufuata ushauri huu ulio badili maisha ya watu wengi na bado elimu hii inaendelea kutoa shuhuda kwa kila mtu aliyekuwa na tatizo hili.

Nguvu za kiume hapo zamani za kale na tafiti za kisayansi zinaonesha ni matokeo yanayotokea uzeeni kuwa ni jambo la kawaida kwa umri mkubwa, lakini napenda nikwambie kuwa uzeeni ambao unaambatana na magonjwa sugu kiasi hicho ni moja wapo ya sababu nikuweke kwenye kundi la watu wanaozeeka vibaya. Kwa kawaida binadamu hustahili kuzeeka na magonjwa tunazeeka na magonjwa kwa sababu tunayasababisha sisi

kwa maisha ya kifahari tunayoishi na kusahau kuwa afya yako sio hazina ya milele,unatakiwa kuiheshimu,kuilinda na kuimarisha ili uje ufurahie uzee wako usio na magonjwa. Najua kuwa hadi sasa ukifanya tafiti vijana wa umri wa miaka 20 hadi 30 ndio wanao ongoza kwa kusumbuka na matatizo haya ya nguvu za kiume tofauti na matarajio yetu wote kuwa tatizo hili tunasoma kuwa linawapata wazee, swali la kujiuliza kwa nini sasa vijana tena katika umri mdogo? Ndio maana nimeamua kukuandikia Makala hii ambapo kama ni miongoni mwa watu wanaosumbuka hili tatizo nina uhakika tatizo lako utapata suluhisho kutokana na elimu hii rafiki yangu. Pia najua unaweza ukawa na mchumba wako, unavumulia mengi kuhusu tatizo hili la mwenzi wako, usiwe mkimya kwani inahitaji utashi wa juu sana kumweleza mwenzi wako kuhusu hili swala kwani upungufu wa nguvu za kiume unasababisha msongo wa mawazo wengine hupelekea hadi kuchanganyikiwa hatimaye kupata MAJOR DEPRESSIVE DISORDER na mbali na hivyo husababisha kutokujiamini na woga wa kuwa na mke na hivyo wengi wamejaa wasiwasi na hofu kubwa ya kugunduliwa na mwezi wake kuwa ana tatizo hilo, na wengi wao ni woga sana kutogunduliwa tatizo hilo,ndio maana inapofikia hatua mwenza wako umembaini ni mara chache sana atakubali kuwa kweli ana tatizo hilo. Kwa nini usumbuke na matatizo kama haya wakati msaada wako upo? Usiendelee kusumbuka na tatizo hili kwani umeumbiwa maisha ya furaha na Mungu ni haki yako kufurahia uumbaji wa Mungu, anza leo kushughurikia tatizo kabla halijawa sugu mpendwa msomaji wa Makala hii.

NINI KISABABISHI MSINGI WA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME?

Katika mwili wa binadamu kuna vichocheo aina ya Testosterone ambavyo hutolewa malengo ya kuimarisha utendaji kazi wa ubongo,ufanye kazi katika hali tulivu,kuondoa,kuondoa msongo,kuondoa mstuko wa aina yoyote ,kuimarisha uwezo wa kufikiri,kuimarisha furaha ya mwili wako na hatimaye kuimarisha nguvu za kiume na hatimaye kufurahia tendo la ndoa. Kazi kubwa ya kichecheo hiki ni kuhakikisha mwili wako unakuwa katika hali tulivu kabisa kwa kuutuliza ubongo wako ndipo utafurahia ndoa yako rafiki yangu.

Sasa endapo kichecheo hiki kikivurugika kinasababisha vichocheo vingine kama insulin,leptin,cortisol,vichocheo vya ukuaji pia kuvurugika kwani matokeo ya hitililafu hii mwilini inasababisha KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME kwa sababu vichocheo hivi vinafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, na endapo kimoja tu kikivurugika vyote vinapoteza mwelekeo na tatizo kuwa sugu Zaidi.

Napenda leo nieleze kwa kina kidogo namna gani nguvu za kiume zinapotea kutokana na mvurugiko wa vichocheo hivyo vikuu vitatu kama nilivyo vitaja hapo juu.

1.       TESTOSTERONE

Kichocheo hiki ndio silaha ya mwanaume kwani ndicho kichocheo ambacho kinakufanya uwe na sifa zote za kiume na ndicho kicheo ambacho kinakufanya uwe imara katika tendo la ndoa. Upungufu wa kicheo hiki kinasababisha kupungua kwa matamanio kwa jinsia tofauti,kupungua kwa nguvu za misuli yako kiutendaji,mafuta kurundikana ovyo mwilini( BELLY FAT AND OBESITY)

Lakini pia ijulikane kuwa kichocheo hiki cha testosterone sio kwamba kinapatikana kwa wanaume tu, la hasha! Kichocheo hiki hata wanawake wanacho ingawaje kwa kiwango cha chini sana, endapo kinapokuwa kimepungua kinaweza kumsababishia mwanamke kukosa matamanio kwa jinsia ya kiume wakati wa tendo la ndoa, kukosa nguvu ya misuli ya kuhimili tendo la ndoa (Kuchoka Sana),kuongezeka uzito kupita kiasi na nyama uzembe pia kupunguza uwezo wako katika kufikiri na kumbu kumbu.

NINI KINASHUSHA TESTOSTERONE MWILINI MWAKO?

Moja ya kisababishi kikubwa cha testosterone kushuka kiwango chake ni kwa sababu ya kuwepo na kizuizi cha insulin (insulin resistance) hii inafanya kiwango cha insulin kuwa juu sana na kusababisha testosterone kushuka kiwango chake. Moja ya sababu zinazo sababisha kiwango cha insulini kuwa juu sana ni unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda na pia ulaji wa vyakula vyenye vionjo mbalimbali vitamu vilivyotengenezwa viwandani. Hivyo basi sukari inapokuwa ipo katika kiwango cha juu sana kwenye damu inasababisha utolewaji wa insulin kuwa katika kiwango cha juu pia kwenda kusawazisha sukari irudi kawaida. Hivyo basi matumizi ya vyakula na vinywaji vya sukari nyingi vinafanya mwili upate kizuizi katika utendaji kazi wa insulin na hatimaye testosterone pia kushuka kiwango chake. Najua umejifunza sasa kwa nini watu wanaotumia vyakula vya viwandani,vinywaji vya sukari nyingi,ulaji wa vyakula vyenye mafuta mabaya jinsi gani inasababisha vichocheo vyako kushuka kiwango na unaendelea kusumbuka sana. Napenda kukuambiwa kuwa siku zote watu hawaogopi vyakula vyenye sukari wanaogopa vyakula vyenye mafuta mengi, hio ni fikra potofu sana! Sugar is more addictive than heroin and cocaine, kwa maana nyingine watu ni walevi wa vyakula na vinywaji vya sukari na haipo siku anaweza kuacha haraka. Usihofu kama una tatizo hilo ujue tayari umeshaathiriwa na ulaji wa vyakula na vinywaji hivyo.

2.       INSULINI

Hiki ni kichecheo ambacho hutolewa na kongosho lako ili kwenda kusawazisha kiwango cha sukari mwilini mwako. Kazi kubwa wa maji haya ya insulin ni kuhifadhi nishati ya mwili kwa matumizi ya baadae pale mwili unapokuwa una nishati ya kutosha na hautaki kupoteza nishati ya ziada. Nishati hii huhifadhiwa asilimia kubwa  katika mfumo wa glycojeni mwilini mwako kwenye misuli,ini nk. Sasa inapotokea kiwango chako cha ulaji wa vyakula vya sukari ni kikubwa sana ndivyo kiwango kingi cha insulin kitatengenezwa na kumwagwa kwenye mzunguko wa damu kwenye kuhifadhi sukari ya ziada ambayo haitumiki wakati ule na hatimaye kusazisha kiwango cha sukari mwilini mwako. Kazi ya insulin sio kushusha sukari kama wengi tunavyofundishwa darasani! Kwa nini nasema hivi? Kazi ya insulin ni kuhifadhi nishati ya ziada kwa matumizi ya baadae na hivyo basi kupungua kwa sukari ni matokeo ya kazi ya insulin mwilini mwako.

HEBU SOMA TAFAKURI HII:

Umeingia katika chumba ambacho umekuta harufu mbaya sana ya deodorant spray au perfume punde tu utakapo ingia katika chumba hicho utasumbuka sana na harufu hio kwa muda mfupi na hatimaye unaizoea na kuona ni harufu ambayo haina madhara wala usumbufu kwako.

Huu mfano utakusaidia kujua kwa nini tunasema insulin yako imeshindwa kufanya kazi, na umepata kizuizi katika utendaji kazi wake. Nimesema insulin hutolewa kwa kiwango kikubwa sana kulingana na kiwango cha sukari mwilini mwako, kiwango hiki kingi cha insulin kwenye damu kwa muda mrefu inaweza kupelekea insulin kupoteza kazi yake kiuhalisia. Na pia kitu kingine ambacho kinaweza kupelekea insulin kutofanya kazi ni vipokea insulin kutoitikia kwa sababu ya mafuta mabaya kuleta kizuizi katika vipokezi vya insulin. Vitendo vyote hivi viwili vinasababisha kiwango cha insulin kuwa juu wakati wote  na kama nilivyo eleza mwanzo kuwa kiwango cha insulin kinavyozidi kuwa kingi mwilini mwako kinashusha vichocheo vya Testosterone ambavyo ndio silaha yako mwanaume. Hivyo basi ukiangalia katika maelezo haya utagundua kuwa ulaji wa vyakula na vinywaji vingi vya sukari vinasababisha kiwango cha insulin kuwa juu muda wote ambapo nacho kinapelekea vichocheo vya kiume kushuka na hatimaye unakumbwa na matatizo ya kukosa matamanio kwa jinsia tofauti,msongo wa mawazo,misuli kukosa nguvu muda wote umechoka,uzito kuongezeka kwa kasi sanana wengine hupelekea kumilki vitambi.

Pia kiwango kingi cha insulin kwa muda mrefu kwenye damu kinaweza kupelekea kupata nywele usoni kwa wanawake,mwanaume kuishiwa vinyweleo sehemu kama kifuani,tumboni na maeneo mengine mengi.

3.       LEPTINI

Hiki ni kichocheo cha pekee sana na huwa napenda sana kukizungumzia kwani kinaonesha jinsi gani binadamu alivyo umbwa kwa kutumia teknolojia ya uhandisi wa hali ya juu. Hiki ni kichecheo ambacho kinatengenezwa na seli zinazohifadhi mafuta ambazo zinapatikana kwa wingi kwenye misuli kazi yake kubwa ni kupeleka ujumbe kwenye ubongo katika kuendesha hamu yako unapokuwa una chakula mbele yako, na ubongo huitikia kwa kutoa taarifa ya kutosheka na chakula kwa kujihsi umeshiba na huwezi tena kuendelea na chakula.

Sasa basi ulaji wa vyakula vingi bila mpango vyenye sukari nyingi unasababisha seli za kuhifadhi mafuta (FAT CELLS) kutengeneza kwa wingi leptin ili kwenda kutimiza kazi yake. Kiwango cha insulin na leptin hupanda kwa pamoja kama mapacha vile. Hivyo hivyo kumbuka tafakuri ile pale juu ya perfume, itafikia wakati kiwango kingi sana kinasababisha leptin kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ( KUKATA HAMU YA CHAKULA) hivyo utakuwa una tatizo la kula mlo mkubwa ambao hata siku moja hautosheki na ukitosheka muda si mrefu unahitaji tena kula. Hawa ndio watu wengi ni wahanga wa muda wote wanapenda kula vyakula vitamu vitamu tu, hamu haiishi (Sugary addicted,sugar craving) na wengi huishia kupata matitizo ya kiafya kama kuishiwa nguvu za kiume,uzito kupita kiasi,kitambi na kuishiwa nguvu kabisa ya misuli yote haya ni kwa sababu kiwango kingi cha leptin na insulin kinashusha vicheo vyako vya testosterone.

4.       CORTISOL

Hiki ni kichocheo ambacho hutolewa na mwili pale unapokuwa katika hali yoyote ya mstuko ili kwenda kukabiliana na mtuko huo.

Mfano labda Dr Boaz Mkumbo nilikuwa natembea njiani ghafla nikaona nyoka huyo mkubwa chatu. Mwili utastuka sana na kutoa vichecheo vinavyo enda kupambana na hio hali iliyoshtua mwili wako, mfano cortisol huenda kuongeza kiwango cha nishati ya mwili (glucose) kwenye damu na kuwa na nguvu ajabu ya kumkimbia adui yako aliyepo ,mbele yako.

Cortisol pia hutolewa hata kama mwili wako umekabiliwa na mstuko ndani kwa ndani mfano,sukari mwilini imepungua mwili unatoa cortisol ambayo kazi yake kubwa ni kubadili ile nishati iliyokuwa imehifadhiwa katika mfumo wa glycogen kwenye misuli na ini kuwa sukari na hatimaye kuongeza sukari mwilini mwako.

Sasa tafiti zinasema kwamba,kiwango kingi cha cortisol kwenye damu kinachosababishwa na msongo,mstuko ndani ya miili yetu inayo endelea inasababisha LEPTIN kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ipasavyo.

Na endapo leptin ikishindwa kufanya kazi yake ipasavyo utakuwa una tatizo la kula sana hasa vyakula na vinywaji  vya sukari bila hamu kukata na hatimaye kusababisha insulin kupanda juu na testosterone kushuka chini na hatimaye kuishiwa nguvu za kiume,matamanio kwa jinsia tofauti nk.

Hongera sana kwa kuendelea kusoma Makala hii, hapo juu nilitaka kukueleza tu nini kinatokea endapo unapatwa na upungufu wa nguvu za kiume kwani wengi mmekuwa mkinipigia simu kutaka kujua kwa nini nguvu za kiume sasa, basi leo nazani umejifunza kitu, kama hujaungana nami katika ukurasa wangu facebook hebu bofya like Dr Boaz Mkumbo MD utafurahia Makala zangu nyingi sana nzuri zimeandaliwa kwa ajili yako.

Basi napenda nikupe vitu vikuu 4 vinavyo angamiza watu kukosa nguvu za kiume hawa ndio maadui wako wakuu kuhusu tatizo lako hilo mpendwa, hebu endelea kusoma upate suluhisho lako,ufurahie ndoa yako,

VITU 4 VINAVYO ANGAMIZA NGUVU ZAKO ZA KIUME NA KUKUACHA MWENYE MSONGO WA MAWAZO NA MPWEKE KATIKA MAHUSIANO AU NDOA YAKO

Hebu basi napenda nikwambie hawa maadui wako, najua utashangaa kuwa ni maadui ambao kila siku ni marafiki zako, na hujui kuwa wanaangamiza msingi wa ndoa yako na inaweza kuwa unajua lakini unayapuuzia haya tunayokufundisha kupitia elimu hii ya afya, huwa napenda kuwaambia wagonjwa wangu kuwa afya yako ni mali yako sio ya daktari wala muuguzi wewe ndiye una mamlaka ya afya yako kuiweka sawa au kuidhoofisha. Hivyo napenda kukuambia kuwa afya yako sio hazina ya milele linda sana afya kuliko vyovyote ulindavyo kwani ndio msingi wa furaha zote duniani.

1.       Vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda

Hivi ndio vimekuwa ni vinywaji vya kila siku hasa kwa wafanya kazi, ndio maana wengi ndio wamekuwa wakisumbuka na matatizo haya ya kiafya kwani wanakula vyakula huwa napenda kuviita vya chapuchapu, yani anataka soda ya kuvuta muda ili baadae akale, ndugu yangu nimeongelea jinsi gani sukari nyingi inashusha nguvu za kiume tena kwa kina Zaidi. Wengine huuliza sasa Dr mimi siwezi kabisa kujizuia kunywa soda hata masaa tu, kwani kwenye friji zimejaa, ni kweli huwezi kujizuia kwa sababu tayari umeshakuwa ni mlevi wa sukari (sugary addicted, sugary craving) vyote hivi unaweza kujizuia kwa kukutana na mshauri wa afya lishe atakupa maelekezo mazuri namna gani unaweza kukata sugar craving kiurahis kabisa. Kumbuka kiwango kimoja cha kichecheo kikivurugika vyote vinavurugika hivyo tunatakiwa kulinda sana kiwango cha insulin kuwa katika kiwango kizuri muda wote ili kufurahia ndoa zetu.

2.       Kuepuka kabisa ulaji wa vyakula vya mafuta

Watu wengi sana huwa na fikra potofu kuwa chakula chochote cha mafuta ni kibaya, na hivyo hujizuia sana kula vyakula hivyo kwa kuogopa kunenepa, napenda nikwambie kuwa hakuna adui mkubwa wa magonjwa yote kama SUKARI hivyo vyakula vya sukari ndio chanzo cha magonjwa mengi ya tabia ambayo ni magonjwa sug hapa duniani, ndio chanzo cha uzito mkubwa kupita kiasi,kitambi,shinikizo la damu,kisukai,upungufu wa nguvu za kiume,uvimbe kwenye kizazi,mzunguko mbaya wa hedhi,ugumba,utasa nk hivyo basi kuna usemi unasema “SIO MAFUTA YANAKUFANYA MGONJWA, BALI SUKARI NDIO INAKUFANYA ULEMEWE NA MAGONJWA”

Tafiti zinaonesha kuwa ulaji wa vyakula yenye mafuta kidogo sana tafiti zinaonesha kuwa vichocheo vya progesterone hupungua na kupelekea kupoteza nguvu za kiume na matamanio kwa jinsia tofauti.

3.       Nyama na vyakula vyote vya kusindika viwandani

Napenda kusema kuwa ulaji wa vyakula hivi sio ufahali katika familia yako, bali ni uzembe katika uandaaji chakula katika familia yako, kuna usemi unasema kuwa, ukitaka uishi kwa bajeti kubwa katika familia yako, kula vyakula asili ambavyo babu zetu walikula enzi zile (EAT ORGANIC) ndio maana watu wengi hawapendi kula vyakula asili, wanatafuta vyakula vilivyo sindikwa kwani havina gharama kubwa. Kuna usemi unasema, unapokuwa upo jikoni unandaa chakula chako kwa familia yako, unatakiwa ujiulize kwa nini vyakula hivi vya kusindika vina bei rahisi kiasi  hiki?

Ulaji wa vyakula hivi,siku zote huenda kuangamiza bakteria rafiki (Normal flora) pia wengi hupendelea kuita gut probiotics na unapokuwa umewaangamiza hawa ndio chanzo cha magonjwa yote kwani katika Makala zangu zilizopita nilieza namna gani mfumo wa chakula unaweza kuwa chanzo cha afya bora yako, na chanzo cha magonjwa yote mwilini mwako. Unapokuwa umeangamiza hawa viumbe katika mfumo wa chakula kwa sababu ya vyakula ambavyo wao, hawavitambui, unakuwa ni mtu wakushambuliwa na maradhi nyemelezi yote na kudhoofisha ukuta wa mfumo wa chakula na hatimaye unaweza kuanza kupenyeza sumu (toxins), bakteria wabaya kama E. Coli, vyakula ambavyo havijameng’enywa vizuri na protini zingine kama gluten ambazo ni hatari kwa afya yako. Hivyo kama wewe umekuwa ukisumbuka na nguvu za kiume na umekuwa ni mlaji mzuri sana wa vyakula hivyo, hakikisha una viepuka kuwa mtu unayependa vyakula asili, vitarudisha uhalisia wa mfumo wako wako wa chakula kwa kuondoa tatizo la tumbo kujaa gesi na choo kuwa ngumu.

4.       Sumu mbali mbali kutoka kwenye mazingira

Watu wengi sana wanapokuwa wanazungumzia tatizo la nguvu za kiume wanasahau kuahusisha mahusiano yaliyopo kati ya upungufu wa nguvu za kiume na mazingira yako. Najua kuwa tumekuwa tukijishughurisha na shughuli mbali mbali ambazo zinatufanya tugusane na sumu mbali mbali, mfano madini ya mercury ambayo sasa yapo kila kona katika biashara zetu, madini ya lead haya ni madini mazito na hatari sana kwenye kudhoofisha utendaji kazi wa mwili wako, kukuletea msongo wa muda mefu na mengine mengi ambayo yanapelekea kupoteza nguvu za kiume. Kwa dunia ya sasa ya viwanda huwezi kuziepuka sumu kama hizi mwilini mwako, ni jukumu lako kuhakikisha unajijengea mazoea ya kuondoa sum nzito hizi na mionzi mbali mbali katika mwili wako na hatimaye kuimarisha afya yako.

Najua umejifunza kwa nini sasa una upungufu wa nguvu za kiume au huna kabisa nguvu za kiume basi ningependa ijifunze jinsi gani unaweza kuhakikisha unaondokana na tatizo hili na ukafurahia ndoa yako na mahusiano yako kuanzia sasa, naomba basi nikuokoe katika tatizo hilo kwa kusoma njia tano za kurudisha nguvu za kiume

NJIA SABA ZA KURUDISHA NGUVU ZA KIUME

Najua umekuwa ukisumbuka kila siku kufurahia ndoa yako, hadi imefikia hatua mbaya, najua umekuwa mnyonge na mwoga wa kugundulika kwa mwenza wako kuwa unasumbuka na tatizo hilo, umejaa woga, umegubikwa na msongo wa mawazo na umekuwa ukizunguka kila sehemu upate msaada na hatimaye umekuwa ukitoa pesa bila hata kurudisha furaha ya ndoa yako na nafsi yako! Pole lakini elimu ni bora kuliko yote yaliyokupata ndugu, hebu soma hiki ambacho nimekuwa nikipewa asante kila siku na wagonjwa wangu wewe pia uwe miongoni mwao.

1.       Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi,vya kusindika, vyenye vionjo vya sukari,rangi na radha katika afya yako kwani vyakula hivyo ni adui mkubwa sana wa afya yako hasa wakati unataka kurudisha nguvu za kiume. Kula vyakula asili, nafaka ambayo haijakobolewa,matunda kwa wingi ambayo hayasagwa yenye nyuzi nyuzi nyingi na pia juice ya matunda na mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula asili na utafurahia ndoa yako. Anza kuanzia leo rafiki

2.       Epuka pombe katika maisha yako yote kwani tafiti zinaonesha kwamba pombe inakupa hamu au shauku ya kufanya tendo la ndoa lakini inakunyima uwezo wa kufanya tendo la ndoa! Najua utashangaa lakini ndivyo ilivyo, kuna usemi wa kiingeleza unasema,  “It provokes the desire, but it takes away the performance,”  sio hayo tu mpendwa pombe pia sugu, ni chanzo cha msongo wa mawazo  na kukupelekea kukosa kabisa hamu ya tendo la ndoa

3.       Fanya mazoezi ya kutosha. Watu wengi wamelemewa na magonjwa kwa sababu tu mwili haupati damu ya kutosha kwenda sehemu mbali mbali kama vile ubongo,ini,figo ambazo ndio sehemu zenye kuufanya mwili wako ufanye kazi katika uhalisia wake. Hivyo basi magonjwa mengi ya msunguko wa damu ni pamoja na nguvu za kiume kwani kama hufanyi mazoezi mwili wako unadhofika na kukosa uwezo wa kuhimili ndoa yako pia inapunguza nguvu za kiume. Basi ningependa kuwa kwa wale wazee siku hizi kuna vituo mbalimbali ambavyo vitakusaidia mwili wako kuwa imara na kurudisha uwezo wako katika tendo la ndoa kupitia mazoezi. Unaweza pia kuwasiliana nami nitakupa taratibu za kufuata kukusaidia uanze mazoezi ya viungo kwa kutumia mashine maalumu kwa umri wako ambazo zitasaidia kuimarisha mwili wako. Mazoezi huimarisha mwili wako na kuweka mbali mwili wako na maradhi mbalimbali yanayo sababishwa na uzembe katika mazoezi, usisumbuke kufanya mazoezi yenye kuumiza mwili wako, wasiliana name kwanza kabla ya kufanya lolote.

4.       Rudisha Virutubisho ambavyo vimepotea mwilini mwako

Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinki,chuma, selenium, manganese na vitamin nyingi, kwani madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango stahiki kwani huwezesha viendesha shughuli za mwili yani enzymes kufanya kazi katika kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako.

Unaweza kupata madini haya yote kutoka kwenye mboga za majani kama wewe ni mvivu basi unaweza kunywa juice inayotokana na mboga mboga kama kabeji,spinachi kale, nk. Kwa wale ambao ni kaz sana kuhimili zoezi hilo unaweza kujipatia kirutubisho hicho ofsini kwetu ambacho kina madini yote hayo.

5.       Ondoa mafuta mabaya amabyo yanapunguza utendaji kazi wa mzunguko wa damu, unaweza kuondoa kolestero mbaya mwilini mwako kwa kutumia mafuta ya omega 3 ambayo unaweza kula vyakula vyenye mafuta haya kama samaki kwa wingi, flaxseeds, blackseeds ni baadhi ya vyakula ambavyo vimekuwa vikionekana kwenye nukuu za habari kuwa ni vyakula vyenye uwezo mkubwa wa kusafisha mafuta mabaya  mwilini mwako. Unaweza pia kufika ofsini kwetu kama utahitaji mafuta haya yaliyotengenezwa kitalamu utayapata na yatakusaidia.

6.       Ondoa Sumu kwa kutumia viondoa sumu. Kuna sumu aina kuu tatu ambazo mimi huwa napenda kuziongelea siku zote na kushughurika nazo kwa wagonjwa wangu kama zifuatazo,

        -Sumu ambayo inatokana na mabaki ya hewa ya oksijeni yani Free radicals ambayo ni moja wapo inaweza kuumiza seli za mwili wako na kusababisha seli zako kubadili mtazamo wa ukuaji na kuendelea kuzalishwa seli mbovu na hatimaye zinaweza kupelekea hata kupata kansa.

      -Sumu ambazo tunazipata kutoka katika mazingira yetu ya kazi kwa kukutana na metali nzito kama lead, na mercury ambazo ni kizuizi kikubwa sana katika utendaji wa mwili wako, pia sumu inayotokana na mionzi mbalimbali inayotokana na kuchokozwa kwa miamba ya ardhi ( Earth’s crust)

       -Sumu inayotokana na vyakula tunavyokula ambavyo huenda na kuathiri mfumo wako wa chakula na hatimaye kuharibu ulizi wa mwili wako katika mfumo wa chakula. Afya yako huanzia katika mfumo wa chakula na magonjwa yote huanzia katika mfumo wa chakula.

Basi unaweza kuondoa sumu hizo kutokana na visababishi vyake kama nilivyo eleza. Unaweza ukajipatia huduma hii kwa kutumia njia kuu zifuatazo

-Tunakupatia package ya siku 30 ambayo napenda kuitambulisha kwako pia utumie kama utaona itakufaa kama wengine SEX DRIVE ENHANCING PACKAGE ambayo itakuondolea sumu zote za free radicals na metali nzito za aina zote na kurudisha utendaji kazi wa mwili wako na kurudisha nguvu za kiume.

- Kwa wale ambao umri kidogo umeenda hawawezi kufanya mazoezi vizuri ningependa ufike ofsini kwetu tuje tukusaidie tatizo lako mpendwa.

Najua umejifunza mengi sana kuhusu tatizo la nguvu za kiume, sasa napenda nitimishe kwa kukuambia kuwa suluhisho la nguvu za kiume lipo kabisa ni kuhakikisha tu, unaliondoa tatizo hilo kwa kufuata elimu hii, na kama unaona elimu hii ni muhimu kwako basi unaweza pia kutupigia na kufika kwetu moja kwa moja kupata suluhisho la tatizo lako

Hizi hapa NJIA RAHISI YA KUPATA MIMBA HARAKA KWA MWANAMKE


1. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.
2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia.
3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation. Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive.
4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito.
5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.
6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu 'enjoyable' na sio tendo 'mechanical' kwa ajili ya kutafuta mtoto. Plan a romantic evening or try something different to spice things up. How you are feeling sexually may increase your chances of getting pregnancy. For women a better orgasm may help pull the sperms into the uterus and for men a better orgasm may increase their sperm count.
7.Kufanya mapenzi katika mtindo (style) ambayo itafanya mbegu za kiume zikae kwa muda mrefu ukeni na hivyo nyingi kupanda kuingia kwenye kizazi na kwenda kurutubisha yai. 'missionary position' ni nzuri zaidi, ambapo mwanaume anakuwa juu, epuka positions
za mwanamke kuwa juu kwani hufanya mbegu zimwagike kwa gravity. Jaribu pia kuweka mto chini ya kiuno ili kukiinua na kufanya mbegu ziingie ndani kwa urahisi zaidi.
Kumbuka kuna asilimia 10 - 25 ya couples ambazo zina matatizo ya infertility lakini vipimo havionyeshi tatizo, inaweza kuwa namna ya kufanya mapenzi ndio ikawa shida, jaribu njia hizo 7 juu.

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo katika habari za kitaifa kimataifa, michezo na udaku

Karibu tunakuletea, kilichoandikwa kwenye headlines za Magazeti ya leo Juni 29, usisahau kulike page yetu ya facebook kwa kubofya hapo chini, na kushare habari zetu. 






Tuesday, June 28, 2016

Askari auawa baada ya kupigwa na wafugaji mkoani Tabora.

Watu watatu wameuawa kwa nyakati tofauti mkoani Tabora akiwemo Askali wa Jeshi la wananchi wa Tanzania,(JWTZ)aliyepigwa fimbo na wafugaji akiwa katika ujenzi wa nyumba yake,baada ya kuwalalamikia kuwa, ng’ombe wamevamia katika kiwanja chake na na kuharibu vitu mbalimbali vya ujenzi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Hamis Issa Suleiman,amemtaja marehemu kwa jina la Carritus Mkunozi (35) wa kikosi cha 212KJ,ambapo ugomvi ulitokea baada ya kupishana kauli na wafugaji,na ugomvi kuanza,ambapo alifariki akiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete muda mfupi,akipata matibabu.

Aidha amesema kuwa katika tukio hilo kundi kubwa la ng’ombe zaidi ya mia mbili,waliokutwa katika kiwanja cha marehemu huyo wanashikiliwa, na muuaji mmoja,huku akiwataja marehemu wengine,waliouawa kuwa ni mama mmoja,mganga wa kienyeji aliyepigwa fimbo kichwani baada ya kuwapa kisogo wauaji waliokuwa wamemwomba maji ya kunywa.

Katika hatua nyingine Kamanda Hamisi Issa Suleiman amesema huko kata ya kijiji cha Motomoto Vumilia wilayani Urambo kijana mmoja kibarua ambaye hakufahamika alipigwa ngumi kifuani na kufariki papo hapo, wakati wakigombea mgao wa posho ya kazi yao.

Gesi nyingine yagunduliwa Tanzania

Hifadhi Kubwa zaidi ya Gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania

Tanzania ni miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.

Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.
Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.

Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.

Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.

Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.

''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.

 

Gallery

Popular Posts

About Us