KINGAZI BLOG: 07/23/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, July 23, 2016

Mzee Makamba: Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo

Mzee Makamba anadai kuwa Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo. Na kwa tafsiri ya kiafrika mtu mwenye laana siku zote hufanana na mtu aliyechanganyikiwa. Ayafanyayo huwa kituko kwa wanaomzunguka, huwafanya watu waingiwe na huruma.

Lakini naamini lengo la Mzee Makamba kumsema Askofu Gwajima ni kumuongezea uadui miongoni mwa wanajamii kwa kuanzia na watu wanaosali kwake. Lengo jingine ni kumchongea kwa Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kufunguliwa Kwa Mfumo Wa Udahili Wa Pamoja (CAS) Unaoratibiwa Na NACTE Na Kutangazwa Kwa Majina Ya Waombaji Udahili Waliochaguliwa Kujiunga Na Kozi Za Cheti Na Diploma

Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni  tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku.

Waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.

Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha orodha ya majina  ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe 18 Julai 2016 na 21 Julai 2016. 

Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). 

Waombaji waliochaguliwa nao wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao binafsi au kwa kubofya hapa.Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia.  

Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi za Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.

Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 22 Julai, 2016

VIGOGO, OFISI YA WAKALA WA MISITU TANZANIA (TFS) WATUMBULIWA. PROF Dos Santos Silayo, Kuwa, KAIMU MTENDAJI MKUU WA TFS.


SERIKALI imemuondoa katika nafasi yake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda na wakurugenzi wenzake, katika jitihada za kufumua na kusuka upya shirika hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza hatua hiyo ya serikali jana alipokutana na vyombo vya habari na kuongeza kuwa, watumishi wengine 41 wamehamishwa vituo vya kazi.

Alifafanua kuwa hatua hizo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lililotaka kufumuliwa na kusukwa upya kwa TFS ili kuongeza ufanisi.

Kutokana na hatua hiyo, Waziri Maghembe alisema Profesa Dos Santos Silayo ameteuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS, wakati Kamwenda anahamishiwa Chuo cha Viwanda vya Misitu kilichopo Moshi.

Aidha, Mwanaidi Kijazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Raslimali za Misitu na Nyuki, yeye amekwenda kuwa Mhifadhi Mkuu Amani Nature Reserve na nafasi yake inachukuliwa na Zawadi Mbwambo.

Waziri Maghembe alisema Mohamed Kilongo aliyesimamishwa kazi Januari 5, mwaka huu uchunguzi umeonekana hana hatia na hivyo anaendelea kuwa Mkurugenzi Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu.

Alisema Wizara imeamua Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Gladnes Mkamba ahamishiwe Idara ya Mipango makao makuu na nafasi hiyo kuteuliwa Dk Ezekiel Mwakalukwa, kuwa Kaimu Mkurugenzi.

Aidha Monica Kagya aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, anakuwa Mtafiti Mwandamizi Idara ya Nyuki (Tawiri). Alisema Kagya ni mtaalamu wa masuala ya nyuki, hivyo atahamishiwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, ili ashughulikie utafiti wa masuala ya nyuki.

Pia alisema katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa anakuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Herman Kerayo ambaye anahamishiwa Idara ya Mipango Makao Makuu.

Profesa Ramadhan Kideghesho, yeye anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Mweka wakati Mabula Misungwi aliyekuwa Meneja Mradi Selous, anakwenda Chuo cha Wanyamapori Pasiansi na nafasi yake inachukuliwa na Jaffary Lyimo, huku Robert Mande akipelekwa kuwa Kaimu Mkurugenzi msaidizi Uzuiaji Ujangili.

Waziri Maghembe alisema Majjid Ally ameteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Leseni, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Haji Mpya ambaye amehamishiwa Shamba Jipya Songea kuwa Ofisa Misitu Alisema Julai 18, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikutana na viongozi na watumishi wa Wizara hiyo na watendaji wakuu na watumishi wa TFS na kuagiza kufumuliwa na kusukwa upya kwa wakala huo.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alitaka kuondolewa kwa utitiri wa vituo vya ukaguzi na kuwekwa vituo vichache na kuondolewa kwa ofisi za makontena yanayotumiwa na ofisi ya TFS, badala yake watumishi wanaofanya ukaguzi wasimame mahali pa wazi ili kuondoa mianya ya rushwa na kuweka uwazi katika utendaji.

GIGY MONEY,IDRIS SULTAN MAHABA MOTOMOTO


 

Idris na Gift Stanford ‘Gigy
Gladness Mallya, Risasi Jumamosi
IMEVUJA! Baada ya hivi karibuni penzi la Wema Sepetu na Idris kusambaratika, mwanadada Gift Stanford ‘Gigy Money’ amedaiwa kuchukua nafasi na sasa ni mapenzi motomoto.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba Gigy Money na Idris kwa sasa ni mapenzi motomoto na mwanadada huyo aliamua kutafuta kazi ya utangazaji kwenye Kituo cha Redio cha Choice FM ili amnase Idris ambaye naye ni mtangazaji wa hapo.

 

 “Idris na Gigy Money sasa ni mapenzi motomoto, alimfuata Choice (Choice FM) ili amnase vizuri na kweli amefanikiwa na hata kuachana kwa Idris na Wema kuna chembechembe za yeye kulivuruga penzi lao kwani baada ya kuachana ndiyo mapenzi yamekuwa motomoto sana,” kilisema chanzo.
Hivi karibuni Gigy Money alitundika picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa na Idris huku akisindikizia na maneno kwamba ‘Hainaga ushemeji tunakulaga, leo niweke wazi kabisa jamani huyu ni mume wangu’.

 

 Baada ya kupata habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Gigy Money ili kuupata ukweli ambapo alikuwa na haya ya kusema;
“Idris ameachana na Wema na nilijitahidi kutafuta kazi kwenye redio Choice ili niweze kumnasa vizuri na kweli nimefanikiwa, kiukweli nimejikuta nampenda sana. Sioni tatizo yeye ni mwanaume, mimi ni mwanamke, acha maisha yaendelee,” alisema Gigy.
Jitihada za kumpata Idris aweze kuzungumzia penzi hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.


Global publishers

Bodi ya Mikopo yatoa uamuzi juu ya Wanafunzi ambao hawajarejesha mikopo

Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao. 

Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho.  Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.

Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.

Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao.  Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.

Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:

A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.

Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAR 23 JULAI KWENYE HEADLINES ZA UDAKU KITAIFA, KIMATAIFA NA MICHEZO




 

Gallery

Popular Posts

About Us