KINGAZI BLOG: 05/01/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, May 01, 2016

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo Mei mosi 2016 kwenye,Habari zaUdaku, Kitaifa,kimataifa na michezo.


    MEI MOSI 2016 naanza kwa kukuletea habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye ,habari za kitaifa,kimataifa Michezo na udaku na stori nyingine kali ili ujue kilichojiri dunian

AUDIO | FEROOZ FT. RAYMOND – NIMEJIFUNZA | MP3 DOWNLOAD

Huyu hapa Gigy Money aamua kufunguka kuhusu picha zake za nusu Utupu Mtandaoni..Adai Ndio zinazomuingizia Pesa kila siku


Video queen aliyetokelezea kwenye video kibao za bongo Gigy Money ameamua kufunguka juu ya masinema yake.
Giggy ambaye haishi vituko na kuibua mapya kila siku mitandaoni aliiambia eNewz kuwa yeye wala hajali maneno ya watu na anapenda sana yale mapicha picha yake ya utupu.

“Mimi sipo kwa ajili ya kiki mimi napenda kile ninachokifanya na ndio ninachokifanya mimi nipo kwa ajili ya kutengeneza pesa tu na kipo kiwango ambacho nakitaka nifikie na sasa natarajia kufikia,” alisema Gigy.

Rais Magufuli Aahidi kupunguza kodi kwa wafanyakazi .wote



Rais John Magufuli ameshusha kodi ya mapato ya mshahara (paye) kwa wafanyakazi kutoka asilimia 11 mpaka asilimia tisa. Rais Magufuli alitangaza punguzo hilo leo mjini Dodoma alipokuwa akihutubia kwenye siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa imefanyika Dodoma.

 Amesema wafanyakazi wamekuwa waaminifu katika kulipa kodi ambayo inachangia kwenye maendeleo ya taifa kupitia mishahara yao. Alisema kwa kuwa bado vita dhidi ya wafanyakazi hewa na ufisadi inaendelea, ataangalia namna ya kuboresha mishahara yao hapo baadaye.

 “Niliwaahidi wakati wa kampeni zangu kuwa nitapunguza kodi ya mapato kwenye mishahara yenu; sasa natamka kuwa nashusha kodi kutoka asilimia 11 hadi asilimia tisa. Najua punguzo hilo litakuwa limeacha pengo kwa serikali, lakini tutaangalia vyanzo vingine vya mapato vya kujazia hapo,” alisema Rais Magufuli.

 Kuhusu wafanyakazi hewa, Rais amesema mpaka jana idadi ya wafanyakazi hewa imefikia 10,295. Amesema wafanyakazi hao hewa wamelipwa zaidi ya Sh 11 bilioni na kama wangeendelea kuachwa kwa mwaka mzima wangelipwa zaidi ya Sh 139 bilioni. Rais Magufuli ameapa kuwashughulika popote walipo.

 Pia amewaagiza waajiri wote nchini kuwapa mikataba ya ajira wafanyakazi wao na kuhakikisha wanapeleka michango yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kukosa.
 

Gallery

Popular Posts

About Us