KINGAZI BLOG: 03/21/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, March 21, 2016

Rihanna akasirika kufananishwa na Karrueche


best-beauty-rihannaMwanamuziki Rihanna.
NEW YORK, Marekani
MWANAMUZIKI Rihanna, amekasirishwa na kitendo cha ‘ex’ wake, Chris Brown kumfananisha na wanawake wengine aliowahi kutoka nao kimapenzi.
Hivi karibuni Chris alipost kwenye Instagram picha aliyoiunganisha ikimuonyesha akiwa na

Majaliwa aeleza kisa mwanajeshi kuongoza Kagera


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoboa siri ya kuteuliwa mwanajeshi kuongoza Mkoa wa Kagera, moja ya mikoa iliyoko pembezoni na yenye tishio kubwa la wahamiaji haramu na matatizo ya ardhi.
Hivi karibuni, Rais John Magufuli alifanya uteuzi wa wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara na kumteua Meja Jenerali mstaafu, Salum Mustafa Kijuu kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera.

JK ashiriki mkutano wa uandishi Katiba ya Libya

USHAURI MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE 2015 KUHUSU KOZI MBALIMBALI AMBAZO ZINAWAFAA KULINGANGA NA MATOKEO WALIOYOPATA NA JINSI YA KUOMBA 2016/2017


Habari zenu,
Kwanza kabisa kama kichwa kijielezavyo hapo juu ,leo nimemaua kuzungumizia kuhusu wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2015 na wanatarajia kujiunga na vyuo mbalimbali kwa masomo mbalimbali mwaka wa masomo 2016/2017.

Akothee ft Flavour - Give It To Me [Official Video]


SAY SHAY - EVERLASTING LOVE (AUDIO)

Witnesz ft Ochu shaggy - Sharifa (Official Video )


WITNESS FT OCHU SHEGGY - SHARIFA(AUDIO)


JOSE CHAMELEONE FT BOB JUNIOR - BAKI NAE(AUDIO)

IZOO BIZNESS FT SHAA,BANANA & HANCE PUFF - USIJIOVADOZE(AUDIO)


AMINI - HAWAJUI(AUDIO)


DOWNLOAD HERE

BREAKING NEWS;CCM YASHINDA TENA UCHAGUZI ZANZIBAR.



Tume ya taifa ya uchaguzi zanzibar kupitia mwenyekiti wake Jecha Salim Jecha, imetangaza matokeo  ya uchaguzi mkuu uliofanyika tar 20 march,huku mgombea wa urais kupitia chama cha

BREAKING NEWS; Matokeo ya UCHAGUZI yaanza kutangazwa ZANZIBAR

Image result for breaking news
Zoezi la kujumuisha kura katoka vituo mbalimbali katika wilaya ya CHAKECHAKE kisiwani PEMBA, limeendelea kwa usiku mzima huku matokeo ya viti vya uwakilishi pamoja na UDIWANI

ZOEZI LA UHAKIKI WA WAFANYAKAZI HEWA LAANZWA KUTEKELEZWA


Image result for magufuli
Siku chache baada ya wakuu wa mikoa kuapishwa na Rais John Magufuli, imeelezwa kuwa wakuu hao wametoa agizo la kuhakiki taarifa za watumishi wa umma kwenye mikoa yao.

Agizo hilo la Rais linalenga kubaini watumishi hewa katika mikoa na wilaya nchini. Kazi hiyo imeanza kutekelezwa kwenye baadhi ya hospitali za Serikali nchini.

Taarifa zilizoptaikana jana, zimeleza kuwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke na nyingine za mikoani, watumishi wote wametakiwa kupeleka viambatanisho kadhaa kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zao za ajira.

Chanzo kutoka hospitali ya Temeke kilieleza kuwa viambatanishi hivyo ni pamoja na barua ya ajira, wasifu wa kazi na stakabadhi ya malipo ya mshahara.

Chanzo hicho kilisema kuwa agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na wafanyakazi wanatakiwa kukabidhi viambatanisho hivyo kuanzia wiki hii.

Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema, “Hatuhakiki watumishi wa sekta ya afya tu ni watumishi wote wa umma.”

Alisema watumishi ambao wako nje ya vituo vyao vya kazi, wametakiwa kurejea mara moja kwa ajili ya kazi hiyo.

WATATU WAKUTWA WAMENYONGWA NA KUCHOMWA MOTO- KYELA


Watu watatu wamefariki dunia kwa kunyongwa na miili yao kuchomwa moto ndani ya nyumba ya wageni iliyopo Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Mauaji hayo yamegubikwa na utata kutokana na mazingira ya tukio hilo kuwahusisha wapangaji wa nyumba hiyo usiku wa kuamkia jana.

Mmiliki wa nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Kyela Kati, Boniface Mtengela alisema waliouawa ni watatu kati ya watu wanne waliofika kwa pamoja saa nne usiku jana.

Alisema watu hao walikuwa  wanaume watatu na mwanamke mmoja na waliouawa ni mwanamke na wanaume wawili.

Mtengela alisema wanaume wawili walijiandikisha kwa jina la Ali Hassan na mwanamke la Mariam.

“Mwanamume mmoja alipanga chumba namba 14, mwingine 105 na mwenye mke alipanga chumba namba 15. 

"Waliokutwa wamekufa ni wanaume wawili wa vyumba na 14 na 105 pamoja na mwanamke huku mwanamume mwenye mke akitoroka,” alisema.

Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Kyela, Francis Mhagama alisema uchunguzi wa miili ya marehemu hao umebaini kuwa waliuawa kwa kunyongwa kisha kuchomwa moto baada ya kumwagiwa mafuta ya taa.

Uchunguzi katika eneo la tukio ulibaini miili yao iliungua, lakini chumba na magodoro havikuungua. Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Kyela Kati, Timoth Luvanda alisema usiku wa tukio hilo hakusikika kelele zozote.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi hakupatikana kuzungumzia tukio hilo wala kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba hiyo na kuhojiwa katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kyela.

Mhudumu wa nyumba hiyo, Hagai Yohana alisema mgeni mmojawapo aliondoka kabla ya saa 12 alfajiri akiwa na kidumu na mfuko wa rambo.

Alisema wageni wote waliandikisha kuwa ni wafanyabiashara na hawakuwa na mizigo.

Mzindakaya ataka timu kubuni miradi



MWANASIASA mkongwe nchini, Dk Chrisant Mzindakaya, ameushauri uongozi wa mkoa wa Rukwa kuunda timu ya wataalamu kupendekeza miradi ya maendeleo inayofaa kutekelezwa mkoani humo.
Alipendekeza timu hiyo ijumuishe wataalamu kutoka katika taasisi za fedha nchini na wizarani ambao watatafsiri wasifu wa mkoa huo na kuandaa kitabu kitakachoeleza mikakati ya maendeleo ya mkoa.
“Mikakati hiyo ni pamoja ya namna ya kuanzisha au kuendeleza viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vitakavyoongeza thamani ya mazao kwa kuyasindika,” alisema. Alisema kuwa inasikitisha kuona Mkoa wa Rukwa ulio miongoni mwa mikoa inayolima mahindi kwa wingi unaagiza mbegu bora kutoka nje ya nchi au kuletewa za bandia na kusambazwa kwa wananchi.
Alilieleza gazeti hili kuwa, maendeleo ya mkoa huu hayatakuja kwa kutegemea watu wengine walioko nje ya mkoa. Aidha, alishauri wafanyabiashara wa kati na wakubwa mkoani humo wakutane kutambuana ili watoke kwenda kutafuta wawekezaji katika miradi mbalimbali mkoani Rukwa.
Alisisitiza kuwa mageuzi ya maendeleo lazima yafanywe na wazawa wenyewe badala ya kukaa kusubiri watu kutoka nje ya mkoa. “Mkoa umeshafanya makongamano mawili (Julai , 2007 na Novemba 2013) na mahudhurio yalikuwa ya kuridhisha, lakini matokeo yake sio mazuri kwa kuwa hakuna mwekezaji kutoka nje aliyeonesha nia wala kuja kuwekeza mkoani kwetu,” alisema Mzindakaya.
Alisema, jibu la kweli na rahisi ni wawekezaji kuja kutoka mikoa mingine, lakini ni vigumu kama hakuna msukumo wa vipaumbele na fursa za uwekezaji zilizo wazi hasa kwa mkoa huo ambao kijiografia uko pembezoni.
Mzindakaya alisema mkoa huo una zaidi ya viwanda 30 vidogo vya kusindika alizeti katika hatua ya kwanza, hivyo kusababisha wananchi kuendelea kutumia mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
Alikumbusha kuwa mwaka 1974 mkoa wa Rukwa katika viwango vya mapato na maendeleo ulikuwa wa 18 kati ya mikoa 20 iliyokuwepo nchini, baada ya miaka minne hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliutangaza kuwa miongoni mwa mikoa minne inayozalisha mahindi kwa wingi nchini.
Alieleza kuwa hayo yaliwezekana baada ya viongozi wa Serikali na wabunge kuwashirikisha wananchi kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo ambayo mkoa unajivunia hadi sasa.

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo March 21 2016 kwenye, Udaku, kitaifa,kimataifa na michezo


March 21 2016 naanza kwa kukusogezea post ya habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye , Michezo na kitaifa na kimataifa ili ujue kinachoendelea. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook/tanzaniampya news blog na twitter/TZmpyasasa,

Mwandishi wa DW aliyetoweka apatikana

Salma

  

                              Salma alikamatwa na watu wasiojulikana Ijumaa
Mwandishi aliyewakilisha kituo cha redio cha Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) visiwani Zanzibar Salma Said na ambaye alitoweka Ijumaa, amepatikana.
Kamanda wa polisi wa Dar Simon Siro amethibitisha kupatikana kwa mwanahabari huyo.
Chanzo cha habari kilizungumza na Mume wa Salma Said, Bw Ali Salim Khamis, ambaye amesema kwa sasa Salma yumo anatoa maelezo kwa polisi Dar es Salaam

Fuatilia sehemu ya 3 ya hadithi ya mapenzi inayoitwa -TARATIBU MPENZI

TARATIBU MPENZI-Sehemu ya 3


Mtunzi;Geofrey Malwa
Mawasiliano;0712507115
Kumbe alikuwa ni Nelson,alimbananisha mlinzi kwenye ile kona huku akimkunja shati na kumkandamiza kwenye shingo yake maeneo ya koromeo na kumtolea macho kwa ukali,,
,,,pochi yangu iko wapi?,,
 

Gallery

Popular Posts

About Us