KINGAZI BLOG: 05/30/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, May 30, 2016

Wengine tena waongezeka wafikia saba,Bunge limeamua kuwafungia kushiriki vikao vya bunge vilivyobaki.


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge limepitisha azimio la  kuwasimamisha kuhudhuria vikao vya Bunge baadhi ya wabunge wa Kambi ya Upinzani waliohusika katika kufanya vitendo vya vurugu ndani ya ukumbi na kudharau Mamlaka ya Spika Januari, 27, 2016.

Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Mhe.Kabwe Zubeiri Ruyangwa Kabwe, Mhe.John Heche, Mhe.Halima Mdee,Mhe.Tundu Lissu, Mhe.Halima Mdee, Mhe.Pauline Gekul  na Mhe. Ester Bulaya.

 

 Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6).

Akisoma adhabu hizo Mwenyekiti wa kamati hiyo yenye wajumbe 15 Mhe.George Huruma Mkuchika amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na Kamati hiyo kwa kuwaita na kuwahoji wahusika ulibaini kuwa wabunge hao walitenda kosa kwa kukiuka kanuni zinazoliongoza bunge hilo.

 

 Imebainishwa kuwa Mhe.Zitto Kabwe alivunja masharti ya Kifungu cha 24(c), (d) na (e) cha Sheria ya Haki na Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na Kanuni ya 60(2) na (12) , 74(1) na (b) kwa kusimama na kuzungumza bila kufuata utaratibu na kudharau mamlaka ya Spika.

Kamati hiyo ilibaini kuwa Mhe.Godbless Lema, Mbunge wa Arusha alivunja Masharti ya kifungu cha 24 (c),(d) na (e) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 pamoja na Kanuni ya 74(1) (a) na (b) ya kanun hiyo Kudharau Mamlaka ya Spika.

Kwa upande wa Mhe.John Heche alivunja kanuni ya 72 (1) na 68(10) ya kanuni za Bunge kwa kuendelea kusimama na kuomba mwongozo kwa jambo ambalo limekwishatolewa mwongozo na kuongeza kuwa vitendo hivyo vilivuruga shughuli za Bunge.

Kwa mujibu wa maelezo ya kamati hiyo Mhe.Halima Mdee, Mhe.Tundu Lissu,Mhe Pauline Gekul  na Mhe.Ester Bulaya walivunja masharti ya kifungu cha 24 (c), (d) na (e) cha sheria ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na Kanuni ya 72 (1)68 (10), 60(2) na 12 na 74(1) (a) na (b) kwa kusimama na kuendelea kuomba mwongozo kwa jambo ambalo limekwishatolewa uamuzi, kuzungumza bila kufuata utaratibu na kudharau Mamlaka ya Spika.

Kufuatia uchunguzi huo Bunge kupitia kamati hiyo limeazimia kuwa Mhe. Ester Bulaya na Mhe.Tundu Lisu wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge la Kumi na Moja vilivyobaki kuanzia tarehe 30 Mei , 2016 pamoja na vikao vyote vya Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi na Moja kwa kuwa walipatikana na makosa ya ukiukwaji wa Kanuni na kuonyesha dharau kubwa kwa mamlaka ya Spika.

Aidha, Bunge limeazimia kuwa Mhe. Pauline Gekul, Mhe.Godbless Lema, Mhe.Zitto Kabwe na Mhe Halima Mdee wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge kuanzia tarehe 30 Mei 2016.

Aidha  Bunge limeazimia Mhe.John Heche asihudhurie vikao kumi mfululizo vya Mkutano wa Tatu wa Bunge hilo kuanzia Mei, 30, 2016 kwa kuwa alipatikana na kosa moja na pia kwa kuwa alitoa ushirikiano kwa kamati kwa kufika na kujibu maswali yote kama alivyoulizwa pamoja na kuheshimu vikao vya kamati na Mwenyekiti aliyeongoza vikao hivyo.

Pamoja na adhabu hizo Kamati hiyo imetoa maoni na mapendekezo kuwa Bunge liandae mafunzo ya kutosha kwa wabunge wote kuhusu matumizi ya uzingatiaji sahihi wa kanuni sahihi wa kanuni za Kudumu za Bunge hasa kanuni za majadiliano ndani ya Bungeni.

Aidha, Kamati hiyo imesema kuwa ipo haja ya kutungwa kwa kanuni za maadili kwa wabunge wote kama kifungu cha 12 A Cha Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kinavyoelekeza ili kuweza kudhibiti nidhamu kwa wabunge kwa kuhakikisha heshima na hadhi ya Bunge inadumishwa.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge wakichangia kwa nyakati tofauti kuhusu suala hilo wamesema kuwa ipo haja ya Bunge kurudisha heshima yake kwa wabunge wote kuheshimiana na kutoa michango yenye staha kwa kuzingatia nafasi walizonazo katika jamii.

Wamesema kuwa michango wanayoitoa ndani ya Bunge hilo lazima ijikite katika masuala yanayowahusu wananchi wanaowawakilisha badala ya mambo yanayochochea vurugu na kulifanya Bunge lipoteze heshima yake katika jamii.

Aidha, wabunge hao wamekubali kwa kauli moja kuanza upya kuzingatia kanuni zinazoendesha vikao vya Bunge huku wakimtaka Spika wa Bunge au Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutosita kuchukua hatua za haraka kwa mbunge yeyote atakayekiuka utaratibu na kanuni zilizowekwa.

Kesi ya Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Zanzibar Kufumaniwa Akifanya Mapenzi na Mtoto Wake Yatupiliwa mbali



Kesi ya Faki Dadi Faki yatupiliwa nje maana binti ni mtu mzima ana miaka 21 though yuko form 6. Na sio mtoto wa kumzaaaa so hakuna incest.Na wala binti hakumshtua mamake ilikuwa Ndo mchezo wao mama mtu aliwafatilia mwenyewe.. Hata ile video ukiangalia utamuona binti anavaa chupi huku anapiga kelele analia... Mtu alie panga na manake Kweli anavua Hadi chupi??? Mimi kilichonistua kuhusu story ya Kuwa binti alisema Kwa mamake ni jinsi alivyo Kuwa analia Kwa mshtuko huku akivaa chupi..So conclusion hapa ni kwamba wooooooote wawili they are to blame because binti ni mzeee mzima.. Wengine 21 Tayari tuna mimba za kina Bhoke, 21 ni mtu na akili zake timamu za kujua asitembeeeee na babake.... Angekuwa 16 tungemtetea Ila Kwa 21 Hapana aiseee....

Tundu Lissu na Esther Bulaya Wapigwa marufuku Kuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya Bunge.

Tundu Lissu na Esther Bulaya wafungiwa kuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya bunge la bajeti na bunge lijalo la mwezinwa tisa. Vilevile Zitto Kabwe, Pauline Gekul, Godbless Lema na Halima Mdee wafungiwa kushiriki vikao vilivyobaki vya bajeti na John Heche afungiwa kuhudhuria vikao kumi mfululizo vya bajeti kuanzia leo.
Huu ni uamuzi wa kamati Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge chini Mh George Mkuchika (Mb)

SUALA LA POMBE AINA YA KIROBA DAWA ZA KULEVYA,SERIKALI YAFANYA MAAMUZI HAYA.




Hakuna kitu kinachowaharibu vijana wa Tanzania kama madawa ya kulevya na viroba.
January
Lakini wakati vita dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya ikionekana kuendelea kuwa ngumu, serikali inakaribia kupata ushindi kwenye vita dhidi ya viroba. Serikali imetangaza kupiga marufuku utengenezaji, usambazaji na uingizaji wa plastiki nchini hadi kufikia mwaka 2017.
Hiyo inamaanisha kuwa viroba vitakuwa vimechimbiwa kaburi lake moja kwa moja. Uamuzi huo umetangazwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba wakati akizungumza na waandishi wa habari Jumapili.
Alidai kuwa mifuko hiyo ambayo mingi hutolewa bure imekuwa mstari wa mbele katika uchafuzi wa mazingira nchini. Alisema uamuzi huo utaanza kutekelezwa ili kuwapa muda wafanyabiashara wanaoingiza mkate wa kila siku kupitia biashara hiyo kutafuta nyingine mapema kabla mambo hayajawa magumu kwao.
Pamoja na kuharibu nguvu kazi ya taifa, viroba ambavyo hutumiwa na vijana wengi katika muda ambao walipaswa wafanye kazi, mifuko yake imekuwa ikichafua mazingira ikiwa ni pamoja na kuziba mifereji mbalimbali ya kupitisha maji.
Hata hivyo kuzuiwa kwa mifuko ya plastiki kutawafanya watengenezaji wa vilevi vya bei chee kufikiria njia mbadala ya kufungasha zaidi ya chupa zilizoeleka.  

BONGO 5

Habre ahukumiwa kifungo cha maisha jela.


Image copyrightAFP
Image captionHabre alipatikana na makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu , ubakaji na utumwa wa ngono.
Aliyekuwa rais wa Chad Hissene Habre amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika kwenye uhalifu dhidi ya ubinadamu , ubakaji na utumwa wa ngono.
Hissene Habre alihusika moja kwa moja katika uhalifu huo ambao ulifanyika wakati akiwa rais wa Chad.
Waathiriwa waliokuwa ndani ya mahakama wakati wa kusomwa kwa hukumu hiyo mji Dakar nchini Senegal, walishangilia wakati jaji alimaliza kusoma hukumu.
Bwana Habre anatuhumiwa kwa kuamrisha mauaji ya watu 40,000 wakati wa utawala wake miaka ya 80, madai ambayo ameyakana
Habre alikamatwa nchini Senegal , na kupelekwa uhamishoni mwaka 2013.

BBC

PICHA 8: Wabunge walivyoamriwa kutoka bungeni baada ya kufukuzwa kwa wanafunzi UDOM

Naibu Spika Tulia Ackson ameamuru Wabunge kutolewa nje ya bunge baada ya baadhi ya Wabunge hao kusimama kupinga kitendo cha bunge kakataa kujadili suala la Serikali kuwataka wanafunzi wa UDOM kurudi kwao ndani ya saa 24 kufuatia mgomo wa Walimu unaoendelea kwa sasa.
AW1A0974
Baadhi ya wabunge wakionekana kujadili jambo
AW1A0973
AW1A0917
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia alivyosimama kuainzisha hoja hiyo
AW1A0956
Mbunge wa Arumeru Joshua Nassari akifafanua zaidi
AW1A0959
Baadhi ya wabunge wakitoka nje
AW1A0960
AW1A0987
AW1A0986
AW1A0984

VIDEO: Waziri Ndalichako katolea ufafanuzi kufukuzwa kwa wanafunzi wa UDOM


Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ilitangaza kuwafuza jumla ya wanafunzi 7802 kutoka Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kufuatia mgomo wa Walimu unaoendelea hivi sasa. Waziri Joyce Ndalichako amesimama Bungeni leo kuongelea suala hilo.

ULIIKOSA HII? ALICHOKIONGEA MBUNGE JOSHUA NASSARI BAADA YA BUNGE KUKATAA KUJADILI WANAFUNZI KUFUKUZWA CHUO

MILLARD AYO

Bunge Laahirishwa Baada ya Wabunge wa Upinzani Kumgomea Naibu Spika Kwa Kukataa Hoja ya Wanafunzi 7000 Waliofukuzwa UDOM


Naibu Spika wa Bunge ameahirisha Bunge kabla ya muda wake baada ya wabunge kutaka kujadiliwa suala la wanafunzi wa Udom kufukuzwa chuoni wakati hawana kosa.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari aliomba mwongozo na kutaka sakata la wanafunzi hao lijadiliwe lakini Naibu Spika, Tulia Ackson alisema jambo hilo haliwezi kusitisha shughuli za Bunge hivyo haliwezi kujadiliwa kwa wakati huo.

Kauli hiyo iliwanyanyua wabunge wa upinzani na baadhi ya wa CCM wakipinga kauli hiyo huku wakiwa wamesimama jambo ambalo lilisababisha kuaihirishwa kwa Bunge hadi saa 10:00 jioni huku akiagiza kukutana kwa kamati ya uongozi ya Bunge

Kimenuka Bungeni, Ni Kuhusu Wanafunzi 7000 wa UDOM Waliotimuliwa.mjadala mkali waibuliwa ni virugu tupu.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali itikadi ya vyama vyao, leo wametoka nje ya ukumbi wa bunge hilo baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kukataa kujadiliwa kwa kauli ya serikali kuhusu wanafunzi 7000 wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) waliosimamishwa.

Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kutekeleza agizo la Maziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako hivi karibuni kiliwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke chuoni hapo mara moja.

Kambi ya upinzani iliwasilisha hoja kwa Naibu Spika, Tulia Ackson ili kulishinikiza bunge kuijadili kauli ya serikali kuhusu wanafunzi hao waliotimuliwa ambapo Naibu Spika alikataa kusikilizwa hoja hayo ndipo vurugu zikaanza na kumlazimu Naibu Spika kufunga Kikao cha Bunge kilichokuwa kikiendelea.

Juzi, lilitolewa tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kuondoka chuoni hapo. Tangazo hilo lilieleza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao kurejea majumbani na wataelezwa mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alitafutwa vyombo vya habari na alipotakiwa kufafanua suala hilo, alisema kwa ufupi kuwa suala hilo lipo lakini akaelekeza apigiwe simu Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrice Baltazal kwa maelezo zaidi.

Baltazal alipotafutwa alisema kusimamishwa kwa wanafunzi hao kulitokana na agizo la Serikali na wametakiwa kulitekeleza.  Kuhusu lini na nini hatima ya wanafunzi hao, alisema bado hawajui hadi hapo watakapoelekezwa vinginevyo.

Hata hivyo, kulikuwa na malalamiko kwa wanafunzi hao juu ya namna walivyopewa taarifa za kusimamishwa masomo yao kwa ghafla na kutakiwa kuondoka.

Kozi ya stashahada ya ualimu wa sayansi, ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM pekee.  Waliokuwa na sifa za kujiunga na kupewa mikopo ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kufaulu vizuri masomo ya sayansi.

Wanafunzi hao waliokuwa wamekopeshwa na Serikali wamesimamishwa siku mbili baada ya wenzao zaidi ya 480 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph kusimamishwa baada ya kubainika hawakuwa na sifa za kudahiliwa.

Rais JPM amteua Mama Makinda kuwa Mwenyekiti Bodi ya NHIF.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo Mhe. Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Uteuzi wa Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge Ia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza tarehe 25 Mei, 2016.

Mhe. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology -DIT).

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro. Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.



Haya hapa Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 30




Wahamiaji 700 wafa maji baharini kwa muda wa siku 3

Umoja wa mataifa unasema kuwa huenda wahamiaji wapatao 700 wanahofiwa kufariki katika kipindi cha siku tatau zilizopita katika bahari ya Mediterranean.
Msemaji wa Shirika la umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi, Carlotta Sami, amesema kuwa mashua kadhaa yalizama katika maeneo ya kusini mwa Italia Jumatano usiku ikiwa na wahamiaji hao.

Wahamiaji waliokololewa juma lililopita kutoka katika boti moja kwenye bahari ya Mediterranea, wamewaambia wafanyikazi wa makundi ya uokoaji kuwa, waliona chombo kimoja cha baharini kilichojaa wakimbizi kikizama.

Juma lililopita pekee, zaidi ya watu 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterranean.
Shirika moja la uokoaji la Save the Children, limeiambia BBC kuwa manusura hao walisema kuwa walingoa nanga katika msafara wa maboti matatu Jumatano usiku kutokea Libya.

Maafisa wa Polisi wa Italia wanasema waliwahoji wahamiaji hao waliofika mjini Sicily hapo Jana Jumamosi.

Juma lililopita pekee, zaidi ya watu 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterranean.

DIAMOND PLATINUMZ AKIONYESHA MENO YAKE YA DHAHABU.

Diamond Platnumz Na  Team yake ya wasafi walikuwa DALLAS kwaajili ya show kunayo moja ya video ambayo alipost instagram meneja wa diamond ilionyeshaPlatnumz akiwa ameweka meno ya Dhahabu.Tumezowea kuona wenzetu marekani wakiwa wanapenda kuweka hivyo na imeshakuwa kama fashion kwa super stars wa marekani ,Unakumbuka msanii AY  pia alishawekaga meno ya dizaini hii.

Takriban 17 Wafariki Kwenye Ajali ya Moto Ukrain


Takriban watu 17 wanahofiwa kufariki baada ya moto mkubwa kutokea katika jumba moja la makaazi ya kuwahudumia wakongwe, karibu na mji mkuu wa Ukraine, Kiev.

Wakuu wanasema kuwa idara ya huduma za kuwaokoa watu ilifaulu kuwaokoa watu wengine 17, watano kati yao wamekimbizwa Hospitalini, wakiwa na majeraha mabaya ya moto.

Taarifa kutoka huduma ya zima moto mjini humo, zinasema kuwa moto huo ulitokea mapema leo Jumapili, katika jumba moja la kibinafsi lililoko karibu na makao hayo, ambayo yalikuwa yakiwahudumia kwa muda watu 35, kutoka katika kijiji kimoja kilichoko hapo karibu.

Lori laparamia kituo cha masi yaendayo kasi Dar.



Gari  lenye namba za  usajili T 369 BUZ linalomilikiwa na DAWASCO likiwa limeparamia kituo cha mabasi

baada ya gari hilo kukosa mwelekeo na kugonga kituo hicho na kujeruhi abiria watatu waliokuwa kituoni hapo. Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 2 usiku jana eneo la Mbuyuni, Barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam





 

Gallery

Popular Posts

About Us