KINGAZI BLOG: 06/04/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, June 04, 2016

Makonda aomba boti za kivita kutoka China.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameomba boti za kivita kutoka nchini China ili kusaidia ulinzi katika ukanda wa bahari ya Hindi.

Aliomba boti hizo Dar es Salaam jana wakati alipotembelea boti ya Jeshi la Wanamaji kutoka China waliokuja nchini kwa ziara ya kirafiki wakiwa wametoka kutekeleza jukumu la kushiriki katika ulinzi katika Ghuba ya Aden.

Alisema upatikanaji wa boti hizo utasaidia kudhibiti wanaoingiza na kushusha mizigo kwa njia wa magendo sambamba na wanaovamia watu na kupora mali za watu katika fukwe hapa nchini.

Makonda alisema kuna nyumba zilizo kama maghala ambayo hayafunguliwi mchana, yanaingiza mizigo usiku na kuisababishia serikali hasara kwa kutoingiza kodi, hivyo boti hizo zitakazokuwa za kisasa zitakuwa msaada mkubwa kwa Polisi katika Kanda ya Dar es Salaam, kufanya ukaguzi katika ukanda wa bahari ya Hindi.

“Naomba mtusaidie boti kama tatu au nne ambazo tunaamini zitasaidia kuimarisha ulinzi, na kuhakikisha vitendo vya uhalifu katika bahari unatoweka kabisa,” alisisitiza.

Alisema pia serikali ya mkoa imezungumza na Balozi wa China nchini kuhusu kuanzishwa kwa kituo kitakachofundisha polisi 300 watakaokuwa na uwezo wa kufika sehemu yoyote ya mkoa linapotokea tukio ndani ya dakika tano.

Alisema kuanza kwa mpango huo mkoa utakuwa wa kwanza kwa Bara la Afrika kuwa na askari wa aina hiyo, hivyo serikali ina wajibu wa kulishughulikia na kufanikisha mchakato huo kwa askari wa nchi kavu na hata majini.

Mkuu wa Tawi la Mipango la Maendeleo Jeshini, Meja Jenerali Simon Mumwi alisema ziara hiyo itawasaidia kubadilishana uzoefu na wanamaji kutoka nchini kwao na taarifa mbalimbali huku akiahidi kudhibiti wa matukio ya kihalifu, hasa katika ukanda wa bahari.

“Niseme tu bahari yetu ni salama na jeshi la wanamaji lipo wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi,” alisema Mumwi.

Balozi wa China nchini, Lu Youqing alisema ujio wa meli hiyo ni ishara ya njema ya mwendelezo wa ushirikiano mzuri kati ya China na Tanzania uliodumu tangu enzi za utawala wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Waziri aomba majina ya majipu ya BoT

WAZIRI wa Fedha, Dk Phillip Mpango, amemtaka Mbunge wa Tabora Kaskazini, Almas Maige (CCM) kumpa ushahidi ikiwemo majina ya wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), aliowatuhumu kufanya biashara na mwajiri wao.

Dk Mpango alisema hayo Jumatano usiku alipokuwa akijibu hoja za wabunge kuhusu Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango na kuongeza kuwa akipewa ushahidi huo, ataufanyia kazi.

Awali katika mchango wake, Maige alisema anao ushahidi wa maandishi (huku akiwa ameushika), unaoonesha kuwa kati ya mashirika ya umma yanayovunja Sheria ya Manunuzi, BoT ipo.

Alidai kuwa Sheria ya Manunuzi imetoa fursa ya kuanzishwa kwa vitengo na idara za manunuzi (PMU), lakini fursa hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na vijana wa vitengo, hivyo kuiibia Serikali.

Kwa mujibu wa madai ya Maige, katika benki hiyo kuna vijana wamefungua makampuni ambao wamekuwa wakiyatumia kuomba zabuni za benki hiyo na kuyalipa.

Mbali na tuhuma hiyo, Maige ambaye alitangaza maslahi kuwa yeye ni mkandarasi wa daraja la kwanza, alidai pia kuna vijana wengine wamekuwa wakitoa zabuni kwa kampuni za nje ya nchi, ili watumie zabuni hiyo kupata safari za nje.

Alidai kuwa vijana hao baada ya kutoa zabuni kwa kampuni za nje, hutengeneza safari za kwenda kufanya uhakiki (due diligence) katika nchi zinakotoka kampuni hizo, ambako huko hupokea rushwa.

Katika kuthibitisha hilo, Maige alidai kuwa vijana hao wamediriki kutoa zabuni kwa kampuni iliyofungiwa na Mamlaka ya Manunuzi ya Umma Tanzania (PPRA).

Akijibu hoja hiyo, Dk Mpango alisema tuhuma hizo ndio kazisikia bungeni, hivyo hana uhakika ila akipewa ushahidi ataufanyia kazi kwa kuwa, utumbuaji majipu umesaidia kuongeza mapato na kutoka mfano wa makusanyo ya Sh trilioni moja kila mwezi.

Hivi karibuni, Serikali ilisitisha utoaji wa Sh bilioni 925 zilizokuwa zimeidhishwa na BoT kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madeni ya Serikali.

Mbali na hilo, Serikali iliagiza Kitengo cha Madeni ya Nje ambacho awali kilikuwa chini ya BoT na baadaye kupelekwa wizarani, kirejeshwe mara moja ili kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.

Kabla ya agizo hilo, ilielezwa kuwa malipo hayo yalikuwa yameidhinishwa na BoT kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madeni mbalimbali lakini Serikali ikaagiza fedha hizo zirejeshwe Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki upya.

Lulu DivA na Gigy Money Wapeana Makavu Live


WAUZA nyago kwenye video za Kibongo, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’ hivi karibuni wamechimbana mikwara na kupakana shombo kila mmoja akimuona mwenzake kituko kutokana na maneno anayoyasikia juu yake.
Ishu nzima ilianza baada ya mwandishi wetu kupata ubuyu kutoka kwa mmoja wa watu wa karibu wa Lulu Diva kuwa anamhofia Gigy Money kumfunika katika gemu wanalofanya.


Baada ya mwandishi wetu kupewa ubuyu huo alimwendea hewani Lulu, aliposomewa  madai hayo mwanadada huyo alisema;

“Nani kakwambia hivyo? Siwezi kumhofia Gigy kwenye kile ninachokifanya, hana kitu chochote cha kunifanya nimhofie maana ni mtu wa kawaida sana kwangu.”

Kwa upande wa Gigy alipotafutwa alisema; “Siwezi kupigizana kelele na huyo demu, anatafuta kiki kupitia kwangu lakini hawezi kuipata hata kwa dawa, haniwezi kwa kila kitu, akajipange sana na akae akijua simuogopi.”

Global Publishers

Magazeti ya Leo Jumamosi ya Juni 4, kwenye habari za kitaifa,kimataifa,udaku na michezo




 

Gallery

Popular Posts

About Us