KINGAZI BLOG: 08/08/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, August 08, 2016

HEBU  JIONEE  WASOMI WETU NA UCHAFU WANAOUFANYA KWENYE KUMBI ZA STAREHE BAADA YA KUMALIZA MITIHANI 👇👇👇







Toa maoni yako hapo chini👇👇👇

Simu milioni 900 za Android ziko hatarini, zicheki hapa!


Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani.

Upungufu huo unaowapa wadukuzi mlango wa nyuma wa kuiga herufi za siri uligunduliwa baada ya watafiti wa hali ya ubora wa programu Checkpoint walipojaribu kusuluhisha hitilafu iliyowezesha kirusi kuambukiza makumi ya mamilioni ya simu zilizokuwa na programu zilizoundwa na kampuni moja ya Marekani Qualcomm.


Kampuni hiyo inayounda programu za simu imeuza programu hiyo kwa watengenezaji wa simu milioni 900.

Hilo linamaanisha kuwa simu milioni 900 zipokatika hatari kubwa ya kudhibitiwa na wadukuzi.

Aina ya simu zilizoathirika

BlackBerry Priv na Dtek50Blackphone 1 na Blackphone 2Google Nexus 5X, Nexus 6 na Nexus 6PHTC One, HTC M9 na HTC 10LG G4, LG G5, na LG V10New Moto X ya MotorolaOnePlus One, OnePlus 2 na OnePlus 3Samsung Galaxy S7 na Samsung S7 EdgeSony Xperia Z Ultra

Mkuu wa kampuni hiyo ya kutathmini ubora wa programu katika kampuni ya Checkpoint Michael Shaulov, anasema kuwa

”hakuna ushahidi kuwa tayari simu hizo zimeathirika ila kwa mtizamo wetu ni kuwa mlango uko wazi kabisa mtu yeyote mwenye ufundi na ubora kama wangu hivi anafahamu waziwazi kuwa hakuna hata kizingiti cha kumuibia mtu herufi za siri katika simu hizo tulizotaja hapo juu”

”upungufu unamwezesha mtu wa tatu kumpokonya mmiliki wa simu udhibiti kwani anaweza hata akabadilisha herufi za siri bila yako wewe kujua”

”Ni hatari sana , ni kama mtu amejenga nyumba akaweka mle ndani mali ya thamani ya juu kisha akaondoka akiwa ameacha mlango wake wazi”alisema Shaulov.

Checkpoint tayari imeanza kutoa programu zenye uwezo wa kudhibiti simu hizo na tayari wameipa kampuni ya Qualcomm mbinu za kudhibiti simu hizo.

Njia moja ya kuimarisha usalama wa simu wanasema ni kununua programu kutoka kwa soko maalum la Google Play.

Qualcomm imenyamaza kimya kuhusu ripoti hii iliyotolewa na Checkpoint.

Kiwanja Cha Ndege Dodoma Kukamilika Mwishoni Mwa Agosti

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa vitendo wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Imeelezwa kuwa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege  cha Dodoma utakamilika mwishoni mwa mwezi Agosti ili kuruhusu ndege za abiria sabini mpaka tisini kuweza kutua na kuruka na hivyo kurahisisha usafiri wa anga kwa ukanda wa kati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa baada ya  kutembelea  kiwanjani hapo kukagua hatua ya mwisho ya ujenzi iliyofikiwa ambapo amesema kasi ya Mkandarasi Chicco anayetekeleza kazi hiyo inaridhisha katika kuhakikisha kiwanja hicho kinakamilika kwa muda na kwa viwango vilivyokubalika.

Amesema mpaka sasa ni asilimia themanini ya kazi iliyotekelezwa kwa siku arobaini na tano tangia kuanza ukarabati hivyo kasi iliyotumika kwenye kiwanja hiki itatumika kwenye ujenzi wa viwanja vingine nchini.

"Tunaamini kabisa kwa kasi ya mkandarasi na msimamizi mtakamilisha ujenzi huu haraka na viwango tulivyokubaliana katika mkataba ili ndege kubwa zianze kutua na kuruka" amesema Prof. Mbarawa.

Naye Msimamizi wa ujenzi wa kiwanja hicho kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. Mhandisi Mbila Mdemu amesema kazi ya ukarabati na upanuzi inaendelea kufanywa usiku na mchana kwa kuzingatia ubora na viwango na kukamilika kwa wakati

"Tulipewa kazi hii na tunaahidi kuwa  itakamilika kama tulivyoelekezwa ili kuwapa wananchi wanaozunguka mikoa ya Dodoma na jirani fursa ya kutumia usafiri wa Anga", amesema Eng. Mdemu.

Ameongeza kuwa kazi zinazokamilishwa sasa ni kumalizia sehemu ya maegesho ya ndege na tabaka la mwisho kwenye barabara  ya kuruka na kutua ndege.

Mradi wa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha  ndege cha Dodoma umegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zaidi ya shilingi bilioni 11.8 na kukamilika kwake kutaongeza idadi ya safari za ndege zitakazosafirisha abiria wa mikoa ya kanda ya kati.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma kutoka kwa Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho, Mkoani Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa kutoka Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho Mkoani Dodoma.

MWANAMKE AAMUA KUFUNGA NDOA NA MBWA WAKE BAADA YA KUACHANA NA MUMEWE

Baada ya ndoa yake kuingiwa na jini kisirani na kupelekea kuachana na mume wake , mwanamke huyu muingereza aliamua kufunga ndoa ya kifahari na Mbwa wake.

Mwanamke huyo aliejulikana kwa jina la Amanda Rodgers alifunga ndoa na mbwa wake ambae jina lake ni Sheba.

Tukio hilo la kustaajabisha lilihudhuriwa na watu wasiopungua 200, kushuhudia ndoa hiyo.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 alisema " Sheba amekuwa katika maisha yangu kwa miaka mingi sana, ananifanya niwe na furaha na anatioa mawazo pale napokuwa na huzuni,sifikirii kitu kingine zaidi ya yeye kuwa ndie mwenza wangu wa maisha"

Amanda aliolewa miaka 20 iliyopita na mwanaume, lakini ndoa yao ilidumu kwa muda mfupi sana,

Mwanamke huyo kwa sasa amebadilisha jina lake katika akaunti yake yaTwitter na anjiita @Shebarodgers

Hebu ona majanga yaliyompata huyu dada baada, ya kujichora tatoo

 Mwandada anekwenda kwa jina la Torz Reynold mwenye umri wa miaka 26 anetokea nchini Uingereza ametoa kali ya mwaka baada ya kulipiza kisasi baada ya kugundua boyfriend wake amekuwa akimcheat.

Torz alikuwa amejichora tattoo yene jina la mpenzi wake huyo mkononi na ndipo alipo amua kuuimenya sehemu hiyo ya ngozi yake na kuiweka kwenye chupa na kuifunga kama zawadi na kumtumia huyo jamaa yake posta.

Inasemekana huyo bwana alimuwaga mpenzi wake kwamba amepata kazi Alaska na akaondoka huku mpenzi wake huyo alimsindikiza airport. Baada ya muda akisikia kutoka kwa marafiki zake kwamba huyo bwana yuko nchini UK anaishi na mwanamke mwingine. 

 Mkono wa Torz ukiwa na tattoo yenye jina la ex wake 'Chopper'

 Torz akionyesha kifaa alicho tumia kumenyea ngozi yake hiyo

 Torz akionyesha mkono wake baada ya shughul hiyo na kipande cha ngozi alicho menya

 Kipande cha ngozi kikiwa kwenye chupa tayari kupelekwa posta

 Alama iliyo bakia baada ya kutoka kipande cha ngozi kilicho kuwa na jina la 'Chopper'

 Majanga

Huyu ndiye bwana aliyetumia zawadi ya kipande cha ngozi chenye jina lake

Jamani tuweni makini na hizi tattoo na pia napenda kunukuu maneno

Oscar Pistorius Ajeruhiwa Gerezani

Maafisa wa magereza nchini Afrika Kusini, wanasema kuwa mwanariadha mlemavu wa nchi hiyo Oscar Pistorius, ametibiwa hospitalini baada ya kupata majeraha akiwa korokoroni.

Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda

Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake

Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake, lakini kwa sasa amerejeshwa gerezani anakohudumia kifungo cha miaka sita kwa kosa la kumuuwa mpenziwe wa kike Reeva Steenkamp.

Kuna ripoti inayosema kuwa alikuwa amejeruhiwa kwenye kifundo cha mkono.
Kumeibuku uvumi katika mitandao ya kijamii nchini Afrika Kusini kuwa Pistorius alikuwa amejaribu kujitia kitanzi lakini hilo limekanushwa na familia ya mwanariadha huyo.

Mwezi uliopita, waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini, walisema kuwa watakata rufaa kupinga hukumu ya miaka sita ya Pistorius, wakisema kuwa ni hukumu ndogo mno.

Mwanariadha huyo alimuuwa mpenziwe wa kike , kwa kumpiga risasi nyumbani kwake wakati wa siku kuu ya wapendanao mnamo mwaka wa 2013, akisema kuwa alidhania ni mwizi.

Maaaaajabuu!! MWANAMKE AJIFUNGUA BAADA YA KUBEBA MIMBA KWA MIAKA MITANO!



An Abuja-based woman, Mrs Adenike Kolawole, (pictured left) who was barren for 27 years, has reportedly given birth to a baby boy after carrying a 5-year pregnancy. Is that even possible

According to PM News, Mrs Adenike gave birth on Sunday October 26th at Evangelical Church of

Cherubim and Seraphim located at Pipeline Road, Mafon area, Ejigbo, Lagos during the church’s Sunday service. Narrating her story to PM news, Mrs Kolawole said she suffered miscarriage in the early period of her marriage and afterwards found it difficult to conceive \

Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Agosti 8 kwenye habari zakitaifa kimataifa michezo n. K

Drake ataka kuzaa na Rihanna!


STAA wa muziki kutoka Marekani ambaye ni raia wa Canada, Aubrey Graham ‘Drake’ kidizaini ameonesha kama kutaka kuanzisha familia na msanii mwenzake, Robyn

 Rihanna Fenty baada ya kutamka hadharani katika Ukumbi wa Air Canada Centre mjini Toronto.

Tukio hilo lilijiri katika moja ya ziara zake kati ya saba zinazofahamika kama OVO Fest ambapo akiwa katikati mwa shoo, Drake alishangaa Rihanna kumsapraizi kwa kuingia jukwaani na kumfanya aweke wazi.

“Hii ni mara ya pili umenionesha sapraizi ndani ya mji wangu, lazima nianzishe familia na wewe ya kuwa na watoto,” alisema Drake.

Rihanna anatajwa kuwa na Drake kwa sasa baada ya kuachana na Travis Scott, pia aliwahi kuwa na Chris Brown.


Serikali Yatangaza Mwongozo Mpya wa Elimu Kuwa Masomo ya Sayansi ni Lazima Yasomwe Na Wanafunzi Wote


SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. 

Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini Tanga  na Waziri wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na mamia ya walimu wa elimu ya msingi kwenye mafunzo ya muda mfupi kuhusu mtaala mpya wa kufundishia wanafunzi wa darasa la tatu na nne.

Alisema hivi sasa nchi imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa kati ambao ni wa viwanda, hivyo suala la sayansi haliwezi kuepukwa kwa sababu ni wakati sasa wa kuwa na wataalamu wengi wa fani za sayansi watakaoweza kutosheleza mahitaji ya sekta ya viwanda nchini.

Alisema kutokana na uhaba wa wataalamu wa sayansi nchini kwenye maeneo mengi, wizara imeamua kuanzia sasa wanafunzi wote wa elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, watalazimika kusoma masomo ya sayansi na kufanya mtihani wa masomo hayo, na kwamba baada ya matokeo kutoka ndipo watafanya uamuzi ama wa kuendelea nayo au la.

Hatua hii kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, itamlazimisha mwanafunzi kusoma kwa bidii ili kuhakikisha anafaulu masomo hayo ingawa hivi sasa wanafunzi walio wengi wanadai masomo hayo ni magumu, ndiyo maana wanachagua kusoma masomo ya sanaa.

Alisema ili kuhakikisha azma ya serikali ya wanafunzi wanapata vitendea kazi vya masomo hayo, Sh bilioni 12 zimetengwa kwenye bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwenye shule zote za sekondari nchini ili kuwepo na zana za kufundishia kwa ajili ya masomo ya sayansi.

"Mafunzo ya vitendo sasa sio mbadala ni lazima, na yatafanywa kama sehemu ya masomo na wanafunzi wote watalazimika kuyafanya kwa vitendo ili wawe na uelewa wa walichosoma kwa manufaa ya taifa,”alisema Profesa Ndalichako.

Alisema Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuona kiwango cha elimu kinachotolewa nchini kina hadhi sawa na elimu itolewayo na mataifa mengine ili kupata wataalamu wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya soko hata kama sio wote wataajiriwa ila hata wale wasiopata ajira wajiajiri kupitia elimu waliyopata.

Aliwataka walimu waliohudhuria mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia uwezo wao na elimu waliyopata kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya taaluma ya ualimu ili kuwajengea msingi mzuri wa elimu wanafunzi wa shule za msingi.

Akizungumzia kauli ya Profesa Ndalichako, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAMANGOSCO), Mahmoud Mringo alisema ni uamuzi mzuri ila umekuja kwa kuchelewa kwa sababu mahitaji ya wataalamu wa sayansi nchini ni makubwa kuliko idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo.

Alisema pamoja na uamuzi huo mzuri uliochukuliwa na serikali, lakini bado kutakuwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo hayo, maabara na maktaba na kwamba hali hiyo inaweza kusababisha mahitaji ya walimu hao kutoka nje yakaongezeka.

Katibu wa Tamangosco, Benjamin Mkonya alisema ni hatua nzuri ingawa utekelezaji wake utakuwa na changamoto nyingi kwa sababu hali halisi ya mazingira ilivyo nchini.

Alisema ikiwa serikali inadhamiria kutekeleza azma hiyo ni vyema kipengele cha vigezo vya shule kuwepo ambavyo vimeainishwa ndani ya sheria ya elimu nchini, vikaangaliwa ambavyo ni uwepo wa maabara ya kutosha, maktaba yenye vifaa na walimu wa kutosha.

Alisema iwapo vigezo hivyo vikiangaliwa shule ambazo hazijakidhi vigezo hivyo zikafutwa na vifaa vilivyopo kwenye maabara na maktaba hizo zikaongezwa kwenye shule zenye vifaa hivyo ili kusaidia utekelezaji wa azma hiyo ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Walimu washiriki wameishukuru serikali kwa mafunzo hayo ambayo walisema ni mazuri na yameongeza kiwango chao cha uelewa na kuwaongezea mbinu za ufundishaji sambamba na kukuza morali ya kazi zao.

Pamoja na kushukuru, wameomba wizara hiyo iangalie jinsi ya kuweka posho kwa baadhi ya maeneo ya kazi, hususan kwenye vituo vya kazi vilivyopo pembezoni na kwenye mazingira magumu ili kuwajengea walimu motisha wa kufundisha maeneo hayo.

Walimu waliohudhuria mafunzo hayo ni 480 wanaotoka halmashauri za Bumbuli, Mji wa Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

Kumbe Nuh kapora demu wa mtu!

Natfal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, na anayedaiwa kumpora Nawali.


DAR ES SALAAM: Ubuyu wa mjini unanyetisha kuwa, mkali wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Jike Shupa aliomshirikisha Ali Kiba, Natfal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anadaiwa kupora demu wa jamaa ambaye naye ni msanii wa wa Bongo Fleva, Valentino Michael ‘Vale wel’.


Mrembo anayedaiwa kuporwa kwa Vale ni yule Nawali ambaye kwa sasa Nuh anamnadi kuwa ni mpenzi wake wa kiyama.


Ubuyu ulionaswa na Wikienda ulidadavua kuwa mwenye demu wake alipigwa na butwaa alipomuona Nuh akimnadi Nawali kwenye mitandao ya kijamii ndipo akang’atwa sikio kuwa kwa sasa hana chake kwani ‘mtoto’ yupo mikononi mwa Nuh.


CHOZI LA VALE

Akimwaga chozi mbele ya Wikienda, Vale alisema kuwa mpaka sasa hajaelewa ni kwa nini Nuh ameamua kumtangaza Nawali kuwa ni mpenzi wake wakati akijua wazi kwamba ni shemeji yake na ni mwanamke wake wa siku nyingi kwani wanafahamiana.


“Kiukweli nilikuwa sijui hili wala lile. Nilipoingia mitandaoni nilipigwa na butwaa kumuona Nuh akijitangazia ufalme kuwa mpenzi wake kwa sasa ni Nawali.

“Mwanzoni nilijua labda ni mambo ya kiki kwa sababu nijuavyo Nuh hana malengo mazuri na Nawali.

“Baadaye ndipo nikawa nahakikishiwa na watu wangu wa karibu kuwa ni wapenzi na hawafanyi kificho.

“Kinachoniumiza nilikuwa sina tatizo wala ugomvi wowote na Nawali na bado naamini ni mpenzi wangu kwa sababu hatujaachana na tukikutana huwa tuko kama kawaida,” alisema Vale.


Valentino Michael ‘Vale wel’ na Mrembo anayedaiwa kuporwa, Nawali.

MWENYE KISU KIKALI?

Vale alizidi kutokwa povu kuwa kwa sasa hasemi sana kwa sababu hana mkwanja wa kumpa Nawali hivyo ule usemi wa mwenye kisu kikali unamtafuna kwani inawezekana Nuh anatumia vijisenti alivyonavyo kumnyang’anya tonge mdomoni.

“Lakini ukweli ni kwamba ‘nafaiti’ na mambo yatakaponinyookea nitahakikisha nafanya kila njia kumrudisha Nawali kwenye himaya yangu kwani ndiye mwanamke wa maisha yangu.

“Najua nilipomtoa, ni mwanamke ambaye ninampenda sana na nimetumia muda mwingi kumbadilisha kimuonekano kwani mwanzoni hakuwa alivyo sasa, alikuwa mgumu hivyo nimefanya jitihada za hali ya juu kumfanya aonekane ‘soft’,” alimalizia Vale.


HUYU HAPA MTUHUMIWA NUH

Baada ya ubuyu huo ulionyooka kutua kwenye Wikienda, waandishi wetu walimweka ‘mtukati’ Nuh aliyedai kuwa hapendi kumuongelea mpenzi wake huyo kwa sababu kama ni maneno yameshasemwa mengi.

“Unajua kuhusu huyu demu wangu, maneno mengi sana yamesemwa hadi nimechoka. Kama huyo mwanaume yupo na anaamini ni mwanamke wake basi amchukue akakae naye,” alisema Nuh akiomba kuachwa atulize mawazo.


NAWALI ANASEMAJE?

Kwa upande wake Nawali, alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa hamjui Vale na wala hajawahi kupiga naye picha za kimahaba ambazo gazeti hili lina nakala zake.

Habari kutoka kwa Wana-Ubuyu wanaolinyaka vilivyo sakata hilo wanadai kwamba Vale ana uhakika kuwa huyo ni mpenzi wake na picha ametoa wakiwa wawili tena kimahaba hivyo inakuwaje Nawali anabisha?

HUYU NDIYE NUH

Mbali na Nawali, baada ya kufungishiwa virago na Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Nuh alitua kwa mrembo mwingine shombeshombe ambaye hata hivyo hawakudumu.



Chanzo:GPL

 

Gallery

Popular Posts

About Us