KINGAZI BLOG: 08/15/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, August 15, 2016

BASATA Yamfungulia Nay wa Mitego

Katikati ni katibu wa Baraza la sanaa Tanzania, BASATA, Godfrey Mungereza akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa tamko la kumfungulia Nay. Kushoto nia msanii Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na kulia mwenye miwani ni Meneja wake, Maneno John. 


Nay wa Mitego akizungumza.

Nay wa Mitego akionyesha cheti chake cha usajili na kibali cha BASATA.

 


Wanahabari wakifuatilia tukio hilo.

(PICHA: DENIS MTIMA/GPL)

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungulia Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego kuendelea na shughuli za Sanaa baada ya kuwa ametekeleza adhabu (maagizo) zote alizopewa kama masharti ya kumfungulia.

Aidha, BASATA kama mlezi wa wasanii linamfungulia kufuatia yeye mwenyewe (Nay wa Mitego) kujutia na kukiri kwamba amejifunza na yuko tayari kubadilika na kwamba hatarudia makosa aliyoyafanya.

Hata hivyo, pamoja na kumfungulia kuendelea na shughuli za Sanaa Baraza linamweka kwenye uangalizi maalum msanii huyo kama sehemu ya kuhakikisha anaendesha shughuli za Sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu sambamba na kuzingatia maadili katika kazi zake.

Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 27/07/2016 Baraza lilimfungia Msanii Nay wa Mitego kwa kipindi kisichojulikana na kumtaka kutekeleza maagizo yafuatayo:

1.Kuhakikisha amesajiliwa na kuwa na  kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa

2. Kulipa faini ya shilingi milioni moja (1,000,000/-)

3. Kuomba radhi watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari na kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii

4. Kuufanyia marekebisho wimbo wa ‘Pale Kati’  ili ubebe maudhui yenye maadili

Msanii Nay wa Mitego ametekeleza adhabu zote tajwa hapo juu. Leo hii tunamkabidhi rasmi cheti chake cha usajili na kibali cha BASATA.

Hata hivyo, pamoja na kuleta marekebisho mara mbili ya wimbo wa ‘Pale Kati’ Baraza bado halijaridhishwa na marekebisho hayo hivyo linaendelea kuufungia wimbo huu hadi hapo litakapojiridhisha umekidhi vigezo vya kimaadili.

Katika kikao na Msanii Nay wa Mitego cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa adhabu yake kilichofanyika tarehe 12/08/2016 Ofisi za BASATA ameagizwa kuendelea kuufanyia marekebisho wimbo wake huo kama bado anaona anauhitaji.

Baraza linatoa maelekezo kwa vyombo vya habari na watanzania kwa ujumla kuacha kuucheza wimbo huo hadi hapo itakapoelekezwa vinginevyo. Hatua na adhabu za kisheria zitachukuliwa kwa chombo chochote cha habari kitakachokiuka agizo hili.

Aidha, katika kikao hicho cha tathimini ilibainika kwamba Msanii Nay wa Mitego kwa taarifa potofu alizopewa alipanda Jukwaani kwenye tamasha la Mwendo Kasi la tarehe 30/07/2016 akiwa katika adhabu. Kwa kosa hili ameandika barua ya kuomba radhi na Baraza linafikiria hatua za kuchukua kwa waandaaji wa tamasha hili.

Baraza linatoa wito kwa wasanii kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji shughuli za Sanaa sambamba na kuhakikisha wanazingatia maadili katika kila kazi wanazobuni ili kuepuka matatizo yasiyo ya lazima ambayo yanaathiri kazi zao kwa kiasi kikubwa sana.

Rais Edgar Lungu Ashinda Uchaguzi Zambia

Rais Edgar Lungu.

RAIS Edgar Lungu ametangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Zambia kwa kupata asilimia 50.35 ya kura na kumshinda mpinzani wake, Hakainde Hichilema aliyepata asilimia 47.67.

Chama Kikuu cha Upinzani, UPND kimepinga matokeo hayo na kudai kura zimeibiwa.

Hakainde Hichilema ambae ni mara yake ya tano kugombea urais anadai kuwepo kwa udanganyifu wakati wa upigaji kura siku ya Alhamisi.

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo na Makampuni Mbali Mbali Kwenye Magazeti na Mitandaoni

TAARIFA RASMI JUU YA SAKATA LA KUJIUZULU MANJI KWENYE KLABU YANGA

Ni kweli Mwenyekiti amekusudia kufanya hivyo kwa sababu anasakamwa , anatukanwa na kudhalilishwa na Makonda na Mzee Akilimali.

Lakini kibaya hakuna tamko kutoka kwa Mwana-Yanga yeyote aliyekemea hilo na kuonyesha kumuunga mkono MWENYEKITI .Hivyo anajiona mnyonge na amesuswa bora akae pembeni. . Hivyo tumewasiliana viongozi wa Kanda wote tumeamua Tuitishe kikao cha Dharula kesho SAA 4 Asubuhi pale makao makuu tutatoa Tamko la pamoja na wengine wataanza kuongea na vyombo vya habari Leo hii.

Hima Tuhamasishane tuwe pamoja kesho .Tuwasihi wanachama wetu wafike club.

Katibu Mkuu.

 

Gallery

Popular Posts

About Us