KINGAZI BLOG: 03/24/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, March 24, 2016

Kleyah - African Drum (Official Video)


RUBY FT WAKAZI - SIJUTII RMX(AUDIO)


VANESSA MDEE - NIROGE(AUDIO)


download: Vanessa Mdee - Niroge (Official Video)


VIDEO;Dkt.Shein aapishwa kuwa Rais wa zanzibar

Image result for hatimaye shein aapishwa









 Hatimaye Rais wa zanzibar Dkt.Ally mohammed Shein ameapishwa kuwa rais wa awamu ya saba visiwani zanzibar nakuwahakikishia wananchi wa zanzibar kuendelea kuwa mstari wa mbele kulinda na kuitetea amani ya zanzibar.

9, wajitosa uspika Zanzibar.


 Image result for majengo ya bunge  zanzibar

VITA ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar imepamba moto, huku mchuano mkali ukionekana kuwa kati ya Spika aliyemaliza muda wake, Pandu Ameir Kificho,

Snura: Sitaki mtoto mwingine wa nje ya ndoa



Snura na meneja wake HK
LICHA ya kuwa na watoto wawili kwa baba tofauti, mkali wa kuimba na kunengua, Snura Mushi, amesema kwa sasa hataki apate mtoto mwingine hadi atakapoolewa.
Msanii huyo anayetamba na wimbo wa ‘Chura’ alisema wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi

Dayna: AY na Prezzo wameniponza.




dayna
MSANII wa Bongo Fleva, Diana Nyange ‘Dayna’, amesema kilichosababisha wakaachana na mchumba wake ni wivu wa mapenzi uliotokana na picha aliyopiga na wasanii wawili wa Kenya, Wahu na Prezzo pamoja na Mtanzania, Ambwene Yessaya ‘AY’.

Wabunge wahojiwa Takukuru




job* Ndugai atoa ufafanuzi wa tuhuma za rushwa
*Asema vyombo vya dola kufanya uchunguzi
*Kamati iliyosusa yaendelea na vikao Dar

SIKU moja baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, kupangua wenyeviti na makamu wenyeviti kwa kuwaondoa kwenye kamati walizokuwa wanaziongoza, hatimaye Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), imewahoji wabunge watatu ambao wanatajwa kuhusika na mgawo wa fedha.

Miaka 20 jela kwa kumiliki digidigi


Männliches Kirk-Dikdik im Tarangire-Nationalpark

MKAZI wa Mabibo, Dar es Salaam, Abraham Warioba (50),  amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh milioni 39, baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki digidigi 20 kinyume cha sheria.

Askari wanaswa wakiiba mafuta ya ndege



MTZ Alhamisi new july.indd
VITA ya kutumbua majipu kwa watumishi wa Serikali wasiokuwa waaminifu imeendelea kushika kasi, baada ya jana Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni kuagiza kusimamishwa kazi mara moja askari watatu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa tuhuma za wizi wa mafuta ya ndege na mizigo ya abiria.

Rais Shein kuapishwa leo


RAIS Mteule wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein anaapishwa leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa. Kuapishwa kwa Dk Shein kunamfanya apate fursa nyingine ya kuongoza Zanzibar kwa

Mwili wa Sarah Dumba kuletwa Dar leo


MKUU wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba aliyefariki ghafla juzi, amefanyiwa ibada na kuagwa rasmi na wakazi wa wilaya aliyokuwa akiiongoza, ambapo mwili wake unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo asubuhi kwa maziko.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk Rehema Nchimbi alisema, ibada ya kumuaga rasmi ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) lililopo mkoani humo.
“Tumemuaga na safari ya kwenda Dar es Salaam itaanza muda mfupi kuanzia sasa (jana jioni), tutasafiri usiku mzima tunatarajia kuingia Dar es Salaam kesho (leo) asubuhi tayari kwa mazishi,” alisema Dk Nchimbi.
Kwa mujibu wa taarifa ya ndani ya familia, mwili wa Dumba unatarajiwa kuwasili saa 4:00 asubuhi na taratibu za mazishi zitafanywa nyumbani kwa baba yake, Mzee Dumba eneo la Kigamboni Midizini.
Baada ya chakula itafanyika ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Magogoni lililopo Kigamboni na maziko yatafanyika kwenye makaburi ya Magogoni. Wakati huo huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa wanahabari wote kutokana na kifo cha ghafla cha mkuu huyo wa wilaya ambaye pia alikuwa ni Mtangazaji Mwandamizi wa zamani wa Redio Tanzania (RTD), Dar es Salaam.
“Pokeeni salamu zangu za rambirambi za dhati kwa kuondokewa na mwanahabari mahiri Dumba aliyekuwa mfano wa kuigwa. Mbali na utangazaji wake mahiri, alikuwa mzalendo wa kweli aliyetumikia tasnia hii ya Habari na Serikali kwa uadilifu na upendo wa kweli, tutamkumbuka na tutaukosa mchango wake,” alisema Nape.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Elisante ole Gabriel alituma salamu za pole na kuwatakia moyo wa subira na uvumilivu ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu. Baadhi ya wafanyakazi waliowahi kufanya kazi naye walisema, kifo chake ni pigo na pengo lisiloweza kuzibika.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba akizungumzia uhusiano wake na Dumba, alisema yeye alianza kazi RTD mwaka 1971 na kumkuta Dumba akiwa tayari kazini hivyo walifanya naye kazi kwenye Idhaa ya Kiingereza ya External Services wakati Dumba akiwa msaidizi wake.

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS YA TAR 24 MARCH 2016 KWENYE HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA UDAKU NA MICHEZO PIA STORI NYINGINE KALI.

March 24 2016 naanza kwa kukuletea habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye habari za kitaifa,kimataifa,udaku na , Michezo ili ujue yaliyojiri duniani. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook/tanzaniampya news blog na  twitter@TZmpyasasa.
 

Gallery

Popular Posts

About Us