KINGAZI BLOG: 04/29/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, April 29, 2016

VIDEO:Trump achekwa kwa alivyotamka Tanzania

Trump

Trump alishambulia sana sera ya kigeni ya Obama
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump amekejeliwa mtandaoni baada ya kuonekana akiboronga akitamka Tanzania wakati wa kutoa hotuba.
Bw Trump alikuwa akizungumzia mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa katika mabalozi ya Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 wakati wa kuzungumzia sera yake ya kigeni.
Badala ya kutamka vyema ‘Tanzania’ anasikika akitamka ‘Tan-zay-nia’.
Mashambulio hayo yalitekelezwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda.
Msemaji wa ikulu ya White House pia alimcheka Bw Trump alipoulizwa kuhusu vile mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York alivyotamka jina Tanzania.
“Kweli, yamkini jinsi ya kutamka huwa haijaelezwa kwenye kifaa cha kuonesha maandishi ya hotuba,” alieleza afisa wa habari wa ikulu Bw Josh Earnest.
Wakati wa hotuba hiyo, alizungumzia pia kuhusu kundi la Islamic State ambalo kwa sasa limeanza kunawiri nchini Libya. Kundi hilo hujulikana pia kama Isis.
“Na sasa Isis wanapata mamilioni na mamilioni ya dola kila wiki kwa kuuza mafuta ya Libya. Na wajua? Huwa hatuwawekei vikwazo vya kutouza, hatuwaangushiwi mabomu, hatufanyi lolote,” alisema.
“Ni kana kwamba nchi yetu haifahamu yanayofanyika, jambo ambalo huenda likawa kweli.”
Kwenye hotuba yake, Bw Trump alikosoa sera za kigeni za Rais Barack Obama.
Lakini Bw Earnest alipuuzilia mbali madai ya Bw Trump ambaye kwa sasa anaongoza miongoni mwa wagombea wanaotaka kupeperusha bendera ya chama cha Republican

.BOFYA HAPA KUONA VIDEO TRUMP AKICHEKWA BAADA YA KUSHINDWA KUTAMKA TANZANIA

Rais Magufuli Awasili Mkoani Dodoma Kwa Usafiri wa Gari.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akitokea mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea Dodoma kutokea mjini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Picha 9 za Jeshi letu la JWTZ Likiwa Katika Uwanja wa Mapambano Huko Congo DRC


Hapa  kuna Picha Kadhaa za Wanajeshi wetu wa JWTZ  Wakiwa  katika  uwanja wa Mapambano katika Misitu ya Ben Congo DRC.

Juzi kati, jeshi letu limetunukiwa  medani na MONUSCO Kwa umahili wake

==>Habari hii,picha pamoja na video ni kwa hisani ya  mwandishi na correspondent wa ITV anayeripoti toka Congo ndg. Eshongulu Eshongulu Eshongulu

Kumbe TID alishawahi kutoka kimapenzi na Wema Sepetu

TID




Msanii mkongwe wa muziki, TID amesema kipindi cha nyuma alikuwa anatoka kimapenzi na malkia wa filamu Wema Sepetu lakini baadae alitemwa hali ambayo ilimuumiza sana.

Akizungumza katika kipindi cha Clouds TV Ijumaa hii, TID amesema hali hiyo ilimfanya atoke na wasichana wengi.
“Nilikuwa ‘namdate’ Wema Sepetu akaniambia sikutaaki, tangu kipindi hicho nimekuwa na wasichana wengi. Ikitokea Wema anataka kurudi hakuna nafasi, I’m occupied,” alisema TID.
TID amesema katika kipindi hicho aliumizwa sana na jinsi magazeti yalivyokuwa yanamuandika vibaya.
“Wakati huo mitandao ya kijamii haikuwepo lakini wamagazeti walizichukua picha na kufanya yao, it was bad. Mimi nikasema sawa lakini niliumia sana,” alisema TID.
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Confidence’ aliyomshirikisha Joh Makini pamoja na Dully Sykes.

Naibu Spika Achafua Hali ya Hewa Bungeni Baada ya Kumwita Mbunge BWEGE


Naibu Spika Tulia Ackson, ambaye katika vikao vya Bunge anatakiwa kusimamia mijadala kwenye chombo hicho cha kutunga sheria, jana alizua kizaazaa baada ya kumuelezea mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Said Bungara kuwa ni bwege, akimtaka aache kuonyesha hali hiyo.


Kwa mujibu wa toleo la pili la Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford) la mwaka 2004, neno bwege linamaanisha “mtu mjinga, mpumbavu, bozi, fala gulagula”.


Kitendo cha kutumia neno bwege kumuelezea mbunge huyo kilisababisha wapinzani wacharuke, na kuibua bungeni kesi ya mtu aliyefunguliwa mashtaka mkoani Arusha kwa kosa la kumuelezea Rais John Magufuli kuwa ni bwege.


Bila ya kuruhusiwa, mmoja alifungua kipaza sauti na kusema: “Hatimaye msamiati wa bwege watua bungeni sasa kutumika rasmi. Futa lugha ya kuudhi; bwege bwege.”


Hata hivyo, wabunge hao wa upinzani hawakushinikiza Dk Tulia kufuta kauliz yake, lakini baadaye wakiwa nje ya ukumbi waliponda kitendo hicho cha kiongozi huyo wa Bunge ambaye aligombea uspika kwa tiketi ya CCM kabla ya kujitoa na muda mfupi baadaye kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa mbunge na hivyo kupata sifa ya kugombea nafasi hiyo ya naibu spika.


Dk Ackson aliamsha tafrani hiyo saa 5:48 asubuhi baada ya Bungara, ambaye ni maarufu kwa jina la Bwege, kusimama bila kufuata kanuni za Bunge, kupinga maelezo ya Waziri wa Habari, Nape Nnauye juu ya uamuzi wa Serikali kusitisha shughuli za Bunge kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni nchini.


“Na wewe Mheshimiwa Bwege, hebu kaa chini. Usionyeshe ubwege wako hapa,”alisema Dk Ackson kumzuia mbunge huyo asiendelee kuzungumza wakati mjadala ukianza kuwa mkali.


Mjadala huo uliendelea bila ya wapinzani kuhamaki, lakini baada ya Nape kutoa taarifa akieleza kuwa uamuzi wa kuanzisha studio za Bunge ulifanywa na Bunge la Kumi ambalo yeye hakuwamo, ndipo wapinzani walipokumbusha kauli hiyo ya naibu spika

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 29 2016 kwenye,Habari zaUdaku, Kitaifa,kimataifa na michezo.


   April 29 2016 naanza kwa kukuletea habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye ,habari za kitaifa,kimataifa Michezo na udaku na stori nyingine kali ili ujue kilichojiri duniani.. usiache kukaa karibu kwenye kurasa zetu za mitandao...
 

Gallery

Popular Posts

About Us