KINGAZI BLOG: 06/21/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, June 21, 2016

Rais Magufuli amteua Dkt. Jim Yonazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji TSN.


 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Juni, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Jim James Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Dkt. Jim James Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel Nderumaki ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

   

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

21 Juni, 2016

Al-Shabab lakiri kutekeleza shambulio Mandera Kenya

al-Shabab

Kundi la wapiganaji wa kiislamu nchini Somalia al-Shabab, limekiri kutekeleza shambulio lililotokea Jumatatu asubuhi nchini Kenya, ambapo askari watano waliuawa.

Shambulizi hilo linaloaminika kutekelezwa na roketi na kulenga gari ya polisi aina ya Land Cruiser lilitokea kilomita chache kutoka mji wa Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Mji wa Mandera uko mita chache kutoka mpaka wa Kenya na Somalia.

Radio Andalus iliyoko nchini Somalia, imetangaza kuwa, shambulizi hilo ni kuipa Kenya adabu ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia.

Kenya ina vikosi vyake vya kijeshi nchini Somalia chini ya muungano wa Afrika AMISOM.

Wabunge wa Upinzani Watoka Bungeni kwa staili ya tofauti leo



Wabunge wa upinzani katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania leo wameendelea na msimamo wao wa kususia vikao vya bunge lakini leo wamekuja na staili tofauti ambapo leo wameua kutoka nje ya ukumbi wa bunge kimyakimya bila kelele.

Inasemekana baada ya hapo wamepanga kufanya kikao kujadili mstakabali wa msimamo wao,wabunge hao wamedhihirisha dhahiri kwamba wamechoshwa na Uongozi wa bunge kupitia naibu spika Dkt.Tulia Akson

Inasemekana pia kwamba baada ya kikao walichoitisha wabunge hao wa upinzani,Watatoa tamko kupitia mbunge wa Vunjo,Mh.James Mbatia.

 

Gallery

Popular Posts

About Us