KINGAZI BLOG: 07/02/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, July 02, 2016

Huyu hapa Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika

 

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wamebaini kuwepo na baadhi ya Makampuni na watu binafsi ambao wamekuwa wakijihusisha na ukwepaji Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Mapato kwa kutumia Mashine za Kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na TRA na kutoa risiti bandia.

Makampuni hayo yamekuwa yakinunua risiti za manunuzi bandia kutoka kwa watu wanaomiliki mashine za kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na kuzitumia risiti hizo kudai marejesho ya VAT bila kuwepo na bidhaa au huduma halisi iliyouzwa au kutolewa na muhusika, kitendo ambacho kinainyima Serikali mapato stahiki kwa mujibu wa sheria.

TRA kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi ili kubaini makampuni yote yanayojihusisha na udanganyifu huu, ambapo hadi sasa jumla ya makampuni manne (4) yamebainika kujihusisha na ukwepaji kodi kwa mtindo huu kuanzia mwaka 2010 hadi 2014; na jumla ya shilingi 29,216,900,301.7 imebainika kutokulipwa Serikalini na makampuni hayo kwa kipindi hicho.

Makampuni hayo manne ni pamoja na Skol Building Material Ltd ambayo tangu mwaka 2012 hadi 2013 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 5,464,915,963 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 10,960,787,861 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 16,425,703,824 kwa kipindi hicho.

Kampuni nyingine ni Farm Plant (T) Limited, tangu mwaka 2010 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 5,930,170,573 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 4,948,393,516 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 10,878,564,089.

Kwa upande wa A.M. Steel & Iron Mills Limited kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 79,016,112 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 131,693,518 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 210,709,630.

Kampuni nyingine ni A.M. Trailer Manufacturers Limited ambayo tangu mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 638,221,034.80 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 1,063,701,724.00 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 1,701,922,758.80

Baada ya kubaini ukwepaji kodi wa makampuni hayo, TRA kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizi na mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukwepa kodi.

“Ni wito wangu kwa wafanyabiashara wote kutojihusisha na kununua risiti za bandia na kudai marejesho ya (VAT) yasiyostahili kwakuwa Mamlaka imejidhatiti kuendelea na zoezi hili la kuwabaini wafanyabiashara wanao kwepa kodi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa hatua stahiki”.

Alisema Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata.

Imetolewa na:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa pamoja.

JACKLINE WOLPER ALIJIA GAZETI LILILOMWANDIKA KUBAKWA NA MSANII WA DIAMOND




Habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Sani la leo jumamosi limemsononesha mrembo Jack Wolper kwa tuhuma za uongo kuwa amebakwa na Msanii wa Diamond...Mwenye Kayaandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram:
@wolperstylish - I am so sad kwakweli
Hii sio kuniabisha mimi tu, ni kuaibisha na wanawake wenzangu, sijui kwanini magazeti ya kibongo yanatumia Nguvu nyingi kushusha hadhi ya wasanii wa kike haswa.. Nyie SANI no wonder mmepotea katika soko.. Hivi mlivyokua mnachapa mmefkiria kuna wadogo zangu wanasoma?? Au mama angu na baba angu!
Naandika kwa uchungu kwakua najua ni limtu limekosa kazi ya kutumia kipaji chake na karama yake vyema linaishia kutumia kwa kuniharibia maisha yangu... Tena front page? Tunafany mangapi mazuri hatuingii page ya kwanza hata siku moja,?! Kesho kutwa nafungua biashara mtaona kama wataandika kitu
Ila kwenye ujinga wa kutunga ndo wakwaza
Mnaniuzi na nawahakikishia kama Mungu aishivyo mtaona kwa wanenu pia
Si mmeamua kuniandika mimi hivi!??!
Na kila siku mnafanya hivi
My loves embu nisaidieni niwaambie nini cha zaidi wauaji kama hawa
Kuna uuaji wa aina nyingi... Hata maneno huua jamani, sisi pia tu a mioyo

Dah!

BIG SHAME ON YOU GUYS

Kuanzia alietunga stori, alieidhinisha ichapishwe na mwenye gazeti

Kwanini Mh @paulmakonda hawa wasiwe wanapigwa faini au hata kupelekwa mahakamani?? Manake msamaha hautoshi

Wanaharibu kabisa maana ya vyombo vya habari

Nancy Sumari na Luca Neghesti Wafunga Ndoa yao Jana Julai 1


YAMETIMIA! Hivyo ndivyo tunaweza kusema kwa sasa baada kushi kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miaka mingi, hatimaye Mwenyekiti Mtendaji wa Bongo5 Media Group Limited, Luca Neghesti na Miss Tanzania 2005 ambaye pia ni Miss World Africa, Nancy Sumari kufunga ndoa jana Ijumaa.

Wawili hao wamefunga ndoa jana jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu takriban 60 ambao wengi wao ni ndugu na marafiki zao wa karibu. Tunawapongeza kwa hatua hiyo kubwa kwenye maisha yao.

Luca na Nancy ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5 wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Zuri.



STAA NICKI MINAJ ATUPIA PICHA HIZI ZA UTATA MTANDAONI.



 

">

Magazeti ya, Tanzania yalichoandika leo Julai 2 kwenye habari za kitaifa, kimataifa Michezo na, stori nyingine kali.

Karibu, tunakuletea uchambuzi wa Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 2 kwenye habari za kitaifa komataifa na michezo



Majengo Ya Mahakama ya Mafisadi Kukabidhiwa Jumatatu

WAKATI Mahakama Maalumu ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi ikitarajiwa kuanza wakati wowote, majengo ya mahakama hiyo yanatarajiwa kukabidhiwa keshokutwa jumatatu.

Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande, alisema jana kuwa mkandarasi aliyekabidhiwa kazi ya kukarabati majengo hayo yaliyopo katika Shule Kuu ya Sheria, pembeni mwa kituo cha mabasi cha Simu 2000, Ubungo Dar es Salaam, yako katika hatua za mwisho za ukarabati.

Akizungumza katika viwanja vya Karimjee baada ya kuapisha mawakili wapya 623 wa Mahakama Kuu, Jaji Chande alisema tayari Bunge limeshapitisha muswada wa sheria ya uanzishwaji wa mahakama hiyo.

Alisema kwa sasa muswada huo utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuusaini ili uwe sheria, kisha sheria hiyo itatangazwa katika gazeti la Serikali ili kuruhusu shughuli za mahakama hiyo kuanza.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama iko tayari kuendesha Divisheni hiyo ya Mahakama na baada ya kukabidhiwa majengo hayo, wataanza kutoa semina kwa majaji na watumishi wengine wa mahakama hiyo, kuhusu divisheni hiyo itakavyoendesha shughuli zake.

Aliweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna kesi hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba itashughulikiwa na mahakama hiyo.

Askofu Gwajima ni Mgonjwa.....Ashindwa Kutokea Mahakamani Kwenye Kesi Inayomkabili

PETER Kibatala wakili wa Josephati Gwajima Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima jana aliiomba mahakama kuahirisha tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili askofu huyo sababu anaumwa.

 

Kibatala alidai mahakamani Kisutu kuwa kutotokea kwa mteja wakejana kulitokana na yeye kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Wakili huyo  aliwasilisha madai hayo jana katika Mahakaama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Syprian Mkeha Hakimu Mfawidhi anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili Gwajima

Mahakama ilikubali ombi hilo na kwamba kesi hiyo itatajwa tena 2 Agosti mwaka huu.

Katika kesi hiyo Gwajima anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam.

Gwajima anadaiwa kufanya tukio hilo kati ya 16 na 25 Machi, mwaka 2015 katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

 

Gallery

Popular Posts

About Us