KINGAZI BLOG: 08/21/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, August 21, 2016

Kauliya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda Aliyetumbuliwa Juzi na Rais Magufuli


Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyeondolewa, Felix Ntibenda amekabidhi ofisi huku akitoa neno la mwisho la kuwakaribisha Kigoma baadhi ya maofisa waliokuwapo kwenye hafla hiyo.

“Karibuni sana Kigoma,” ndiyo lilikuwa neno la mwisho kwa Ntibenda alilolitoa baada ya kukabidhi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa mpya Mrisho Gambo, hafla iliyofanyika kwa muda mfupi.

Ntibenda aliyehamishiwa ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya kusema neno hilo alipanda gari na kuondoka. 

Kabla ya makabidhiano,alikuwa wa kwanza kufika ofisini saa 3.30 asubuhi na kulazimika kusubiri hadi 5.05 asubuhi, alipowasili mkuu mpya wa mkoa Gambo aliyeapishwa Ikulu jijini Dar es Saalam juzi na Rais John Magufuli. 

Gambo kabla ya uteuzi huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Arusha na aliwasili ofisini akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama.

Aliingia ofisini kwake na kukutana na Ntibenda, ambapo walifanya makabadhiano na kutoka huku wakizungumza.

Makabidhiano hayo yalifanyika haraka kwa kile ambacho kilielezwa na mkuu mpya wa mkoa kutakiwa kusafiri kwenda Loliondo kupokea Mwenge wa Uhuru.

Katibu Tawala, Richard Kwitega alisema Gambo baada ya makabidhiano alikuwa na ratiba moja tu kuzungumzia mbio za Mwenge wa Uhuru ambao leo unaingia mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Gambo alisema jana alitarajia kuzungumzia mbio za Mwenge pekee na kwamba unatarajiwa kuzindua miradi yenye thamani ya Sh12.9 bilioni.

UVCCM wampokea Gambo 

Kama ambavyo, ilitarajiwa jana, viongozi wa UVCCM Mkoa wa Arusha wakiongozwa na mwenyekiti wao, Lengai ole Sabaya walijitokeza katika mapokezi ya Gambo. 

Sabaya alisema wanampongeza Rais Magufuli kwa kusikiliza kilio chao na pia kumteua kijana kuongoza mkoa.

“Sisi kama UVCCM tumekuja hapa kumpongeza mkuu mpya wa mkoa na tuna imani naye sana kuwa atasaidia maendeleo ya mkoa huu,” alisema.

Man Fongo awachimba mkwara wa Bongo fleva

Kwa kasi iliyopo kwenye muziki wa Singeli, ni wazi kwamba unaelekea kuupoteza muziki wa Bongo Fleva kutokana na kasi ya kuenea kwake hapa nchini, jambo linalosisitizwa na mkali anayetesa katika muziki huo, Amani Hamisi ‘Man Fongo’.

Man Fongo ambaye amepachikwa jina la Mfalme wa Singeli, anayesumbua na kibao chake cha Hainaga Ushemeji amesema wasanii wa Bongo Fleva wana kazi kubwa kuhakikisha wanabaki kileleni kutokana na namna muziki wao ulivyopokelewa vizuri na mashabiki.

“Muziki tunaouimba ni wa mtaani ambapo ndiko chimbuko na watu wa uswahilini, kwa sasa huwaambii kitu kuhusu muziki wetu. Nawaambia ukweli kabisa wasanii wa Bongo Fleva, wakaze buti twende sawa au watafute kitu kingine cha kufanya.

“Ujue wao wanaimba vitu vya kubuni wakati sisi tunaimba maisha halisi hasa ya uswahilini kwa masikini wenzetu,” anasema Man Fongo.

Picha za Mwisho za Marehemu Shakila Mjini Dodoma L

 Aliyekuwa msanii mahiri wa Taarab, marehemu Shakila Said wakati wa uhai wake akipongezwa na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete wakati wa Tamasha la wasanii kumuaga Kikwete usiku baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa chama hicho, mjini Dodoma Julai 23, mwaka huu. 

 Shakila akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana.

Akitafakari jambo.

30 wauawa wakiwa, harusini nchini uturuki

Watu wapatao 30 wameuawa na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa, baada ya mlipuko wa bomu kutokea katika sherehe moja ya harusi katika mji wa Gaziantep, kusini mashariki mwa Uturuki.
Hayo ni kwa mjibu wa maafisa wakuu nchini humo.

Gavana wa jimbo hilo, Ali Yer-likaya, ametaja shambulio hilo kama tukio la kigaidi.

Naibu waziri mkuu Mehmet Simsek, amesema mlipuko huo ni tendo la kinyama, huku akiongeza kuwa huenda lilitekelezwa na wapiganaji wa kujitoa muhanga

Rais Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa kundi la Islamic State, ndilo lililotekeleza shambulio hilo.

Ameongeza kusema pia kuwa hakuna tofauti kati ya IS, Vuguvugu lililopigwa marufuku la PKK na wafuasi wa kiongozi wa kidini aliyeko uhamishoni nchini Marekani Fetullah Gulen, ambaye alilaumiwa kwa kupanga jaribio la mapinduzi lililotibuka mwezi uliopita.

 

Gallery

Popular Posts

About Us