KINGAZI BLOG: 08/04/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, August 04, 2016

RAY C APOST KWA MARA YA KWANZA TANGU APELEKWE KWENYE MATIBABU BAGAMOYO

Usiku wa June 16 2016 kuamkia June 17 kuna video ya mwimbaji wa longtime Bongoflevani Rehema Chalamila au Ray C ilisambaa mitandaoni akiwa anachukuliwa na gari la Polisi Kinondoni Dar es salaam ambapo baadae ilikuja kugundulika alipelekwa Hospitali.
Kesho yake mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahabaalionge na Amplifaya ya CloudsFM pamoja na millardayo.com na kuthibitisha kwamba mwimbaji huyu amekubali mwenyewe kwa hiari yake na kupelekwa kwenye nyumba ya matibabu ya kuachana na dawa za kulevya huko Bagamoyo Pwani.Baada ya hapo tuliona ukimya sana kwenye mitandao ya kijamii na Ray C hakuwa anapost chochote tofauti na tulivyozoea alikua mtu wa kupost na hata kuongea mara kwa mara.
Leo August 3 2016 amepost maandishi yasemayo >>> ‘Sala ya amani, Mungu amenipa amani, amenipa nguvu ya kubadilisha vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wangu na hekima ya kujua utofauti, kuishi siku moja baada ya nyingine, kufurahia mda mmoja baada ya mwingine, kukubaliana na ugumu kama njia ya kukupa amani’Picha nyingine aliyoiweka ilisema ‘KUPONA HUJA KWANZA, bili zitalipwa, kazi yako utamaliziwa, orodha itafanyika na utalipa kodi, bado familia yako itakupenda, maisha yako ya upendo yatachanua pale yakiwa tayari, utakuwa na vitu uvipendavyo, fanya moyo wako, afya yako, na msimamo wako kuwa juu ya vitu hivyo, KUPONA HUJA KWANZA’


SABABU 4 ZA WANAWAKE WAJAWAZITO KUFANYA MAPENZI KARIBU KILA SIKU

Baadhi ya wanawake wamekuwa wakiona ujauzito kama mzigo,walioubeba na baadhi wakiona kama zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenye miili yao.

Kubeba ujauzito sio jambo dogo,kukibeba kiumbe tumboni kwa miezi tisa kunaweza kuleta msongo wa mawazo.Zipo njia mbalimbali zinazoweza kumpunguzia mwanamke mjamzito msongo wa mawazo.S.ex katika kipindi cha ujauzito ni best S.ex ambayo huwezi kuipata katika kipindi kingine cha maisha na inasiadia kuimarisha misuli katika njia za uzazi hata baada ya kujifungua.

1.Husaidia presha kushuka.
S.ex katika kipindi cha ujauzito inasidia kushusha presha ya damu.Oxytocin, love homoni inayozalishwa kwa wingi mtu akifanya mapenzi inasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa msongo wa mawazo na kuhakikisha presha iko katika hali ya kawaida ya mwili.

2.Husaidia mjamzito kupata usingizi mnono.
Mjamzito anakumbwa na mambo mbalimbali yanayoweza kumnyima usingizi kama maumivu kwa mbali kwenye uti wa mgongo,kukojoa mara kwa mara,masaa ya kulala kupungua/kuonekana mafupi fetus anavyozidi kukua katika mfuko wa uzazi.S.ex katika kipindi cha ujauzito kunamsaidia mwanamke kufika kileleni na hivyo kupata usingizi mnono kwani huisi kupungukiwa na mzigo(anarelax).

3.Inasaidia mwanamke kuwa karibu zaidi na mumewe kwenye kipindi hiki.
Bond kati ya mume na mke inaendela kuwepo kwani wanaweza kuendelea kufanya mapenzi kwenye kipindi hiki cha ujauzito.Wanawake katika hiki kipindi wanakuwa na hali isiyo ya kawaida na mara nyingi huwa na hasira wanatakiwa kuangaliwa kwa umakini.Oxytocin inamfanya mwanamke awe anajali,na kuamini kuwa mpenzi wake anamjali.
4.Kupunguza maumivu
Homoni kama oestrogen,prolactin na progesterone zinasaidia damu kupita kwa wingi katika maeneo ya nyonga,na hata kwenye uke uongeza hisia na utelezi.


DIAMOND PLATINUMZ AWATAJA WATANZANIA ANAOTAMANI KUKUTANA NAO USO KWA USO


Mwanamuziki Diamond Platnumz Agosti 2 akifanya mahojiano na kituo cha redio ameulizwa kuwa, tayari...
Mwanamuziki Diamond Platnumz Agosti 2 akifanya mahojiano na kituo cha redio ameulizwa kuwa, tayari amefanikiwa kukutana na watu wengi duniani, watu wa tasnia mbalimbali, akipata nafasi ya kukutana na watu wawili Tanzania, Je! atamchagua nani?
Akijibu swali hilo, Diamond ametaja watu wawili na kueleza sababu kwanini anataka kukutana nao, watu hao ni;-
1. Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli. Alisema, amewahi kukutana naye wakata hajawa Rais, hivyo angependa kukutana nae sasa hivi aone reaction ya Rais kwake kama itakuwa sawa na ile ya wakati wa kampeni au itakuwa ya namna gani.

2. Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Kampuni ya Bakhresa Group, Said Salim Bakhresa. Alisema anatamani kujua ni namna gani mfanyabiashara huyu anaweza kufanikisha mambo yote anayoyafanya. Alisema Bakhresa ana biashara nyingi, lakini zote zinakwenda vizuri. Diamond alisema licha ya yeye kuwa mwanamuziki lakini pia anapenda kufanya biashara.

MAGAZETI YA TANZANIA LEO ALHAMISI YA TAR 4 AUGUST KEENYE HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,MICHEZO .


 

Gallery

Popular Posts

About Us