KINGAZI BLOG: 07/08/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, July 08, 2016

Picha 5:Polisi wanne wauawa Dallas, Marekani






Maafisa wanne wa polisi mjini Dallas nchini Marekani wamepigwa risasi na kuuawa huku wengine saba wakijeruhiwa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi.

Maafisa wa polisi katika mji ulio katika Jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha (snipers).

Msako mkali unaendelea kuwasaka washambuliaji hao, mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema.
Maafisa wengine saba wa polisi wamejeruhiwa, Bw Brown amesema.

Kati ya hao majeruhi,wawili wamefanyiwa upasuaji wa dharura na mmoja yumo mahututi.

Ufyatuaji risasi ulianza waandamanaji walipokuwa wakipitia barabara za mji na kuwafanya waandamanaji kukimbilia usalama wao.

Maandamano hayo yametokana na kuuawa kwa wanaume wawili weusi, Philando Castile Jimbo la Minnesota na Alton Sterling eneo la Baton Rouge Jimbo la Louisiana.

Magazeti Ya Tanzania Leo Ijumaa ya July 8, Ikiwemo Habari ya Magufuli Kufyeka Kizazi cha JK



Bozi: Wa ku-date na mimi ajipange sana!




MSANII wa filamu Bongo ambaye pia anauza nyago kwenye video mbalimbali za wanamuziki, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema kutokana na maisha yalivyo, mwanaume anayetaka ku-date naye lazima ajipange sana.

Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi, Bozi alisema yeye kama msichana anayekwenda na wakati hawezi kukubali kujiweka kwa mwanaume kapuku kwa kuwa, ikiwa hivyo lazima atachepuka tu.

“Unajua sababu ya wasichana wengi kusaliti wapenzi wao ni kutotimiziwa na wapenzi wao, unaweza kukuta unahitaji hiki, ukimwambia baby wako anakuambia hana kitu, anatokea mtu anakuambia sema unachotaka unadhani kwa maisha ya sasa utakataa, lazima utasaliti tu,” alisema Bozi

Msemaji wa Yanga Jerry Muro Afunguka Baada kufungiwa Kujishughulisha na Soka Tanzania.


Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Yanga Jerry Muro jioni ya July 7 2016 ameingia kwenye headlines baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya maadili, kutangaza kumfungia mwaka mmoja kujihusisha na soka na faini ya Tsh milioni 3.

Jerry Muro amefungiwa na kamati ya maadili kwa makosa mawili, moja alilifanya mwaka 2015 la kukaidi kulipa faini ya Tsh milioni 5 iliyoamuliwa kulipa na kamati ya nidhamu baada ya kufanya makosa, kosa ambalo limemfanya afungiwe mwaka mmoja kujihusisha na soka.

Kosa la pili ni kutuhumiwa kuchochea vurugu kuelekea mchezo wa Yanga wa Kombe la shirikisho dhidi ya TP Mazembe uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, baada ya hukumu hiyo Jerry Muro ameongea haya:

“Taarifa hizo nimezisikia japo kwa sasa nipo kijijini Machame kwa ajili ya likizo yangu, nimesikia watu wameandika kwenye mitandao kuwa nimefungiwa, lakini mimi nipo Machame na maamuzi yao yametoka nikiwa likizo Machame, yaani wametoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja”

Tatizo la kuvurugika mzunguko wa hedhi


TATIZO la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huwapata wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa na wale waliomaliza majukumu yao ya uzazi.

Tatizo linapojitokeza huleta athari nyingi kwa mwanamke kwa kumfanya ashindwe kupangilia mipango yake.

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA

Mwanamke hulalamika kutofahamu vizuri siku zake, hajui anaingia lini, yaani damu inaweza tu kutoka na inachukua muda mrefu hata zaidi ya siku saba ikiwa nyingi au matone matone. Mwanamke hushindwa kupangilia siku za kupata mimba, tatizo huanza taratibu na mwishowe huchukua muda mrefu.

CHANZO CHA TATIZO

Tatizo hili huweza kusababishwa na kuvurugika kwa mfumo wa homoni mwilini, hasa homoni au vichocheo vinavyoendesha na kudhibiti hedhi na uzazi kwa ujumla.

Uwepo wa uvimbe ndani ya kizazi au kwenye vifuko vya mayai pia ni tatizo. Mabadiliko katika tabaka la ndani la kizazi, maambukizi sugu ya kizazi na kuharibika kwa mimba ni mojawapo ya matatizo haya yanayochangia siku za hedhi zitoke bila ya mpangilio.

Matumizi ya baadhi ya madawa na hata dawa za uzazi wa mpango kwa wengine mfano sindano au vipandikizi huweza kuvuruga homoni na kusababisha matatizo haya.

DALILI ZA TATIZO

Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika kutokufahamu mwenendo wa mzunguko wake, hulalamika damu kutoka muda mrefu au siku chache sana chini ya siku tatu, wakati mwingine hapati kabisa.

Anaweza kuwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu, maumivu wakati wa hedhi, maumivu wakati wa kujamiiana na hata damu kutoka mabonge au nyingi na nyepesi. Pia ataelezea ni muda mrefu anatafuta mtoto lakini hapati.

UCHUNGUZI

Tatizo hili humuathiri mwanamke kwa kiasi kikubwa hasa pale damu inapotoka kwa muda mrefu kwa zaidi ya siku saba au asipopata kabisa hedhi katika umri wake kama unamruhusu, pia mwanamke hatakuwa vizuri anapopata maumivu wakati wa hedhi, au anapotafuta mtoto halafu hapati ujauzito.

Uchunguzi hufanyika katika kliniki za madaktari bingwa wa akina mama katika hospitali za mikoa, vipimo mbalimbali vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa. Vipimo pia vitazingatia mahitaji ya mwanamke kama yupo tayari kushika ujauzito kwa kipindi hicho. Kwa hiyo katika upimaji atachunguzwa na mfumo wake wa uzazi.

NINI CHA KUFANYA?

Ni vema mwanamke mwenye matatizo haya akazingatia ushauri wa daktari wake ili aweze kupona na kufanikiwa malengo yake ya kupata ujauzito. Baada ya uchunguzi wa kina ndipo utaratibu wa matibabu unaanza.

Mwanamke ambaye ameshafikia ukomo wa kuzaa yaani zaidi ya miaka arobaini na tano na ana matatizo haya basi azingatie sana uchunguzi na tiba.

Pamoja na kwamba tumeona vyanzo mbalimbali vya tatizo hili, lakini pia tusisahau saratani au kansa ya shingo ya kizazi na ya kizazi kwa ujumla vinabidi vichunguzwe kwani dalili zake hazitofautiani sana na matatizo mengine. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.

 

Gallery

Popular Posts

About Us