KINGAZI BLOG: 06/14/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, June 14, 2016

Africa's Electricity: Needs are being met with innovative new projects



Africa´s entire installed capacity for electricity generation of 147 GW (Gigawatts) is equivalent to that of Belgium and to what China installs every two years.
     
inShare
0

A satellite image of the world at night shows a brightly lit Europe covered with starry dots and in sharp contrast, a dark, unlit Africa.

More than a century after the light bulb was invented, African school children “often cannot read after dusk, business cannot grow, clinics cannot refrigerate medicine or vaccines, and industries are idled hampering economic growth, jobs, and livelihoods,” says a report by the World Bank.

According to the U.S. government, there are 1.2 billion people on the planet who live without electricity and half of them are in sub-Saharan Africa. The total installed capacity in Africa is 147 GW, the equivalent of the total capacity installed in Belgium, according to the International Energy Agency. It is also roughly the equivalent of what China installs every two years.

Other comparisons show the gigantic gap between our richly lit “first” world and unlit Africa. For instance: one refrigerator in the U.S. consumes in one year six times more electricity than an average person in Tanzania.

Yet, the continent has enormous power potential: huge rivers, vast reserves of oil and gas, coal, as well as the resources for solar, wind and geothermal energy. But it lacks infrastructure for generation, transport and distribution or the capacity to finance projects.

Since the mid-1990s, external finance to Africa’s power sector has averaged only around $600m per year of public assistance, plus a similar volume of private finance, according to the World Bank.

Indeed, according to the International Energy Agency, sub-Saharan Africa needs more than $300bn in investment if it wants to achieve universal electricity access by 2030.

With Africa having already achieved an average growth rate of 5%, new projects are being developed which require new sources of financing, in particular from the private sector. Following is a brief presentation of some of the most exciting ones:

Ghana: the largest solar park in Africa.

Already an exporter of electricity, oil and gas, Ghana is on course to develop the largest solar photovoltaic park in Africa. In this sense, it is leading the way among African countries looking to develop renewables as a viable solution to reduce their dependency on oil imports.

The 155 MW Nzema solar park, which will have about 630,000 photovoltaic panels, is scheduled to start operating by mid-2015. Plans for the $400m plant were first unveiled in December 2012 as part of Ghana’s initiative to expand its renewable energy industry, which is set to produce 10% of its energy needs by 2020.

Rwanda: harnessing volcanic gases from Lake Kivu

Lake Kivu, in Rwanda, just at the border with the Democratic Republic of the Congo, is a rare “exploding lake” that contains an estimated 256 cubic kilometres of carbon dioxide (CO2) and 65 cubic kilometres of methane.

A groundbreaking project is being carried out here to produce electricity by extracting the methane trapped deep in the water. The state-owned Kibuye Power plant already produces 3.6 MW but the government forecasts Lake Kivu could provide about a third of Rwanda’s electricity within two years.

Already, local and foreign investors are committing hundreds of millions of dollars to new methane plants along the lakeshore, both in Rwanda and DR Congo (the border between the two countries crosses the lake). According to a research by Bloomberg Energy Finance, Rwanda could generate 100% of its electricity through renewable sources by 2030.

Tanzania: a  British-built wind farm

Although it has considerable resources in natural gas –estimated at 41.7 trillion cubic feet– which it is beginning to exploit to produce much needed electricity, Tanzania, East Africa’s second largest economy, is also looking into renewable sources of power.

PICHA: PROFESA JAY NAYE ATINGA NDANI YA WCB,DIAMOND AFUNGUKA HAYA.




Linah Aweka Hisia zake za Mapenzi Kwa Mwanamuziki Darasa..Asema Anatamani Kuzaa Naye mtoto


Linah amesema anatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za rapper Darassa.

Muimbaji huyo amesema kwa jinsi ambavyo amewahi kukaa na Darassa na kumsikia akiongea kwa muda mfupi, alibaini kuwa anaweza kuwa baba mzuri.

“Ni mtu ambaye ana sifa zote za kuweza kuwa mwanaume ambaye namtaka. Namchukulia kama kaka yangu yaani sijawahi kumfeel kimapenzi lakini nimekaa naye kwa muda mfupi, nimemuona ni mtu fulani mwenye busara. Ni mwanaume ambaye nikimuona nasema ‘this guy, I wish ningekuwa nina hisia za kimapenzi naye. Katika wasanii wote I wish my boyfriend angekuwa hivi,” Linah ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Ameongeza kuwa Darassa anajua kuwa anakumbali na rapper huyo pia anamkubali Linah na ukaribu wao ni wa kama kaka na dada tu.

Chid Benz' ajiunga katika lebo ya WCB

Msanii maarufu wa miondoko ya kufoka/kurapu Rashid Abdallah Makwiro al maarufu kama CHID BENZ amejiunga rasmi katika lebo ya Wasafi Classic Baby WCB jana mchana Iliyo chini ya mwanamuziki machachari kabisa Diamond platnumz.

Taarifa hizi zimepatikana kupitia mtu wa karibu sana wa Babu Tale. Na pia kituo cha kuaminika cha redio yaani CloudsFM kimetaarifu mchana wa jana.

PICHA:Mdada aliyetikisa mtandao wa instagramu jana usiku

Anajulikana kwa jina la #Nancystery huko instagram,huyo ndio anayetikisa mtandao wa instagram Jana usiku,hizi APA no baadhi ya picha zake zilizozua gumzo mtandaoni!!!


Ben Pol Afunguka 'Muungano wa Diamond Platnumz na Rich Mavoko na WCB


Mkali wa wimbo ‘Moyo Mashine’, Ben Pol amefunguka na kuzungumzia hatua ya Diamond Platnumz kumsani msanii kubwa kama Rich Mavoko katika label yake WCB.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Ben Pol amesema hatua ya Diamond kuamua kumsaini Rich Mavoko katika label ya WCB, itafungua njia kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.

Ni vizuri sisi kwa sisi tukaaminiana na kufanya kolabo kwenye kazi,” alisema Ben Pol. “Diamond ni mpiganaji na Mavoko ni mtu ambaye ana kipaji na mjanja mjanja, kwa hiyo muungano wao unaweza kuleta mapinduzi makubwa katika muziki,”

Pia muimbaji huyo amewataka wale wasanii wenye uwezo wa kuwasaidia wenzao wasisite, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbele zaidi.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE YA TAR 14 JUNE KWENYE HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA,MICHEZO NA UDAKU





Viongozi wa CUF wamkana Profesa LIPUMBA wadai kilichomfanya aondoke bado kipo,kwa nini arudi????


Wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akitengua uamuzi wake wa kung’atuka kwenye wadhifa huo na kuomba kurejea, viongozi wa juu wa chama hicho wamepinga hatua hiyo wakisema katiba yao hairuhusu na kwamba anakwenda kukiua chama.

Kauli za viongozi hao, zimekuja muda mfupi baada ya Profesa Lipumba kutangaza nia hiyo jana kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, Buguruni huku akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kuombwa.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema Lipumba hawezi kuwa na nia njema ya kukijenga chama hicho endapo atarudishwa kwenye nafasi aliyoikataa.

“Anataka kuja kukiharibu chama,”alisema Mazrui. Alifafanua kuwa tayari chama hicho kimefanya mambo mengi bila Lipumba ambaye alikuwa anaona kila kinachoendelea, hivyo alichokisema hakina mashiko kwani CUF ilisharidhia kuitisha mkutano wa uchaguzi kujaza hiyo.

Akieleza sababu alizozitoa mwenyekiti huyo, Mazrui alisema haoni chochote cha maana.“Sababu zilizomuondoa zingalipo. Kinachomrudisha ni nini?” alihoji naibu katibu mkuu huyo.

 Alisisitiza kuwa Wazanzibari wanaendelea na mchakato wa kuidai haki yao iliyoporwa Oktoba 25 na hawana nafasi ya kushughulika na masuala yasiyokuwa na tija kwao, hivyo haoni kama kuna sababu ya kumjadili Lipumba na nafasi yake badala ya kuendelea pale walipo.

 “CCM wanaona kinachoendelea, hivyo wameona wamtumie Lipumba kuja kuharibu mipango yetu. Hatuna muda wa kumjadili.Tunataka haki iliyoporwa,” alisisitiza. 

Msimamo wa Mazrui haukutofautiana sana na ule wa Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Twaha Taslima aliyebainisha kuwa amesikia taarifa za kurudi kwa Profesa Lipumba, lakini haoni uwezekano huo. 

“Katiba hairuhusu hilo.Hakuna kifungu kinachotoa nafasi kwa kiongozi aliyejiuzulu kurudi kwenye nafasi yake pindi atakapotaka kufanya hivyo,” alisema Taslima.

Aliielezea Ibara ya 117 (2) iliyotumiwa na Profesa huyo kuandika barua ya kutengua uamuzi wake, kuwa inatoa tafsiri zaidi ya moja hivyo kuwapo haja ya viongozi kukutana na kujadili suala hilo kabla ya kutoa maamuzi.

Kwa kuwa hakuwapo kwenye mkutano huo, Taslima alisema:“Tunahitaji kukutana haraka na kujadili. Tutafanya mkutano wetu na tutavijulisha vyombo vya habari ndani ya wiki hii.”

Taslima alisema kipindi alichoongoza kilikuwa na changamoto nyingi ambazo ni tofauti na sasa, hivyo haoni haja ya mtu mwingine kuja wakati mambo yametulia. Chama hicho kilipanga kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo Agosti mwaka huu.

Baada ya kung’atuka kwa Lipumba, Taslima alichukua mikoba yake na kukivusha chama hicho kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, pamoja na ule wa Zanzibar ambao uliahirishwa na chama hicho kususia marudio yake Machi 20 mwaka huu.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama hicho, Abdul Kambaya alisema upo uwezekano wa Lipumba kurudi kwenye nafasi yake kwasababu mpaka sasa haijazibwa.

“Mwenyekiti huchaguliwa au kutenguliwa na halmashauri kuu. Haikupitisha kujizulu. Barua ya kujiuzulu itaenda pamoja na hii ya kutengua uamuzi wa awali,” alisema Kambaya.

Kauli ya Lipumba 

Awali, Profesa Lipumba alisema mara kadhaa amekutana na viongozi wa dini na chama pamoja na wanachama wa CUF na wote walikuwa na ujumbe mmoja tu…’rudi tukijenge chama.’ 

Profesa Lipumba hakushiriki mchakato wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ambao kwa upande wa Zanzibar, kutokana na hitilafu zilizojitokeza ulifutwa na kurejewa Machi 20 mwaka huu huku chama hicho kikiwa kimesusia marudio hayo. 

Pamoja na hayo yote, Lipumba alisema ametafakari sana juu ya hali ya kisiasa Zanzibar na kuona umuhimu wa kutoa ushirikiano ili mambo yaende kwa manufaa ya taifa. 

“Ni lazima nchi iendeshwe kwa misingi ya demokrasia ambayo itapatikana kwa umoja wetu.Nimerudi kushirikiana na wenzangu kutimiza malengo hayo ili kuchangia maendeleo ya Tanzania,” alisema Profesa Lipumba. 

Lipumba aliachana na uongozi wa chama hicho, Agosti 8, mwaka jana, siku chache baada ya vyama vinavyounda Ukawa kukubaliana kumsimamisha Edward Lowassa.

Alimuandikia barua Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Shariff Hamad kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama chake kuridhia makada waliohama Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Lowassa, kupewa fursa ya kugombea nafasi za uongozi.

Baada ya kukatwa kwenye mchujo wa ndani ya CCM, Lowassa akiwa na makada kadhaa wa chama hicho akiwamo aliyewahi kuwa waziri mkuu, Frederick Sumaye, alihamia Chadema ambako alipewa fursa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kilichomo ndani ya Ukawa.

Lipumba hakukubaliana na hilo, alikaa pembeni na kuachia ngazi ingawa alishiriki tukio la kumkaribisha Lowassa ndani ya Ukawa.

Jana, wakati anatangaza kufanya mabadiliko ya kile alichokiamua miezi 10 iliyopita, hakuruhusu maswali, ila alifafanua kile kitakachofuata baada ya kuwasilisha ombi hilo, kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho: “Katibu Mkuu anashauriana na wanasheria kabla suala langu halijapelekwa kwenye halmashauri kuu kama katiba inavyosema,” alisema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba Atangaza Kurejea Kwenye Nafasi yake ya Mwenyekiti wa CUF taifa.


HATIMAYE Prof. Ibrahim Lipumba, aliyekuwa Mwenyekti wa Chama cha Wananchi (CUF) ametangaza kurejea kwenye nafasi yake ya uenyekiti-taifa wa chama hicho.

Amesema, anarejea kwenye nafasi hiyo baada ya muda wa kutosha alioutumia kutafakari siasa za nchini na namna demokrasia inavyokanyagwa na watawala wa nchi hii.

“Nimemwandikia Katibu Mkuu (Maalim Seif Sharif Hamad) kutengua barua yangu niliyoandika 5 Agosti mwaka jana,” amesema Prof. Lipumba.

Prof. Lipumba alijiuzulu nafasi yake mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na uamuzi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumridhia Edward Lowassa kupeperusha bendera ya umoja huo kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 kupitia Chadema.

Hata hivyo amesema, analazimika kurejea kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa kutokana na kuguswa na matatizo ya demokrasia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam amesema kuwa, amemuandikia barua Maalim Seif ili atengue uamuzi wake wa awali wa kuachia nafasi hiyo.

Katiba ya mwaka 1992 Toleo 2013 Ibara ya 117 inaeleza kwamba, barua ya kujiuzulu inapaswa kujadiliwa na Mkutano Mkuu kujadili jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika.

Prof. Lipumba aliteuliwa kutwaa nafasi hiyo na Mkutano Mkuu mwaka 1999. Ibara hiyo inaipa mamlaka mkutano huo kukubali ama kukataa kujiuzulu kwake na kwamba, kauli yake ya leo kuwa Maalim Seif atengue barua yake inatokana na kutokwenda kwenye ngazi hiyo (Mkutano Mkuu) nyingine ya uamuzi.

Prof. Lipumba amesema kuwa, dhuluma iliyofanyika katika visiwa vya Zanzibar ya kuporwa kwa haki ya wananchi, imemsukuma kurejea kwenye mapambano ya haki nchini.

Amesema, demokrasia ya Tanzania ina matatizo akitaja miongoni mwayo ni Bunge kuendesha kwa itikadi ya chama.

Pia amesema  kuwa, uongozi wa Rais John Magufuli unaonekana kuwa wa kasi isiyojali Demokrasia.

Akizungumzia Zanzibar amesema, chama chao na watanzania wapenda haki hawatambui utawala wa Dk. Ali Mohammed Shein visiwani humo kwa kuwa hakupatikana kwa njia halali ya kidemokrasia.

Amesema kuwa, Rais Magufuli asipozingatia  misingi ya demokrasia nchi haitakuwa na uwajibikaji.

 

Gallery

Popular Posts

About Us