KINGAZI BLOG: 06/03/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, June 03, 2016

Magufuli: Wanaopita Kwenye Barabara za Mwendokasi Chomoeni Tairi za Magari Yao Muuze.



Rais John Pombe Magufuli achukizwa na uharibifu na matumizi mabaya ya miundombinu ya mabasi ya mwendo kasi na kuagiza mamlaka zinazohusika ziwachukulie hatua kwa wasiofuata sheria.

Amewataka wachukue magari yao na wapeleke kituoni kisha wachomoe matairi ya watuhumiwa wauze na watakuwa wamepata biashara Msikilize Hapa 

Nay wa Mitego Anaimba Hip Hop Kama Taarab, Abadilike – Gigy Money


Video vixen machachari, Gigy Money amedai ni muda wa rapper Nay wa Mitego kubadilika kwasababu anachokisikia kwenye nyimbo zake ni taarab na sio hip hop ya ukweli.

image

Gigy ambaye hapo awali amewahi kuzinguana na hitmaker huyo wa ‘Nasaka Pesa’ baada ya kutumika kwenye video ya Shika Adabu Yako ya rapper huyo na kutolipwa ujira wake, amemuambia mtangazaji wa Jembe FM ya Mwanza, JJ kuwa hip hop ya Nay imejaa uswahili mwingi.

“Inabidi abadilishe uimbaji wake uwe wa kisasa zaidi. Nay anaimba hip hop as taarab, imekuwa ni lugha ya mafumbo wakati hip hop ni zamani ilikuwa inatritiwa nyimbo sexy ambazo anasikiliza mtu akiwa ametulia,maneno unayasikia,” amesema Gigy. “Lakini yeye anataka kuimba vitu vingi katika muda mmoja halafu anaponda, so he is bad to me kwa asilimia 00.0.”

Kwa upande mwingine Gigy amesema msanii wa hip hop anayemkubali Tanzania ni Joh Makini.

“Anajielewa, hana skendo, yaani ana nyota yake kali, msafi,” amesisitiza.

“Anaimba vizuri, unamsikia hata kama ni M-Arusha, yaani R na L zinatofautiana.”

Wabunge wa CCM wamepinga shinikizo la wapinzani kutaka kumuondoa naibu spika Dk.Tulia

Baada ya June 2 2016  kambi rasmi ya upinzania bungeni kutoa tamko la kutaka Naibu spika wa Tanzania Dr. Tulia Ackson aondolewe madarakani kwa azimio la kuvunja sheria inayoendesha bunge, leo June 3 2016 Wabunge wa CCM wamepinga shinikizo hilo.

Wakiongea mbele ya Waandishi wa habari Dodoma, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Abdallah Possi ambaye amesema..>>’Kitu alichokifanya Naibu spika amefanya kwa mujibu wa kanuni, na kama watu hawakuridhika na maamuzi kanuni zinatoa njia ya wao kuyakatia rufaa ‘

‘Kile ambacho Spika amefanya na hii movie inayoendelea sasa ni vitu viwili tofauti na kwakweli haina maana yoyote zaidi ya sarakasi, kwahiyo alichokifanya Spika ni sahihi kwa asilimia mia‘

Naye Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni mbunge wa Muleba hajalikalia kimya hili>>>’Matukio ambayo yanatokea hapa bungeni mimi kwa uzoefu wangu na umri wangu nimeliangalia kwa mtizamo wa kitamaduni na kijinsia ‘

‘Jamii inaona mtu akitolewa nje lakini haioni ule mchakato kwasababu bunge halipo live, jamii ijitambue kwamba tunampinga Tulia Ackson amekosea au kwasababu ni mwanamke kijana. ‘

MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO.


Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi bungeni mjini Dodoma Juni 3, 2016.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (kulia)  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye wakiteta na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah Bungeni mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maaluum, Lucy Mayenga kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa CCM kutoka Wilaya ya Ruangwa, Salum Seif Mapatu (kushoto) na Idrisa Said Mtalika kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Mzumbe waliotembelea Bunge kwa Mwaliko wa Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete  (mwenye kanzu katikati) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Basi la mwendo kasi Lagongana na Pikipiki Shekilango Dar es Salaam

Ajali zimeendelea kutokea katika barabara za mabasi yaendayo haraka ambazo zimekuwa zikisababishwa na madereva wasiotaka kufuata sheria za barabarani ambapo leo katika mataa ya kuongozea magari Shekilango basi moja liendalo haraka limegongana na pikipiki.

Ajali hiyo ambayo haikusababisha vifo wala majeruhi imetokea majira ya saa sita ambapo kwa mujibu wa mashududa dereva wa boda boda akiwa na abiria mwanamke alikuwa akikatiza kwenye taa hizo akitokea upande wa soko la shekilango akielekea milleniam park huku taa zikiwa zimeruhusu basi hilo kupita na kusababisha kugongana na pikipiki kupinduka.

Askari wa usalama wakiwa katika harakati za kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo akatokea dereva
mwingine wa bodaboda kukatiza katika eneo hilo bila kufuata sheria ambaye nae alikamatwa na kuambatanishwa na waliosababisha ajali hiyo na kupelekwa kwenye vyombo vya dola kwa hatua zaidi.

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA TPDC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Prof. Sufian Hemed BUKURURA kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia tarehe 30 Mei, 2016.

Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.), amewateua wafuatao kuwa  Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC kuanzia tarehe 3/6/2016 hadi tarehe 2/6/2019;

1. Mhe. Jaji Josephat M. Mackanja

2. Balozi Dkt. Ben Moses

3. Prof. Abiud Kaswamila

4. Prof. Hussein Hassani Sosovele

5. Dkt. Shufaa Al-Beity

6. Bi. Mwanamani Kidaya

Imetolewa na;

KATIBU MKUU 

3 JUNI, 2016

Profesa Tibaijuka: Wapo Waliochota Fedha za Escrow Lakini Wamenyamaziwa


Jinamizi la kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow bado linamsumbua mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka baada ya kuliibua kwenye semina ya mapambano dhidi ya ufisadi, akichongea wabunge ambao hawajaguswa.

Profesa Tibaijuka alipoteza uwaziri wa nyumba, ardhi na makazi kwenye sakata hilo baada ya kubainika kuwa aliingiziwa fedha zinazoonekana zilitoka kwenye akaunti hiyo iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja na Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Profesa Tibaijuka alikuwa mmoja kati ya viongozi wa ngazi ya waziri, mbunge, jaji na viongozi wa dini walioingiziwa fedha ambazo zinatokana na Sh306 bilioni zilizochotwa kwenye akaunti hiyo.

Akichangia katika semina hiyo inayolenga kuwajengea wabunge uwezo wa kupambana na ufisadi na ambayo iliandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Ufisadi (ACFE), Profesa Tibaijuka alisema wakazi wa jimbo lake walimchagua kwa mara nyingine licha ya tuhuma za Escrow kwa sababu hawakuziamini.

Alisema fedha hizo za Escrow zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kwenda benki ya Stanbic na Mkombozi, lakini cha ajabu majina ya watu waliopewa fedha kupitia benki moja yalitolewa na yale ya benki nyingine yalifichwa.

Alisema inakuwaje yeye anakuwa katika tuhuma, wakati aliyempa fedha hizo hatuhumiwi.

Watu waliotajwa kwenye sakata hilo ni wale waliopewa fedha zilizopitia benki ya Mkombozi, lakini hadi sasa wale waliopewa fedha zinazodaiwa kuwa ni taslimu kutoka Stanbic hawajatajwa.

Alisema sheria pekee yake haiwezi kufanya lolote katika mapambano dhidi ya ufisadi na hakubaliani na wabunge wanaosema kuwa hata kama mahakama imeshindwa kuthibitisha ufisadi, watuhumiwa wataifishwe mali zao.

“Sisi wabunge hatukuja kufanya kazi hiyo, tumekuja kutunga sheria ili zisaidie katika kutuongoza,” alisema.

“Ni vyema kuzungumzia unyofu wa watu kwa kuanzia katika shule, makanisa, misikiti na wabunge.”

Aliituhumu Takukuru kuwa inakubali kutumiwa kwa kuchagua kesi za kuchunguza.“Tume ya Maadili ndio usiseme,” alisema.

“Mie nimeshawahi kushtakiwa Tume ya Maadili, najua kuwa kuna mbunge mwenzetu hapa alipata fedha za Escrow, lakini kwa sababu hakuwa mzungumzaji ameondoka bungeni wala hakuna mtu anajua kama alipata. Unaona jinsi ambavyo hawa watu hawako makini,” alisema.

Mbunge wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu alilia na watu aliowaita wazushi kwamba wanawazushia wenzao kuchukua rushwa wakati hakuna ukweli.

Hiki ndicho alichojibu Wema kuhusiana na katuni hii aliyochorwa na mastaa wengine wenye uhusiano na mastaa wanaowazidi umri

Hivi karibuni gazeti moja la udaku liliwachora mastaa wa kike wenye uhusiano na mastaa wa Bongo wanaowazidi umri. Mastaa hao ni pamoja na Jacqueline Wolper aliyechorwa akimnywesha uji mpenzi wa Harmonize anayeonekana akiwa amebeba mdoli.

Wengine ni Wema Sepetu akiwa amempakata Idris Sultan, Zari the Bosslady akimweka Diamond kwenye kitolori cha kuwafundishia watoto kucheza na Aunty Ezekiel akiwa amembeba mgongoni mpenzi wake Mose Iyobo.

Ni Wema pekee ndiye aliyeijibu kwa kupost picha hiyo kwenye akaunti yake na kuandika: Aliechora hii natamani tu nimuone… Nimpe mkono. Leo nimeongeza siku za kuishi wallahy…. I jus laughed too much today….. Ukisoma na dialogue ndo unakufa kabisa…. Nimeipenda hio ya “Aogopa Mimi… Aogopa chacha.”

Aliyewalisha watu nyama ya mbwa azua taharuki!


Akiwa ameshika upaja wa nyama ya mbwa.

TANGA: Kitendo cha kijana aliyefahamika kwa jina la Zakaria Swaki, mkazi wa Kijiji cha Mlalo, wilayani Lushoto mkoani Tanga kukutwa na hatia ya kuwalisha watu nyama ya mbwa kimezua taharuki huku wengi wakidai kuwa, kwa hali ilivyo watakuwa hawawaamini wauza nyama.


Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, wananchi hao wa Mlalo na viunga vyake walisema walikuwa wanatilia shaka nyama aliyokuwa akiuza kijana huyo hivyo kutiwa kwake hatiani kunaonesha alianza kufanya hivyo muda mrefu.

“Kwa kweli nimeshitushwa sana na taarifa hii, sina hata hamu ya kula tena nyama maana inavyoonekana amewauzia watu nyama hiyo kwa muda mrefu,” alisema Jamali Shemshahuo, mkazi wa Kijiji cha Ngazi. Naye Mama Jenny anayefanya biashara ya kuuza pombe za kienyeji maeneo ya Misheni alisema:


“Niliwahi kununua nyama kwa yule kijana lakini niliitilia shaka licha ya kwamba niliipika na kuwauzia wateja wangu. “Halafu sasa, wapo walioisifia supu yake kuwa ni tamu, kumbe maskini nilikuwa nawalisha nyama ya mbwa. Yule kijana akafungwe tu maana ametutia kwenye dhambi kubwa ila tumepata fundisho la kutojinunulia nyama mtaani.”

Kijana huyo alitiwa mbaroni hivi karibuni kufuatia tuhuma za kwamba amekuwa akiwauzia wananchi nyama ya mbwa ambapo alifikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Mlalo na akakiri kufanya kosa hilo. Kufuatia kukiri huko, kijana huyo alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela ambapo ameshaanza kukitumikia katika Gereza la Lushoto.

 

Gallery

Popular Posts

About Us