KINGAZI BLOG: 03/26/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, March 26, 2016

Adele aomba msamaha baada ya shabiki kujeruhiwa

Image result for adele

Adele
Mwanamuziki wa muziki wa Pop Adele ameomba msamaha baada ya shabiki mmoja kujeruhiwa

Mkenya aliyejiweka katika picha za wengine

 Sevelyn
Mwanamke mmoja kutoka Kenya amejiweka katika msururu wa picha za likizo za watu wengine katika mtandao wake wa facebook.
 
Sevelyn
Baada ya kushindwa kuwa na uwezo wa kusafiri kwenda barani Asia,Sevelyn Gat alijiweka katika picha karibu na ndege,katika ukuta mkubwa wa Uchina na hekalu moja.
 
Sevelyn akisema anaondoka Kenya
Picha hizo zilizowekwa kwa njia ya nzuri ili zisiweze kubainika kuwa za uongo zilikuwa mbaya zaidi na hivyobasi kuweza kupendwa na mara nyingi sana.
 
Sevelyn akisema kuwa ni siku yake ya mwisho akiwa china
Mfanyibiashara wa Nairobi sam Gachuru amejitokeza na kumsaidia kutafuta fedha ili kwenda likizo.
 
Sevelyn
Kulingana na Sich Chirpse Sam aliwasumbua rafikize kuchangisha fedha za mahala pa kulala,nauli bima na pesa za kutumia.
 
Seve Gats
Seve pia amepata kibali chake cha kuzaliwa anemtuma ombi la pasipoti na amepata kufunzwa kama meneja wa mradi.

Video za Justin Bieber zatazamwa mara bilioni 10

  Justin Bieber
Mwanamuziki Justin Bieber amevunja rekodi ya Vevo kwa video yake kutazamwa mara bilioni 10.
Msanii huyo wa Canada ambaye alitoa kibao kipya Purpose in Novemba alipata idadi hiyo katika kipindi cha miaka sita na miezi mitatu au siku 2,316.

Wanariadha wala sabuni wakidhania ni chakula


Wanariadha waliokuwa wanakimbia mbio ndefu za marathon walijipata wamekula sabuni baada ya kudhania kwamba zilikuwa chakula kutokana na kukosa kuelewa lugha ya kiingereza.
Takriban wanariadha 20,000 katika mbio za Qinyuan marathon kusini mwa mkoa wa Guangdong nchini Uchina walipata zawadi mda mfupi baada ya kumaliza mbo hizo katika utepe kulingana na gazeti la kila siku nchini humo la Peoples daily.
Wakidhania kwamba walikuwa wanakula chakula,wanariadha hao badala yake walikuwa sabuni zilokuwa zikinuka harufu nzuri .
Walioshuhudia wanasema kuwa sabuni nyingi zilitupwa kandakando ya barabara huku zikiwa zimeumwa.
Tatizo ni kwamba sabuni hizo zilikuwa zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza na hivyobasi wanariadha hao hawakuelewa lugha hiyo kulingana na gazeti hilo.
Hatahivyo walioandaa mbio hizo waliomba msamaha.Pakiti za sabuni hizo zilikuwa kama zile za chakula.
 
 
Sabuni zilizowekwa katika pakiti na kunuka vizuri kama chakula
Pia kulikuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya majeraha katika mbio hizo huku wanariadha 12,200 wakihitaji kupatiwa matibabu wakati na hata baada ya mbio hizo.
Haijulikani ni majereha mangapi yalisababishwa na kisa hicho cha sabuni.

Wagombea warushiana matusi Marekani


Wagombea wa urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican Ted Crus na Donald Trump walirushiana cheche za matusi katika mjadala
Wagombeaji wawili wa Urais wa chama cha Republican nchini Marekani wamegombana vikali na kurushiana matusi juu ya wake zao

New AUDIO | Yemia Alade Ft. Sauti Sol - Africa | Download


New AUDIO | Shery Zuu Ft. Msaga Sumu - Babu Uyo | Download

Official VIDEO | Sam Misago - Ballin And Chillin

https://youtu.be/E6LrT4psIPk

MAALIM SEIF AREJEA ZANZIBAR BAADA YA MAPUMZIKO HOTELINI DAR.

Image result for maalim seifSiku chache baada ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliosusiwa na baadhi ya vyama vya upinzani, Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea Zanzibar.

Maalim Seif ambaye alikuwa mapumzikoni katika hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam kwa takribani siku 17, jana alirejea Zanzibar kuendelea na mapumziko yake.

Maalim Seif alilazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal ya jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuruhusiwa March 8 mwaka huu alishauriwa na Daktari wake kupata mapumziko ya muda mrefu.

Kurejea kwa Maalim Seif visiwani humo kunazidisha shauku na kiu ya baadhi ya Wazanzibar kutaka kusikia atakachokisema kiongozi huyo wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.

Maalim Seif aliugua wakati Wazanzibar wakiwa katika maandalizi ya kurudia uchaguzi mkuu uliofanyika March 20, mwaka huu baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar( ZEC), Jecha Salim Jecha kwa madai kuwa uligubikwa na dosari nyingi.


Gharama za Hotelini
Taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari siku chache zilizopita zilidai kuwa kila siku aliyokaa kwenye hoteli hiyo, Maalim Seif alikuwa akitumia wastani wa Sh. 6,162,500.


Kutokana na takwimu hizo, hadi kufikia jana, Maalim Seif atakuwa ametumia kiasi kisichopungua sh. Milioni 92.4


Chumba alichokuwa akilala Maalim Seif katika Hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano kinalipiwa dola za Marekani 2,500 kwa usiku mmoja.


Maalim Seif alikuwa akiishi hotelini hapo na wasaidizi wake watano, ambao wote gharama zao zinalipwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ

Majambazi mipaka ya Kenya, Tanzania wauawa



WATU sita, wakiwemo wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi hatari katika mipaka ya Tanzania na Kenya, wameuawa katika mji wa Isebania, Kenya wakati wa uporaji fedha kutoka duka la mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi katika eneo la

Kificho ang’oka uspika zanzibar


ALIYEKUWA Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa zaidi ya miaka 20 sasa, Pandu Ameir Kificho, ameng’olewa katika nafasi hiyo baada ya kushindwa katika kura za kuwania awamu nyingine ya uongozi wa baraza hilo.

Haya hapa Magazeti ya leo March 26 2016 kwenye,habari za`kitaifa kimataifa Udaku, na michezo

March 26 2016 nakuletea habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye ,habari za kitaifa,kimataifa Michezo na udaku na stori nyingine kali ili ujue kilichojiri duniani.. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook/tanzaniampya news blog,  pia kwenye twitter @tanzaniampysasa.

20160326_043306 20160326_043331
20160326_043401
20160326_043415
20160326_043430
20160326_043445
20160326_043502
20160326_043516
20160326_043536
20160326_043548
20160326_043607
20160326_043619
20160326_043633
20160326_043646
20160326_043700
20160326_043711
20160326_043731
20160326_043740
20160326_043752
20160326_043803
20160326_043816
20160326_043840
20160326_043855
20160326_043905
20160326_043917
20160326_043928
20160326_043940
20160326_043948
 

Gallery

Popular Posts

About Us