KINGAZI BLOG: 06/07/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, June 07, 2016

Rais Magufuli Apokea Shilingi Bilioni 12 Ya Tume Ya Uchaguzi Zilizokuwa Zimebaki Baada ya Uchaguzi Mkuu

Ra

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekabidhi shilingi Bilioni 12 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, zilizobaki baada ya uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha kwa Rais Magufuli leo tarehe 07 Juni, 2016 Ikulu Jijini    Dar es Salaam na kueleza kuwa bakaa ya fedha hizo haikuathiri kwa namna yoyote uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

"Mheshimiwa Rais fedha ambazo tunakukabidhi, tulijibanabana sana, japo muda wenyewe ulikuwa mfupi lakini tulijibanabana sana bila kuathiri utendaji wa shughuli za uchaguzi, isije ikawa inatoa sura kwamba iliathiri, haikuathiri, na katika hali hiyo kama ambavyo wengi ni mashahidi, hatujisifii, lakini uchaguzi ulienda vizuri" Amesema Jaji Mstaafu Lubuva.

Akizungumza baada ya kupokea mfano wa hundi hiyo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuokoa fedha hizo na kuzirejesha serikalini ili zipangiwe majukumu mengine na ametaka taasisi nyingine za serikali ziige mfano huo wa uzalendo na kutanguliza maslahi ya taifa.

"Kitendo hiki ambacho mmekionesha leo, kinaonesha ni kwa namna gani Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya uongozi wako Mheshimiwa Mwenyekiti ilivyo na watu makini na waadilifu sana, kwa sababu hizi fedha ambazo kwa lugha uliyotumia ni bakaa, kutokana na zile ambazo mlipewa zaidi ya Shilingi Bilioni 270, mkatumia shilingi Bilioni 261.6, mkabakiza shilingi Bilioni 12, mngeweza kuamua kusema hamkubakiza na hakuna mtu yeyote ambaye angewauliza, na saa nyingine pengine hakuna mtu yeyote ambaye angejua, mngeweza pia kusema kiasi mlichotupa hakijatosha, tunaomba mtuongezee ama mngetengeneza maneno mazuri mazuri ya matumizi, bado nina uhakika serikalini wasingejua" Amesema Rais Magufuli.

Pamoja na kukabidhi hundi ya bakaa ya shilingi Bilioni 12, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amemuomba Rais Magufuli aisaidie tume hiyo kupata jengo lake la ofisi kwa kuwa hivi sasa tume inatumia majengo ya kupanga ambayo yanaigharimu tume hiyo takribani shilingi Bilioni 1 na Milioni 400 kila mwaka kwa kulipia kodi ya pango, usafiri na gharama nyingine za uendeshaji.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amelikubali ombi hilo na kuamua kuwa fedha ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeziokoa (Shilingi Bilioni 12) kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana zitumike kujenga ofisi ya tume, na amependekeza ofisi hiyo ijengwe mkoani Dodoma.

"Na mimi ningefurahi zaidi kama hilo jengo lingejengwa Dodoma, kwa sababu Dodoma ndio makao makuu ya nchi hii, na hasa kwa sababu Dodoma ni katikati ya Tanzania"Amesisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amelikubali pendekezo la tume hiyo la kuanzishwa kwa mfuko wa tume ya uchaguzi ambao utakuwa unakusanya fedha kila mwaka kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaofuata, badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kusubiri mwaka wa uchaguzi ndipo zitengwe fedha zote za kugharamia uchaguzi huo.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es Salaam

07 Juni, 2016


;

MIKOPO YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ST JOSEPH YAFUTWA RASMI

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha St Joseph (SJUIT) Kampasi ya Arusha (kilichofutiwa usajili), waliokuwa chini ya programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi, wametakiwa kusoma ngazi ya cheti au stashahada.

Kama watataka kusoma ngazi ya juu, watapaswa kuomba upya udahili.

Aidha, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imesema wanafunzi waliokuwa wakipata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),mikopo yao pia imesimamishwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Simon Msanjila alitoa agizo hilo jana kupitia taaarifa kwa vyombo vya habari.

Profesa Msanjila alisema hatua hiyo, inatokana na kubainika kwamba wanafunzi hao hawastahili kusoma shahada na pia hawakustahili kupewa mkopo.

“Tunawafahamisha wanafunzi wa SJUIT waliokuwa kwenye programu ya miaka mitano kwamba watatakiwa kuishia daraja la cheti na stashahada… Kama wanafunzi hao watataka kuendelea na masomo ya juu, watatakiwa kuomba upya,” ilisema taarifa hiyo.

Februari 25, mwaka huu, Wizara kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) baada ya kujiridhisha kuwa Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Joseph Tanzania imepoteza sifa na vigezo vya kuendelea kutoa elimu ya chuo kikuu, ilifuta kibali cha kuanzishwa kwake.

Iliidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote, waliokuwa wanasoma katika Kampasi hiyo ya Arusha kwa gharama za Chuo Kikuu cha SJUIT.

Aidha, ilifuta udahili wa wanafunzi wapya katika programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi.

Ilielekeza wanafunzi waliokuwa wakiendelea na masomo katika programu hiyo, wahamishiwe katika Kampasi ya Luguruni, Dar es Salaam.

TCU ilielekeza kwamba wanafunzi watalazimika kwanza kuhitimu katika ngazi ya Stashada, kama ilivyokuwa imeidhinishwa na Tume hapo awali.

Wanafunzi waliohamishiwa kwenye vyuo mbalimbali, waendelee na masomo.

Taarifa hiyo ilisema wakati wa mchakato wa uhamisho, wanafunzi wote walihakikiwa kubaini kama wanakidhi vigezo vya kusoma kwenye ngazi hiyo.

Wanafunzi wote waliokuwa wakisoma programu hiyo ya miaka mitano, walihamishiwa kwenye Kampasi ya Luguruni, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kutokana na mchakato wa uhakiki, baadhi ya wanafunzi walikutwa hawana sifa za kujiunga na mafunzo hayo ya ualimu.

Wale waliobainika kuwa na sifa, walitaarifiwa kuendelea na masomo kwenye kampasi hiyo ya Luguruni.Wanafunzi katika kundi hili waliobainika kuwa na vigezo, walitaarifiwa kuendelea na masomo katika Kampasi ya Luguruni.

“Maana ya kuwa na vigezo vya ufaulu tunavyovizungumzia hapa ni kwamba wanafunzi husika wamefaulu katika masomo lengwa yanayowawezesha kusoma Cheti cha Ualimu Daraja “A” ambacho ni kigezo cha kwanza kwa mujibu wa mtaala wa programu hiyo.”

Chanzo:GPL

Jeshi la Polisi Lapiga Marufuku Maandamano na Mikutano Yote ya vyama vya Siasa




Ndugu zangu waandishi wa habari,
Katika siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi nchini, limepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano . hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder).

Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao.

Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.

Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 07/06/2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.

Jeshi la Polisi linawataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi. 

Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.

Aidha Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.

Asanteni sana kwa kunisikiliza .

Imetolewa na:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi.

Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa Jaji kiongozi leo juni 7

Rais Magufuli amteua Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji Kiongozi




Mbunge Godbless Lema asema: Sishangai Waziri kuingia Bungeni Amelewa wakati kulikuwa na bar ndani ya uzio wa bunge


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) ameeleza kutoshangazwa na taarifa za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kuingia Bungeni na kujibu swali akiwa amelewa kwani awali kulikuwa na bar ndani ya uzio wa Bunge.
Lema ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, aliyasema hayo katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV, ambapo alieleza kuwepo kwa tatizo kubwa la ulevi ndani ya Bunge ambalo kimsingi linatokana na kukosekana kwa maadili.
“Wakati wa mikutano ya Bunge la Katiba, kulikuwa na bar mbili ndani ya uzio wa Bunge. Kwahiyo, sishangai suala la mbunge kuingia ndani ya Bunge akiwa amelewa kama mwanzo kulikuwa na mazingira hayo,” alisema Lema na kuongeza kuwa hivi sasa hazioni tena bar hizo katika eneo la Bunge.
Alisema kuwa tatizo la ulevi linalitafuna Taifa na linaogofya kusikia watunga sheria wanaingia ndani ya Bunge wakiwa wamelewa lakini dawa ya tatizo hilo ni kuandaa Taifa katika misingi ya maadili.
Alisisitiza kuwa ili kuwa na Taifa lenye maadili, ni vyema somo la Maadili likaanza kufundishwa tangu shule za msingi ili kujenga jamii yenye maadili mema na hofu ya Mungu. Lema aliwataka Watanzania kuhakikisha wanajenga familia zilizo na maadili na misingi bora ili kuandaa Taifa lenye maadili na hofu ya Mungu

NAFASI YA KAZI HIZI HAPA NBC BANK MWISHO WA MAOMBI TAREHE 16 JUNE 2016



HEAD OF RETAIL BANKING

POSITION DESCRIPTION:

NBC BANK
Head of Retail Banking (1 position)
Job Grade: Director
Reporting to: Managing Director
Head Office: Dar es Salaam

Key Objectives:

CIR reduction
Improve Branch profitability
Market Leader In Digital banking
Net promoter score, Improve multi products engage clients

Job Purpose:
• To lead and direct the strategic delivery of all Retail Banking activities across the Country. This will include, but not limited to, planning and coordinating with product heads In Country and at lower case Level to optimize the relevance of retail banking product and services across Retail, Business Banking, Products and Channels to ensure a fully integrated strategy and seamless delivery of retail banking solutions. Drive and deliver change required to ensure we succeed in our vision of becoming the Go To Bank, while optimizing the 5 C’s (Customer & Client, Colleague, Citizenship, Conduct, and Company). Formulate, drive and deliver on business strategic objectives for retail banking, with specific focus on a deep understanding of the local markets and customers while leveraging the available expertise and economies of scale of the regional office. Ensure the infrastructure required to deliver the business plan Is in place and the service levels agreed with the various Infrastructure heads. CIR reduction, Improve Branch profitability, Market Leader in Digital banking, and Improve multi products engage clients

Main Responsibilities:
Provide strategic leadership

Outputs to deliver this accountability:
Stay abreast of Industry trends, role players and in country opportunities and challenges to ensure that the business is well positioned to provide competitive and industry leading product and services.
Identify strategic role players and stakeholders and engage all stakeholders, role players and Industry forums to understand changes to strategy, regulations and markets.
Direct the review and design of the optimal business model and deliver on required changes to ensure the business maintain competitive advantage, meet client expectations, reduce cost and Improve profitability

Drive sustainable cost and processing efficiencies within retail benchmarking and alignment to best practices leveraging the global, regional and local matrix
Scan the external market to understand future challenges and ensure that retail banking is well positioned to anticipate market Changes
Drive business performance directly and through enabling functions
Outputs to deliver this accountability:

For areas managed by this role, Implement performance controls to proactively measure achievement against strategic targets and address changes or non-performance.
Implement governance structures and stakeholder frameworks to ensure effective customer management and engagement.
Build and maintain effective stakeholder relationships within the industry and within the Bank to ensure the unit is successfully positioned to manage risks and expectations and deliver on shareholder value.

Drive and influence the enabling functions to meet business requirements and enable the business to achieve the retail banking objectives continuously.
Participate and contribute to industry and Bank wide forums and governance structures as required or directed.

Maintain a healthy risk profile
Outputs to deliver this accountability:
Drive a culture of proactive compliance and risk management within the executive team and the function as a whole.
Manage the financial sustainability and effective use of resources with
Outputs to deliver this accountability:
Drive the annual planning and review of MTP, STP and Revised Annual Forecast (RAF) budgets for the function including the setting of MTP and STP Financial targets and standards and related measures and anticipated financial cost targets.
Ensure rigorous cost management within Business by implementing a highly structured budget, monitoring and reporting process and instilling discipline within the team around cost control.
People Management
Outputs to deliver this accountability:
Together with the Head of HR for the cluster, determine the people management strategy for the area with a focus on talent management development, resourcing and retention.
Establish and maintain a succession plan for the key roles in the area and review and approve succession plans for one level below.
Review reward practices and requests in the area, together with Human Resource; ensure alignment to Group Reward framework which includes ensuring consistent and fair
Experience and Qualifications Required
Honours Bose-degree in Finance / Business Sciences or a related NQF Level 6 equivalent qualification (10) years’ experience in the Financial Services sector which must include proven experience (5) years’ experience on a senior management level in a large corporate (5) years Retail/Business Banking Experience

Technical skills /competence
Strategic thinker
Strong Leadership ability
Effective communication skills
Experience managing diverse teams
Experience of operating In a changing environment
Combination of risk awareness and commercial savvy
Relevant senior business leadership experience
Entrepreneurial and commercial thinking
Adapting and responding to change
Coping with pressures and setbacks
Deciding and Initiating action
Delivering results and meeting customer expectations
Knowledge, Expertise and Experience
In-depth understanding of full range of Retail, Local Business and an overview of Corporate.
Good understanding of Retail risk policy.
Maintain up to date knowledge of competitor and local market activity.

Remuneration:

Attractive salary including performance based bonus on achieving targets and overall business performance

APPLICATION INSTRUCTIONS:

NBC IS AN EQUAL OPPORTUNITY EMPLOYER
Applicants are invited to submit their CVs, copies of certificates,2 reference and their contacts to; Priscilya Othman
Resourcing Lead
National Bank of Commerce (NBC)
Priscilya.Othman@nbctz.com

If you are not contacted by NBC within thirty (30) days after the closing you should consider your application is unsuccessful

Source Guardian,3rd June 2016

MAGAZETI YA LEO JUMANNE 07/6/2016 KWENYE HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA UDAKU NA MICHEZO




 

















CCM Yatangaza Kuzunguka Nchi Nzima Kuharibu ngome za CHADEMA na wote waliopanga kumchafua Rais Magufuli Magufuli.


Siku chache baada ya Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kuishtaki kwa wananchi Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, CCM wamejibu mapigo  kwa kuapa kuwafuata kila kona watakayopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema kuwa chama hicho hakiwezi kuvumilia kuona Chadema wanazunguka kuharibu taswira ya Rais Magufuli na Serikali yake ambayo alieleza kuwa imefanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi katika kipindi kifupi.

Alisema kuwa wamepata taarifa zisizo na shaka kuwa Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana Mei 16 mwaka huu ilibaini kuwa kwa muda mfupi, Magufuli ametekeleza ajenda zote ilizokuwa ikinadi wakati wa Uchaaguzi Mkuu.

Ole Sendeka alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli unatuma ujumbe wa dhahiri kuwa Chadema watashindwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Aliongeza kuwa malalamiko ya udikteta wanayoyasambaza yanaonesha kuwa hawana mjadala wowote wa kumkosoa Rais Magufuli.

“Tunawaonya viongozi wa Chadema. Wanapaswa kutumia majukwaa hayo kunadi sera za Chadema. Nataka kuwahakikishia kuwa, kama Chadema wataenda sehemu fulani Jumatatu, sisi tutakuwa pale Jumanne kusafisha hali ya hewa kwa kuwaeleza ukweli wananchi,” alisema Ole Sendeka.

Chadema wamepanga kufanya mikutano nchi nzima kwa kile walichoeleza kuwa ni kuishtaki Serikali kwa wananchi kuhusu mwenendo wa Serikali ikiwa ni pamoja na kubanwa kwa Demokrasia na Bunge kwa ujumla na utumbuaji majipu usiofuata sheria na taratibu.

Rais Mseveni Amteua Mkewe KuwaWaziri mkuu wa nchi hyo


 Rais Yoweri Mseveni na Mkewe, Janeth Mseveni.

Kampala, Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, jana alitangaza Baraza lake jipya la mawaziri 50 huku akimteua mkewe Bi. Janet Kataaha Museveni kuwa Waziri wa Elimu na Michezo.

Bi. Janeth Mseveni

Baraza Jipya la Mawaziri la Uganda.

H.E. the Vice President ─ HON. KIWANUKA EDWARD SSEKANDI
Rt. Hon. Prime Minister ─ DR. RUHAKANA RUGUNDA
1st Deputy Prime Minister & Deputy Leader of Gov’t Business in Parliament─ GEN. MOSES ALI
2nd Deputy Prime Minister and Minister of East African Affairs ─ HON. KIRUNDA KIVEJINJA
Minister of Education and Sports ─ HON. JANET KATAAHA MUSEVENI.
Minister of Public Service ─ HON. MURULI MUKASA
Minister of Trade, Industry & Cooperatives ─ HON. KYAMBADDE AMELIA ANNE
Minister of Internal Affairs ─ GEN. JEJE ODONGO
Minister of Agriculture, Animal Industry and Fisheries ─ HON. VINCENT SSEMPIJJA
Minister of Finance and Economic Planning ─ HON. KASAIJA MATIA
Minister of ForeignAffairs ─ HON. SAM KUTESSA KAHAMBA
Minister of Health ─ DR. ACENG JANE
Minister of Works and Transport ─ ENGINEER NTEGE AZUBA
Minister of Lands, Housing & Urban Development ─ HON. BETTY AMONGI (UPC)
Minister of Water & Environment ─ HON. SAM CHEPTORIS
Minister of Justice & Constitutional Affairs ─ MAJ. GEN.KAHINDA OTAFIIRE
Attorney General ─ MR. BYARUHANGA WILLIAM (ADVOCATE)
Minister of Defence and Veteran Affairs ─ HON. ADOLF MWESIGE
Minister of Local Government ─ HON. TOM BUTIME
Minister for Karamoja Affairs ─ HON. JOHN BYABAGAMBI
Minister of Energy and Minerals ─ HON. MULONI IRENE
Minister of Information, & Communications ICT ─ HON. FRANK TUMWEBAZE
Minister for Science, Technology and Innovation─ DR. TUMWESIGYE
ELIODA
Minister in Charge of General Duties/Office of the Prime Minister ─ HON. MARY KAROORO
OKURUT BUSINGYE
Minister of Disaster Preparedness & Refugees ─ HON. ONEK HILARY
Minister of Tourism,Wildlife and Antiquities ─ EPHRAIM PROF. KAMUNTU
Minister for the Presidency ─ HON. MBAYO ESTHER MBULAKUBUZA
Minister of Security ─ LT. GEN. HENRY TUMUKUNDE
Minister without Portfolio ─ HAJJI NADDULI
Minister for Kampala City Authority─ HON. KAMYA BETTY
Government Chief Whip – HON. SENTAMU RUTH NANKABIRWA
Minister of Gender, Labour & Social affairs ─ HON. JANAT MUKWAYA
MINISTERS OF STATE:
Office of the President:
Minister of State for Economic Monitoring ─ HON. KASIRIVU BALTAZAH ATWOKI
Minister of State for Ethics and Integrity Office of the Vice President: ─ HON. SIMON LOKODO
Minister of State Vice President’s Office of the Prime Minister:─ HON. ONZIMA ALEX
Minister of State for Relief and Disaster Preparedness ─ HON. ECWERU MUSA FRANCIS
Minister of State for Northern Uganda ─ HON. GRACE KWIYUUCWINY
Minister of State for Karamoja ─ HON. MOSES KIZIGE
Minister of State for Luwero Triangle ─ HON. GALABUZI DENNIS SSOZI
Minister of State for Teso Affairs ─ HON. AKIROR AGNES
Minister of State for Bunyoro Affairs Ministry ─ HON. KIIZA ERNEST
Minister of State for Public Service ─ HON. DAVID KARUBANGA
Ministry of East African Affairs
Minister of State for East African Affairs ─ HON. MAGANDA JULIUS WANDERA
Ministry of Agriculture, Animal Husbandry and Fisheries
Minister of State for Agriculture ─ HON. CHRISTOPHER KIBAZANGA
Minister of State for Fisheries ─ HON. RUTH ACHIENG
Minister of State for Animal Industry ─ MRS. JOY KABATSI
Ministry of Defence and Veteran Affairs
Minister of State for Defence ─ COL. SAM ENGOLA
Minister of State for Veteran Affairs ─ BRIGHT MAJOR RWAMIRAMA
Ministry of Education and Sports
Minister of State for Higher Education ─ DR. MUYINGO JOHN CHRYSOSTOM
Minister of State for Primary Education ─ HON. NANSUBUGA ROSEMARY SENINDE
Minister of State for Sports ─ HON. CHARLES BAKABULINDI
Ministry of Energy and Mineral Development:
Minister of State for Energy ─ HON. SIMON D’UJANGA
Minister of State for Minerals ─ HON. LOKERIS AIMAT PETER
Ministry of Finance, Planning & Economic Development:
Minister of State for Finance (General) ─ HON. AJEDRA GABRIEL GADISON ARIDRU
Minister of State for Planning ─ HON. DAVID BAHATI
Minister of State for Privatization and Investment ─ HON. EVELYN ANITE
Minister of State for Micro- Finance ─ HON. HARUNA KYEYUNE KASOLO
Ministry of Works and Transport:
Minister of State for Transport ─ HON. AGGREY BAGIIRE
Minister of State for Works ─ HON. OROT ISMAEL
Ministry of Water and Environment:
Minister of State for Water ─ HON. RONALD KIBUULE
Minister of State for Environment ─ HON. KITUTU MARY
Ministry of Lands, Housing and Urban Development:
Minister of State for Housing ─ DR. CHRIS BARYOMUNSI
Minister of State for Urban Development ─ HON. ISAAC MUSUMBA
Minister of State for Lands ─ HON. PERSIS NAMUGANZA
Ministry of Health:
Minister of State for Health (General) ─ HON. OCHIENT SARAH OPENDI
Minister of State for Primary Health Care ─ DR. MORIKU JOYCE
Ministry of Justice and Constitutional Affairs
Deputy Attorney General ─ HON. MWESIGWA RUKUTANA
Ministry of Trade and Industry and Cooperatives:
Minister of State for Trade ─ HON. WERIKHE MICHEAL KAFABUSA
Minister of State for Industry ─ HON. HARRIET NTABAZI
Minister of State for Cooperatives ─ HON. GUME FREDRICK NGOBI
Kampala Capital City Authority ─ HON. NAMUGWANYA BENNA
Ministry of Foreign Affairs:
Minister of State for International Affairs ─ HON. ORYEM OKELLO
Minister of State for Regional Affairs ─ DR. PHELEMON MATEKE
Ministry of Local Government
Minister of State for Local Government ─ HON. JENNIFFER NAMUYANGU
Ministry of Tourism, Wildlife and Antiquities:
Minister of State for Tourism ─ HON. KIWANDA GODFREY
Ministry of ICT
Minister of State for ICT and Communications ─ HON. NANTABA AIDA ERIOS
Ministry of Gender, Labour and Social Development:
Minister of State for Gender and Culture ─ PEACE MADAME MUTUUZO
Minister of State for Youth and Children Affairs ─ MRS. NAKIWALA FLORCENCE KIYINGI
Minister of State for Labour, Employment and Industrial Relations ─ HON. KABAFUNZAKI
HERBERT
Minister of State for the Elderly and Disability ─ ADRIAN MRS. TIBALEKA
Ministry of Internal Affairs
Minister of State for Internal Affairs ─ HON. OBIGA KANIA

DIAMOND PLATINUMZ NI LEVEL ZA KIMATAIFA,LEO KAJA NA HILI HEBU ONA HAPA






MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) YATOA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2016.


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa mwelekeo wa hali ya hewa kwa kipindi cha Juni hadi Agosti mwaka huu. Akizungumzia kuhusiana na mwelekeo huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Bw. Samwel Mbuya alisema “Nchi yetu inatarajia kuwa na hali ya baridi kiasi katika kipindi hiki sambamba na vipindi vifupi vya mvua vinavyotarajiwa kujitokeza katika maeneo machache hususanya ukanda wa Ziwa Viktoria na ukanda wa pwani ya Kaskazini (Visiwa vya Unguja na Pemba).

Katika kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti 2016, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya baridi kiasi katika majira haya ya kipupwe. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha matarajio ya hali ya joto la wastani hadi chini ya wastani katika maeneo yaliyopo Kusini-magharibi mwa nchi. 

Hata hivyo,katika msimu wa Kipupwe wa mwaka huu maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kuwa na joto la wastani hadi juu ya wastani. Aidha, izingatiwe kuwa hali ya ubaridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi mapema asubuhi. “Aliendelea kueleza sababu za hali hiyo kuwa ni pamoja na kupungua kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya Pasifiki sambamba na Joto la baharí katikaeneo la magharibi wa bahari ya Hindi kuwa la wastani kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2016”. 

Aidha, joto katika bahari ya Atlantiki linatarajiwa kuwa chini ya wastani. Hali hiyo inatarajiwa kusababisha upepo kuvuma kutoka magharibi ukielekea mashariki hususankatika maeneo ya Ukanda wa Ziwa Viktoria. Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la ncha ya kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi.

Kwa upande mwengine, Afisa Uhusiano wa TMA, Bi. Monica Mutoni alitoa msisitizo kwa wananchi kufuatilia taarifa hususan za tahadhari zinazotolewa na Mamlaka kupitia vyombo mbalimbali vya habari, tovuti ya Mamlaka n.k ili kuokoa maisha na mali. Bi. Monica alisema “Hivi karibuni TMA imekuwa ikitoa tahadhari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa kwenye ukanda wa Bahari Hindi, Maziwa na nchi kavu hivyo ni vyema wananchi hasa wale watumiaji wa bahari na maziwa kuchukua hatua stahiki pindi taarifa kama hizo zinapotolewa”.

Aidha, TMA ilipongeza sekta mbalimbalipamoja na Taasisi, Mamlaka za Serikali na jamii kwa ujumla kwa hatua stahiki zilizochukuliwa katika kipindi chamsimu wa mvua za Masika 2016 kwa kutumia Taarifa, Agalizona Tahadhari za utabiri zilizotolewa na Mamlaka. Ni wazi kuwa kwa hatua hizo madhara ambayo yangeweza kujitokeza yalidhibitiwa na hivyo kuchangia katika kufanikisha mipango na utekelezaji wa shuguli za kiuchumi na kijamii katika kipindi husika.

Kwa tarifa ya kina kuhusiana na mwelekeo wa hali ya hewa kwa mkoa wako ingia kwenye tovuti ya TMA www.meteo.go.tz au tembelea ofisi zetu

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

 Meneja wa Kituo Cha Utabiri Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. Samwel Mbuya akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mwelekeo wa Hali ya joto na mvua katika kipindi cha juni hadi Agosti 2016 ambapo inatarajiwa kuwa na hali ya baridi kiasi na vipindi vifupi vya mvua. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi Monica Mutoni

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)na vyombo vya Habari Leo Jijini Dar es salaam.

 

Gallery

Popular Posts

About Us