KINGAZI BLOG: 05/12/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, May 12, 2016

Kinyambe kuzikwa kesho Kwao Mbeya.



Marehemu James Peter a.k.a Kinyambe

MSANII wa vichekesho James Peter Nsemwa maarufu kama Kinyambe ambaye alifariki dunia jana mkoani Mbeya, atazikwa kesho katika makaburi ya Uyole mkoani Mbeya.
Baba wa marehemu, mzee Lugendelo Nsemwa, ameuambia mtandao huu akiwa nyumbani kwake Uyole, kuwa mwanaye ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa uchekeshaji,
alianza kuumwa tangu Juni mwaka jana, ambapo tumbo na miguu ilikuwa imejaa maji. Alisema tatizo hilo lilipelekea mapafu yake kushindwa kufanya kazi sawasawa.
“Kwa kipindi kirefu alikuwa amelazwa katika hospitali binafsi ya Abaja iliyopo Uyole, lakini Mei 9 mwaka huu, hali yake ilibadilika, alizidiwa na kupoteza fahamu, kitu kilichofanya tumkimbize katika hospitali ya mkoa wa Mbeya iliyopo maeneo ya Forest ya zamani, ambako alilazwa katika wodi ya ‘private’ chumba namba 4, na bahati mbaya jana (Jumatano) saa 3.5 akafariki dunia,” alisema mzazi huyo.
Katika hali ya kushangaza, mzazi huyo alisema jina la Mohamed Abdalah, ambalo linafahamika kwa wengi kama ndilo halisi la msanii huyo, yeye halitambui, kwani tangu amezaliwa alipewa jina hilo na hakuwahi kusikia kama alilibadili.
Aidha, aliwalaumu wasanii wenzake kwa kutotoa msaada wowote wakati wa ugonjwa, kwani kwa kipindi chote hakuwahi kuwaona wasanii wa Dar es Salaam wala kupata salamu zao, zaidi ya kuwaona wale wa Mbeya ambao nao walikuwa wakienda mara mojamoja.
Daktari mmoja wa hospitali hiyo aliyemhudumia marehemu tangu alipolazwa, ambaye jina lake linahifadhiwa kwa kuwa siyo msemaji wa hospitali hiyo, alisema marehemu alipopokelewa na kupimwa, aligundulika kupungua kwa kiwango cha sukari mwilini huku pia akiwa na homa ya mapafu.
Wakati wa uhai wake, Kinyambe aliwahi kuishi na wanawake watatu, ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja, lakini imefahamika kuwa wa kwanza alizaa naye mtoto mmoja, wa pili alizaa naye mtoto mmoja pia, lakini alifariki mwezi uliopita akiwa na miaka mine. Mwanamke wake wa mwisho, ni mjamzito ambaye endapo Mungu atamjaalia, atajifungua mwezi ujao.
Marehemu alijipatia umaarufu kwa vichekesho vyake kupitia vipindi mbalimbali vya televisheni, kikiwemo cha Vituko Show katika Channel Ten na pia aliwahi kufanya kazi na Sharo Milionea.
Mungu Ilaze Roho ya Marehemu Mahali Pema!

ALLY KIBA KUTOA VIDEO MPYA HIVI KARIBUNI,CHECK KIPANDE KIDOGO CHA VIDEO HIYO



Aje video by Ali Kiba to be released soon, as the times going own Kingkiba starts to trend through our Social network of Makubwa haya news, after he starts to post the photos of his new video of Aje by Alikiba, he have reveals through makubwa haya news that he will be releasing his new Video of aje on 13 May 2016, so stay tune with your number one entertainment website of Tanzania Makubwa haya, so that when that date reaches we will be the first site to show you that Video.

Hebu jionee Shilole alivyochapia kiingereza wakati akitambulisha Video mpya.

Video Of Silole Aka Shishi Baby speaking Brocken English by inroducing her new Video of say my name

Picha Diamond na Mafikizolo Walivyotinga Bungeni leo

May 12 2016 kundi maarufu la muziki kutoka Afrika Kusini Mafikizolo pamoja na staa wa bongofleva Diamond Platnumz walipata mwaliko wa kuingia Bungeni Dodoma ambapo wakali hawa wapo Dodoma kwa ajili ya kuidondosha burudani Chuo kikuu Dodoma.


Tazama Video Hapa:

diamondplatnumz

1 hour ago

+ FOLLOW

Ilibidi kujikausha na kueka sura ya userious ili furaha isiwazidi tukaja haribu Hali ya hewa ikawafujo tukapelekwa Polisi bure kwa kusababisha Zogo Bungeni.... too Much Love thanks alot Our People .... Shukran sana Mh Waziri Nape Nauye kwa Mualiko huu #ColorsOfAfrica #Vodacom4G#VodacomOngeaDeilee

4699

156

POWERED BY INK361.COM

Ubonge wa Mwili Wamtesa Joyce Kiria, Ahofia Kuipoteza Ndoa yake.


MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa kupitia EATV, Joyce Kiria ameweka wazi kuwa hivi sasa yuko kwenye mikakati ya kupunguza mwili wake ili asije kupoteza ndoa.
 Akizungumza na Amani Joyce alisema, amekuwa akiuweka mwili wake sawa ili usinenepe sana kwa kuwa hataki tena kuonekana mzee akawapa nafasi wasichana ‘potabo’ wakaingilia ndoa yake na kuipoteza.
“Akuu!! Kisa cha kujizeesha na mwili hata ukitembea na mumeo uonekane kama shangazi yake mimi sitaki kabisa, sasa hivi ni diet kwa kwenda mbele kila kukicha nisije kuwapa madungaembe nafasi ya kuingilia ndoa yangu,” alisema Joyce.

Magazeti ya tanzania yalichoandika leo Alhamisi tar 12 Mei 2016 kwenye habari za kitaifa kimataifa na michezo.


Video: Hebu jionee baadhi ya video za vichekesho za KINYAMBE enzi za uhai wake.

Baadhi ya kazi alizofanya marehemu Kinyambe enzi za uhai wake;akiwa na kundi la vituko show. R. I. P. KINYAMBE


TANZIA:MSANII MAARUFU WA VICHEKESHO KINYAMBE AFARIKI DUNIA

Msanii aliyekuwa anakuja kwa kasi katika Tasnia nzima ya filamu za kuchekesha za bongo (Bongo comedy),Maarufu kama KINYAMBE ambaye jina lake Halisi ni JAMES PETRO NSEMWA  hatunaye tena duniani baada ya kufariki dunia jana usiku. 
 
Habari kutoka kwa ndani ya familia zinasema KINYAMBE amefariki Dunia  baada ya kuugua kwa siku kadhaa japo taarifa zaidi zitaendelea kutolewa juu ya undani wa kifo cha staa huyo wa vichekesho nchini. Kinyambe ataendelea kukumbukwa kutokana na jitihada mbalimbali alizozifanya katika tasnia ya filamu za vichekesho hasa kwa staili na sauti yake ya uchekeshaji wa aina yake.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMINA.
(R.I.P.KINYAMBE)
 

Gallery

Popular Posts

About Us