KINGAZI BLOG: 05/11/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, May 11, 2016

MALAIKA:NIMECHOKA KUFANANISHWA NA LULU WA BONGO MUVI

MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya anayefanya vizuri, Malaika Exavery amesema anakerwa na kitendo cha watu wengi kumfananisha na muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Akizungumza na gazeti hili, Malaika alisema huko nyuma alipokuwa akifananishwa na msanii huyo hakujali, lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda imekuwa ni shida hadi wengine wanamsimamisha.

“Unajua kufananishwa na mtu siyo tatizo, lakini kwa hali ilivyo hivi sasa lazima mtu usikie kuchoka kabisa kwa sababu hata wakati mwingine unaendesha gari mtu anakusi mamisha halafu akikuangalia usoni vizuri anaondoka, anasema alidhani ni Lulu,” alisema Malaika

Huyu ndiye binti wa miaka 19 anayedai kupewa ujauzito na Papa Wemba


Binti wa miaka 19 anadaiwa kuspend one night on the same bed na Hayati Papa Wemba amekua gumzo kwenye mitandao ya kijamii ndani na nje ya Congo(D.R.C) akidai kuwa na ujauzito wa Mfalme huyo wa Rhumba aliefariki April 24 mwaka huu baada ya kuanguka jukwaani jijini Abidjan nchini Ivory Coast.

Picha zinazodaiwa kuwa copied kutoka kwenye akaunti za social media za binti huyo,zinamuonesha akiwa kwenye pozi tofauti za kimahaba na Papa Wemba,picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya picha hizo zikionesha tumbo lake na nyingine zikimuonesha akikiss na Hayati Papa Wemba.

Mpaka sasa hakuna taarifa yeyote rasmi kutoka kwenye familia ya Papa Wemba juu ya madai ya binti huyo ambae baadhi ya mashabiki wa Mfalme huyo wa Rhumba wameahidi kumsaidia kwa lolote hadi atakapojifungua.

Mwanamke Aunda Boti Lenye Umbo kama sehemu zake za siri.

Mahakama moja ya Japan imemwachia huru mwanamke mmoja aliyetengeza boti iliyofanana na uke wake.

Jaji aliamuru kwamba boti ya Megumi Igarashi iliofanana na uke wake na yenye rangi nyingi haikuashiria umbo la uke.

Hatahivyo ,alipigwa faini ya dola 3,700 baada ya jaji kuamuru hakuvunja sheria kwa kusambaza data ya uke wake ambayo inaweza kutumika kutengeza umbo la uke wake.

Sheria kali za Japan zinapinga kuonyeshwa hadharini kwa sehemu za siri.

Igarashi mwenye umri wa miaka 42, kwa jina Rokudenashiko au ”good for nothing girl” alikamatwa mwaka 2014 baada ya boti yake kuonyeshwa katika duka moja la vifaa vya ngono mjini Tokyo.

Alishtakiwa chini ya sheria ya mambo machafu kwa kuonyesha boti hiyo na kusambaza data yake kwa wale waliochangisha fedha ili itengezwe.

Siku ya Jumatatu jaji mmoja aliamua kwamba rangi zake zinazong’aa na mapambo yake hayaonyeshi ukweli wa umbo la uke.

“Lakini data yake licha ya kutokuwa na umbo la uke itatumika kutengeza uke wa Bi Igarashi kwa kutumia 3D na hivyobasi ni uchafu,” alisema jaji.

Bi Igarashi alipigwa faini nusu ya Yen 800,000 zilizohitajika na afisi ya mashtaka.

Source:BBC

SNURA :CHURA IMENIONGEZEA UMAARUFU KWA KASI KUBWA.

STAA wa Muziki wa Kizazi Kipya, Snura Mushi amefunguka kuwa licha ya changamoto ya kutakiwa kutengeneza video mpya yenye maadili ya wimbo wake wa Chura, umaarufu wake umeongezeka kwani jina lake limekuwa gumzo kila kona nje na ndani ya nchi. Akipiga stori na gazeti hili, Snura alisema tangu aanze muziki hajawahi kufanya mahojiano na watu wengi kama kipindi hiki, kwani japokuwa alitakiwa na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kurekebisha wimbo huo, amepata faida kubwa kimuziki na kiakili.
“Ukiachana na changamoto nimefarijika sana kwani jina langu limekuwa gumzo kila kona, nimepata elimu ambayo sikuwa nayo ambapo wizara imenipa ubalozi wa kuwafundisha wenzangu wasitoe nyimbo zisizokuwa na maadili, hivyo kila ninapokutana na wasanii wenzangu nawafundisha,” alisema

Maajabu!!!!! !! ! Mwanamke wa miaka 72 ajifungua mtoto wa kiume.

Daljinder Kaur alitibiwa kwa miaka miwili

Mwanamke wa umri wa miaka 72 amejifungua mtoto mvulana katika hospitali moja nchini India.
Mwanamke huyo alipachikwa mimba kupitia njia ya kitaalamu ya IVF ambapo yai la mwanamke hutolewa kutoka kwenye ovari, kutungishwa mbegu ya kiume na kisha kurejeshwa kwenye mji wa mimba. Yai hilo linaweza kutolewa kwa mwanamke mwingine.

Njia hiyo hutumiwa kuwawezesha wanawake tasa kupata watoto.

Daljinder Kaur alijifungua mtoto wake baada ya kupokea matibabu kwa miaka miwili katika hospitali iliyoko jimbo la Haryana.

Matabibu walifanikiwa kumtungisha mimba kupitia IVF mara yao ya tatu.

Mumewe Kaur ana umri wa miaka 79.

Kisa hicho kimezua mjadala mkali kuhusu kutumiwa kwa teknolojia hiyo ya IVF na umri ambao wanawake wanaweza kuruhusiwa kuitumia kupata watoto.

Dkt Kanad Nayar, katibu mkuu wa chama cha upachikaji mimba nchini India anasema sheria ya kuamua umri wa juu ambao mwanamke anaweza kuruhusiwa kutumia teknolojia hiyo itatungwa karibuni.

Sana umri huo utakuwa miaka karibu miaka 55.

Daktari huyo anasema jambo la kuzingatiwa zaidi ni uwezo wa mwanamke kumlea mtoto hadi akomae.

„Ukimzaa mtoto lazima uweze kumlea mtoto kwa karibu miaka 20 hivi. Huwezi kujifungua mtoto kisha uwaache watu wengine wakimlea,” amesema Dkt Nayar.

Ni mara ya pili kwa mwanamke mkongwe kujifungua mtoto India. Awali, mwanamke wa miaka 70 alijaliwa mtoto nchini humo.
Lakini mwanamke huyo alifariki miaka miwili baadaye na sasa mtoto huyo anatuzwa na jamaa zake.

Hebu mcheki Mtoto wakike wa staa wa filamu za 'Action' Van damme akifanya kama baba yake alivyokuwa.


Mtoto wa nyoka naye ni nyoka vile vile. 

Bianca, binti wa Van Damme

Uzuri wa Bianca Van Varenberg, 25, usikulaghai ukadhani ni binti wa kuchezea tu. Atakupa mkong’oto hadi usahau njia uliyopitia. 

Ni mtoto wa muigizaji mkongwe wa movie za mapigano, Jean Claude Van Damme.

Anajulikana zaidi kikazi kama Bianca Bree. Miaka mitano iliyopita alionekana kwenye uzinduzi wa filamu ya baba yake lakini akawa kimya tena, hadi sasa.

Mwaka 2012 alisema angependa atoke kinyake bila kutumia jina la baba yake ndio maana hajaliweka kwenye majina yake.

Yeye pia anapenda kuja kuwa muigizaji wa filamu.

Kasi ya Watanzania Kujiunga na Makundi ya Kigaidi ya Al-Shabaab na IS Yaongezeka........Waziri Asimulia Wanavyojiunga, Wapinzani Wahoji Wanajeshi Kupewa Ukuu wa Mikoa


Serikali imesema imeshtushwa na wimbi kubwa la vijana wa Kitanzania wanaojiunga na makundi hatari ya kigaidi ya Al-Shabaab na Islamic State, maarufu kama ISIS.

Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake ya Sh trilioni 1.6 kwa mwaka 2016/17.

Dk. Mwinyi alisema pamoja na hali hiyo, Serikali imeendelea kupambana na makundi hayo kwa kila njia ili kuhakikisha nchi inakuwa salama katika maeneo yote, yakiwamo ya mipakani.

Alisema matukio ya kigaidi yameendelea kuwa tishio duniani, hivyo Tanzania inapaswa kuchukua tahadhari ya kila namna.

Dk. Mwinyi alisema kuwapo kwa makundi hayo ya Al-Shabaab, Al-Qaeda, Boko Haram na Islamic State, kunafanya tishio la ugaidi kusambaa duniani kote.

“Taarifa za kuwapo baadhi ya Watanzania wanaojiunga na makundi ya Al-Shabaab na ISIS tunazo, kunahatarisha usalama wa Tanzania, hasa ikizingatiwa kiujumla mwingiliano mkubwa uliopo kati ya wananchi wetu na watu wenye malengo tofauti.

“Hatari iliyopo ni uwezekano wa baadhi ya vijana waliojiunga na makundi ya kigaidi ya kimataifa kurejea nyumbani kwa lengo la kutekeleza vitendo vya kigaidi nchini mwetu.

“Tuna kila sababu ya kujizatiti na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema kipindi kilichopita, kumejitokeza viashiria vyenye mwelekeo wa kigaidi, ikiwemo kuvamiwa baadhi ya vituo vya polisi, kuporwa silaha na baadhi ya askari kuuawa na kundi ambalo nia yake haijafahamika.

“Matukio yenye mwelekeo wa kigaidi, ni kama yaliyotokea katika mapango ya Amboni mkoani Tanga, Kitongoji cha Nyandeo wilayani Kilombero pale Morogoro na kukamatwa mabomu ya kutengenezwa kwa mkono katika maeneo mbalimbali yakiwamo Zanzibar,” alisema.

Alisema pamoja na hali hiyo, kwa upande wa mpaka wa kusini mwa nchi, hali imeendelea kuwa shwari, licha ya uwapo wa utata wa mpaka wa Ziwa Nyasa ambao bado haujapatiwa suluhisho.

Kutokana na hali hiyo, amewataka Watanzania  kuendelea kuchukua tahadhari kwa kutoa taarifa ya matukio yanayotishia kuashiria uvunjifu wa  usalama.

Kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana na ule wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu Zanzibar, alisema umefanyika kwa amani na utulivu, licha ya baadhi ya maadui wa ndani na nje kutabiri mambo mabaya.

“Watanzania tunayo sababu ya kujivunia kuwa uchaguzi mkuu ambao kikalenda ni wa tano tangu kuingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, uliendeshwa na kuhitimishwa kwa amani, utulivu na mshikamano mkubwa kinyume na maadui wetu wa ndani na nje ya nchi waliotutabiria mabaya,” alisema.

Dk. Mwinyi alisema kwa kutambua umuhimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa vijana, Serikali itaendelea na azma yake ya kuwajenga vijana uzalendo, ukakamavu, maadili mema, utaifa na kutoa stadi za kazi.

Alisema kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, suala hilo sasa litatekelezwa kwa kutoa mafunzo kwa baadhi ya vijana wa kujitolea kwa mujibu wa sheria.

“Katika mwaka 2015/16, vijana 27,463 walipatiwa mafunzo mbalimbali, yakiwamo ya kuwapa ujuzi na stadi kazi ili wajiandalie mazingira mazuri ya kujiajiri.

“Nachukua fursa hii kuwaomba vijana wanaopata mafunzo ya JKT, wazingatie maarifa na ujuzi wanaoupata, hususan wa stadi za kazi ili waweze kujiajiri badala ya imani iliyoanza kujitokeza kwa baadhi ya wahitimu kudai ajira kwa maandamano.

“Katika hatua ya kutekeleza agizo la Serikali linalohusu vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuajiri idadi kubwa ya vijana wanaopatiwa mafunzo ya JKT, hadi kufikia Februari, mwaka huu vijana 5,453 waliajiriwa na vyombo vya ulinzi.

“Kati ya vijana hao, 3,521 waliajiriwa na JWTZ, polisi 1,185, Usalama wa Taifa 106, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) 617. Hata hivyo, idadi ya vijana waliopatiwa ajira imeongezeka. Hadi kufikia Aprili, mwaka huu vijana 7,170 wamejiariwa na vyombo hivyo,”alisema Dk. Mwinyi.

==>Kambi ya upinzani wahoji wanajeshi kupewa ukuu wa mikoa

Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, msemaji wa wizara hiyo, Juma Hamad Omar, alihoji hatua ya Serikali kuwateua maofisa wa vyombo vya ulinzi kushika nafasi za kisiasa kama wakuu wa mikoa na wilaya.

Omar ambaye ni Mbunge wa Ole (CUF), alisema Serikali imekuwa na utamaduni wa kuwateua maofisa wa vyombo vya dola waliopo kazini, na baada ya uteuzi huo hufanya kazi kwa mujibu wa chama tawala.

“Wakuu wa wilaya na mikoa wanafungwa na ibara ya 80 (1) (C) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 inayowataja kuwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM katika wilaya husika. Hali kadhalika wakuu wa mikoa wanafungwa na ibara ya 94 (1) (C) inayowataja kuwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM katika mkoa husika.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali itambue ibara 147 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka kwamba; ‘Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara 5 ya Katiba hii’,”alisema Omar.

Akizungumzia utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo, alisema katika bajeti ya mwaka 2015/16 Serikali imeweka rekodi mbaya ya kutoa fedha chini ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge kwa miradi ya maendeleo.

Magazeti Ya Leo Jumatano Mei 11 kwenye habari za kitaifa , kimataifa udaku na michezo.


Rais Magufuli Awasili Nchini Uganda Leo Kuhudhuria Sherehe Za Kuapishwa Rais Museveni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Entebbe, nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni, kesho.

 

 

Gallery

Popular Posts

About Us