KINGAZI BLOG: 06/06/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, June 06, 2016

MPANGO WA KUMWONDOA NAIBU SPIKA DK. TULIA WAIVA ... BARUA YATINGA RASMI OFISI YA BUNGE



Prof Tibaijuka awa gumzo atumia usafiri wa bajaj


Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka, leo ametumia usafiri wa Bajaj hatua inayomfanya kuwa mwanasiasa wa kwanza mashuhuri nchini kutumia usafiri huo hadharani.

Tukio hilo limetokea leo majira ya asubuhi muda mfupi baada ya Profesa Tibaijuka kufungua mkutano wa Kimataifa unaohusu upatikanaji wa majisafi na usafi wa mazingira, mkutano unaoendelea jijini Dar es Salaam ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.

Profesa Tibaijuka ni Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kimataifa la Ushirikiano wa Upatikanaji wa Maji Safi na Salaam lijulikanalo kwa kifupi kama WSSCC ambalo pamoja na mambo mengine ndiyo linalohusika na mfuko wa dunia wa ufadhili wa miradi ya maji ambao unafadhili miradi kadhaa ya upatikanaji wa maji katika wilaya kadhaa za mkoa wa Dodoma.

EATV imefanikiwa kuzungumza na Profesa Tibaijuka ili kufahamu sababu za kutumia usafiri huo unaoonekana kutumiwa zaidi na watu wa kipato cha chini na haya yalikuwa majibu yake "Unajua mimi ni mbunge, ukiwa mbunge ni mwakilishi wa watu kwa hiyo sina tofauti yoyote na wale watu ninaowawakilisha," amesema Profesa Tibaijuka.

Ameongeza kuwa " sasa hivi natakiwa kuwahi ndege uwanja wa ndege kwenda mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoendelea huko kwa hiyo badala ya kutumia usafiri wangu ni bora nitumie hii bajaj ambayo kwa kweli ni msaada sana pale unapotaka kuwahi mahali,"

Idadi kubwa ya wageni waliohudhuria mkutano huo ambao wengi ni kutoka nje ya nchi hawakuamini kile kilichokuwa kikitokea kwani ni nadra kwa kiongozi wa hadhi yake ambaye amewahi kushika nyadhifa kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa na taasisi mbali mbali za kimataifa kutumia usafiri unaoonekana kama ni wa hadhi ya chini.

"Huyu kweli ni kiongozi wa watu, mengi yanaweza kusemwa lakini huyu anaonyesha utu na upendo kwa watu anaowaongoza," alisikika mshiriki mmoja akisema kwa mshangao na kuongeza kuwa hata miradi ya maji iliyotekelezwa chini ya uongozi wake,jimboni kwake na hata mkoani Dodoma inaonyesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.

Awali katika mkutano huo, Profesa Tibaijuka amesema suala la upatikanaji wa majisafi na salama ni muhimu iwapo nchi inahitaji kutokomeza umaskini na kwamba wananchi wanachotakiwa kufanya ni kuzingatia usafi wa mazingira na miili yao kwa kufuata kanuni za afya bora.

Profesa Tibaijuka ameongeza kuwa "Wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa umaskini sio chanzo cha uchafu bali ni tabia ya mtu..hivyo basi licha ya umaskini tulionao kama taifa sio sababu ya uchafu kutawala majumbani kwetu na kuwa chanzo cha magonjwa....kuna haja ya jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na rais Dkt John Pombe Magufuli za kutokomeza uchafu katika jamii kwani kama kiongozi wa nchi yeye mwenyewe ameonekana akichukia uchafu kwa vitendo,"

Kwa upande wake, Mratibu wa Baraza hilo hapa nchini, mhandisi Wilhelmina Malima amesema Tanzania inahitaji uwekezaji mkubwa kwenye miradi ya maji safi na salama na hivyo kuiwezesha kutekeleza lengo namba sita kati ya malengo kumi na saba endelevu ya Umoja wa Mataifa ambayo hujulikana kwa kiingereza kama Sustainable Development Goals au kwa kifupi SDGs.

Lipumba ruksa kuwania umwenyekiti CUF

Dar es Salaam. Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kama aliyekuwa mwenyekiti wake wa Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba anataka kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika Agosti 21, mwaka huu ruksa.

  Agosti 5, mwaka jana Profesa Lipumba alijiuzulu wadhifa huo akisema ataendelea kuwa mwanachama wa kawaida wa chama hicho.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Shaweji Mketo alisema alipozungumza na waandishi wa habari.

Picha:Hatimaye Mwana FA Afunga Ndoa, jana.

Mwana FA unaoa lini? Hatimaye jibu lake limepatikana. Rapper huyo amefunga ndoa Jumapili hii.

Hitmaker huyo wa Asanteni kwa Kuja amefunga ndoa na mchumba wake aitwaye Helga.

Ndoa hiyo ya kiislamu imehudhuriwa na ndugu na marafiki zake wa karibu wakiwemo AY, Hermy B, Ommy Dimpoz, Sallam, Dully Sykes, Alberto Msando na wengine.

Mama Harmonize Amtilia Shaka Wolper


 Jacqueline Wolper Massawe na mkwe wake, mama Harmonize.

DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya staa wa Wimbo wa Bado, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ kumtambulisha mchumba’ke, Jacqueline Wolper Massawe nyumbani kwao katika Kijiji cha Mahuta mkoani Mtwara, siri imevuja kuwa wakati wa zoezi hilo, mama mzazi wa jamaa huyo, anadaiwa kumtilia shaka mrembo huyo juu ya mwanaye na kumpa wosia mzito.

 Tukio la utambulisho huo lilifanyika nyumbani kwa akina Harmonize Mtwara mara baada ya jamaa huyo kutinga mkoani humo kwa shoo yake ya kwanza maeneo hayo tangu alipochomoka kimuziki.

Ilielezwa kwamba, akiwa katika harakati hizo mapema siku ya tukio, Harmonize alikwenda nyumbani kwao na kumtambulisha Wolper kisha usiku wake akampandisha mama yake kumtambulisha kwa mashabiki na baada ya kumtambulisha Wolper ambaye ni staa wa Bongo Muvi.

Rajab Abdulhan ‘Harmonize’na mama yake mzazi.

Chanzo hicho ambacho kilishuhudia hatua kwa hatua ya matukio hayo kilitunyetishia kwamba siku hiyo baada ya kufika Mtwara, Harmonize alikwenda nyumbani kwao na Wolper ambapo baada ya utambulisho, mzazi huyo alionekana kuwa na shaka kwa Wolper juu ya usalama wa mwanaye.

“Kiukweli Wolper amekubalika kwa mama Harmonize ila mzazi huyo alionesha shaka kama kweli Wolper ataweza kuishi na mwanaye maana alidai mastaa wengi wa kike huwa hawadumu kwenye uhusiano wa kimapenzi, hivyo alionesha kuwa shaka kama kweli Wolper atakuwa na nia njema na mwanaye au yupo kwa ajili ya kuchota vijisenti kisha ammwage kama ambavyo wasanii wengine wamekuwa wakifanyiana,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, Wikienda lilimsaka Harmonize ili kujua kama kweli mama yake alimkubali Wolper au alionesha shaka naye kama chanzo chetu kilivyotonya. Msanii huyo aliliambia gazeti hili kuwa kwa namna moja au nyingine mama yake alimpokea mpenzi wake huyo kwa moyo mkunjufu japokuwa aliwahusia kuheshimiana na kuvumiliana kwa kila jambo.

“Mama alimpokea vizuri sana kiasi kwamba hata mimi nilibaki nikishangaa kwani alimpenda na hata kufikia hatua ya kututaka tuendelee kuheshimiana kwa kila hali kwani njia pekee ya kufika mbali ni kuheshimiana na kuvumiliana kwa kila jambo japokuwa kwenye maisha ya kila siku kukwaruzana hakuepukiki,” alisema Harmonize.

Kwa upande wake Wolper aliliambia gazeti hili kuwa kwenye maisha hakuna raha kama kuishi kawaida kwa sababu ukawaida ndiyo ulimfanya kukubalika kwa mama Harmonize.

“Hayo ni maneno ya watu lakini alifurahia sana staili yangu ya kuishi kawaida maana kama ningekuwa na tabia ya kujiona staa basi watu wasingeweza kunizoea na kunikubali kama ilivyokuwa kwa mama mkwe,” alisema Wolper.

Wolper na Harmonize walianza uhusiano wa kimapenzi hivi karibuni huku wengi wakidhani kuwa ni ‘kiki’ kabla ya mambo kukolea na sasa uhusiano wao umegeuka habari ya mjini.

Picha: Naibu Spika, wabunge wakicheza mziki kwenye show ya Lady Jaydee Dodoma

Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, wikiendi iliyomalizika aliunga wabunge wengine pamoja wapenzi wa muziki kwenye show ya Lady Jaydee ya Naamka Tena Tour mjini Dodoma.

Show hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Royal Village huku pia Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akihudhuria.






 Mbunge wa Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji akizungumza na Alvaro Rodriguez

Kwenye show hiyo Lady Jaydee alitumbuiza pamoja na bendi yake.





 Lady Jaydee akiwa kazini







Msanii Diamond Platnumz atoa msaada kwa wanafunzi 1800 jijini Dar es salaam

e

Msanii Diamond Platnumz akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Msanii Diamond Platnumz na uongozi wake siku ya Ijumaa kwenye kipindi cha Friday Night Live alitoa ahadi kuwa Jumatatu watapeleka zawadia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa ajili ya watanzania.

Na leo hii msanii huyo ametimiza ahadi hiyo kwa kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa madawati 600 ya wanafunzi ambayo yatasaidia takribani ya wanafunzi 1800 katika jiji la Dar es Salaam ambao walikuwa wanakaa chini.

"Mapema leo na familia nzima ya WCB wasafi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda tulivyoenda kumkabidhi Madawati 600 kwajili ya Wanafunzi wa shule za Dar es Salaam. Madawati hayo ambayo yataweza kusaidia Wanafunzi elfu moja na mia nane kutoka kwenye kukaa chini na kuweza kukaa kwenye dawati na kupata elimu Vyema" alisema Diamond Platnum



MAGAZETI YA TANZANIA YALICHOANDIKA LEO TAREHE 6/6/2016 KWENYE HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA UDAKU NA MICHEZO.
















 

Gallery

Popular Posts

About Us