KINGAZI BLOG: 06/11/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, June 11, 2016

Mauaji ya Anathe Msuya… Hawara wa House Girl Atiwa Mbaroni



Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watu wengine wawili, akiwamo mpenzi wa mfanyakazi wa ndani wa Anathe Msuya, aliyeuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake.

Anathe, ambaye ni dada wa Bilionea Erasto Msuya, aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana Mei 26 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Wauaji hao hawakuchukua chochote kwenye nyumba hiyo. Bilionea Msuya aliuawa Agosti mwaka jana kwa kupigwa risasi na tayari watu 12 wamekatwa, wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Kamanda wa Kanda hiyo, Simon Sirro alisema hadi sasa wamekamata watuhumiwa wanne wakihusishwa na mauaji ya dada wa bilionea huyo.

Kati ya watuhumiwa waliokamatwa, yumo mume wa Aneth, msaidizi wa ndani wa Anathe na mtuhumiwa mwingine ambaye Kamanda Sirro hakumtaja jina.

“Mwanzo tulimkamata mume wa marehemu na msaidizi wa ndani wa marehemu, lakini sasa wameongezeka wengine wawili, akiwamo hawara wa msaidizi wa ndani. Tunaendelea kuwahoji na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani,” alisema Sirro.

Kwa mujibu wa mama mdogo wa marehemu, Lilian Benjamin, msaidizi wa ndani wa dada wa bilionea huyo aliondoka saa sita mchana na kuacha funguo nyumba ya jirani.

Lilian alisema msaidizi huyo alimpigia simu ghafla bosi wake mchana na kumwambia anaondoka na hataendelea na kazi.

Mauaji ya Aneth ni mwendelezo wa mauaji yanayoikumba familia hiyo ya Msuya baada ya kaka yake, Erasto ambaye alikuwa ni mfanyabiashara tajiri wa madini, kuuawa Agosti 7, 2013 kwa kupigwa risasi zaidi ya 12 kwa kutumia bunduki ya SMG katika eneo la Mijohoroni wilayani Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.

Februari 10, mawakili wanaosimamia kesi ya Erasto, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emanuel Safari na John Lundu, waliiambia mahakama kuwa Serikali inakusudia kuita mashahidi 50 kuthibitisha shtaka hilo na kuwasilisha vielelezo 40, ikiwamo bunduki hiyo.

Mawakili hao walidai mipango ya kumuua bilionea Msuya ilianza Julai 26,2013 jijini Arusha, ikiwahusisha washtakiwa na waliotekeleza mauaji hayo wangelipwa Sh5 milioni kila mmoja.

Wakitoa maelezo ya tukio hilo, mawakili hao waliiambia mahakama kuwa washiriki ambao wasingeenda moja kwa moja kwenye mauaji, wao wangelipwa Sh3 milioni kila mmoja.

Mshtakiwa wa kwanza, Shariff Mohamed anadaiwa kuwa ndiye alikuwa mpangaji mkuu na alitoa fedha za maandalizi yote ya mauaji.

Washtakiwa wengine ni Shaibu Jumanne, ambaye anafahamika kwa jina la utani la Mredii, Mussa Mangu, Jalila Zuberi (Said), Karim Kihundwa, Sadick Jabir (Msudani) na Ally Mussa (Mjeshi).

Ajali Mbaya Yaua 6 na Kujeruhi 8, Same papo hapo kilimanjaro


Hiace ya abiria ikiwa nyang’anyang’a.
Hali halisi ya ajali hiyo.
Mashuhuda wa tukio hilo, wakitaharuki.
Ajali ilivyotokea
Majeruhi wa ajali hiyo, Musa Chikira (35), akiwa amelazwa katika wodi ya wanaume, hospital ya Wilaya ya Same.
Majerhi wa ajali hiyo, Noel Bakari Kanumba (36), alikuwa anatokea Same Mjini akienda Kavambughu.
Majeruhi wa ajali hiyo, Musa Chikira (35), akiwa amelazwa katika wodi ya wanaume, hospital ya Wilaya ya Same.

Same, Kilimanjaro;

WATU sita wamefariki dunia na wengine nane wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi dogo la abiria aina yaHiace lililokuwa likitokea Mjini Same kuelekea Njoro wilayani Same, ambapo liligongana na gari ya mizigo aina yaFuso muda mfupi baada ya kuondoka katika kituo cha abiria cha Same Mjini.

Daktari aliyezungumza na chanzo cha habari hii katika Hospital ya Wilaya ya Same, Dkt Mlay, amesema wamepokea maiti sita ambazo amebainisha kuwa wanaume ni watano na mwanamke ni mmoja.

Aidha, ameongeza kuwa Majeruhi nane walipatikana kufuatia ajali hiyo, ambapo katika Majeruhi hao nane wanawake ni wawili na wanaume sita na kati yao waliopewa rufaa kuelekea Hospitali ya KCMC -Moshi ni watatu, wanaume wawili na mwanamke mmoja.

Majeruhi Noel Bakari Kanumba, aliyekuwa anatokea Mjini Same kwenda Kavambughu, akizungumza na Mwandishi  katika wodi ya Wanaume katika Hospitali ya Same, amesema alikuwa amekaa kwenye kiiti cha mbele na dereva ambapo aligundua kuwa dereva yule alikuwa amelewa akamwonya asikimbize gari lakini hakutaka kumwelewa, ndipo gari lilimshinda na kuhama upande wake na kuelekea upande wa pili na kugonga Fuso upande wa dereva la Fuso hali iliyosababisha ajali ambapo dereva na abiria wake waliokuwa wamekaa kiti cha mbele walifariki dunia papo hapo.

Majeruhi wengine ni Musa Chikira (35), alikuwa anatokea Mjini Same kwenda Njoro na Mariam Omary Mbaga aliyekuwa katika wodi ya wanawake.

Chanzo: JF

Wabunge wa Kambi ya Upinzani Wajitoa Kamati ya Bunge ya Ukimwi Baada ya IKULU Kuwanyiima Kibali cha Kwenda Marekani


Ofisi ya Rais Ikulu imewanyima vibali vya kusafiri kwenda Marekani wabunge wawili wa Kambi ya Upinzani, bungeni na kumruhusu mbunge wa Geita Mjini (CCM), John Kanyasu.

Wabunge hao wa kambi ya upinzani waliochaguliwa kwenda Marekani ni Savelina Mwijage (CUF) na  Mwita Mwaikabwe (Chadema)

Wabunge hao watatu ni wajumbe wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi, lakini baada ya kunyimwa vibali hivyo wamejitoa kwenye kamati hiyo wakipinga kitendo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma, mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Mwikwabe alisema walipata barua ya kuteuliwa kushiriki safari hiyo kutoka Ofisi ya Bunge Mei 24.

“Tunapenda kukufahamisha kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amekuteua kushiriki mkutano wa ngazi ya juu ya maamuzi kuhusu Ukimwi duniani utakaofanyika 08-10 New York, Marekani,” alinukuu barua hiyo iliyosainiwa na Patson Sobha kwa niaba ya Katibu wa Bunge.

Katika barua hiyo wametajwa wabunge wengine kwenye safari hiyo kuwa ni mbunge wa viti maalum (CUF), Savelina Mwijage.

“Nikiwa Tarime nilipata simu kutoka kwa Patson kwamba, Naibu Spika alipokea simu kutoka Ikulu kuwa imezuia vibali vyetu vya kwenda Marekani na badala yake Kanyasu ameteuliwa,” alisema Mwikabe.

“Tunashangaa, kuteuliwa tuliambiwa kwa barua, lakini kukataliwa tuliambiwa kwa simu,” alisema Mwita.

Alisema kutokana na kutopewa kibali, wajumbe wote wa kambi hiyo wamejitoa kwenye Kamati ya Bunge ya Ukimwi.

“Hayo yote yanafanyika kwa sababu Naibu Spika hatupendi kabisa wabunge wa upinzani ndiyo maana wametufanyia haya,” alisema.

Kwa upande wake, mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaambia katika mkutano wa wabunge wote kuwa hawahusiki katika uombaji wa vibali kutoka Ikulu.

“Mimi mwenyewe nimeshawahi kusafiri zaidi ya mara tatu mbona sijawahi kuomba kibali kutoka Ikulu?” alihoji Mbatia.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alihoji kama wabunge hao ndiyo wenye haki ya kusafiri. Pia alihoji haraka waliyonayo wabunge hao wakati walishapeleka malalamiko yao kwa maandishi dhidi ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

“Kwani wanaharaka gani wao? Si walishapeleka malalamiko hayo na yapo kwenye kamati. Wasubiri uamuzi ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge),” alisema.

 

Gallery

Popular Posts

About Us