KINGAZI BLOG: 04/06/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, April 06, 2016

Hii Ndiyo Mipango ya Diamond kwa Mwaka Huu



numz akitangaza kolabo na wasanii wa kutoka Marekani lakini hakuna hata moja tuliyoona hata cover yake,mwaka jana rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alimuunganisha Diamond na meneja wa Trey Song na ikasema kuwa kuna kolabo itafuta hiyo ni mbali na

Mbunge anusurika Kifo kufuatia shambulio la Al Shabaab


Polisi nchini Somalia imesema Mbunge mmoja amenusurika kifo karibu na soko la Mogadishu wakati watu wasiojulikana walipolimiminia risasi gari lake katika shambulizi lililowauwa walinzi wake wawili.
Al-Shabaab Kämpfer in Mogadishu
Baadhi ya wanamgambo wa Al Shabaab

DRAKE FT WIZKID & KYLA - ONE DANCE(AUDIO)


Shein atangaza kutumbua majipu Zanzibar.

Watumishi hewa 4,317 wafutwa Serikali Kuu




AGIZO la Rais John Magufuli la kuwataka viongozi sehemu za kazi kuondoa watumishi hewa, limesaidia watumishi hewa

Afungwa Kifungo cha Maisha Jela Kwa Kumlawiti Mtoto Mlemavu wa kusikia na kuongea.



Mkazi wa Gongo la Mboto, Omary Hamis (25) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya

Hatimaye Utumishi Wafafanua Kuhusu Mshahara wa Rais Magufuli na Kikwete



Siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli, kutaja mshahara wake kuwa ni Sh. milioni 9.5 kwa mwezi, Wizara ya Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imefafanua mshahara aliokuwa anapokea Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, kuwa unalingana na wa kiongozi huyo.


Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro jana  alisema Kikwete aliondoka madarakani akiwa anapokea Sh. milioni 9.5, ikiwa ni kiwango sawa na cha Rais Magufuli.


“Hadi Kikwete anaondoka madarakani, mshahara wake kwa mwezi ulikuwa Sh. milioni 9.5, siyo kweli kuwa alikuwa akipokea Sh. milioni 34 kama ilivyowahi kuelezwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari,” alisema.


Mwishoni mwa wiki akiwa kwenye mapumziko nyumbani kwake Wilaya ya Chato mkoani Geita, Rais Magufuli alitaja mshahara wake, huku akiahidi kuweka hadharani stakabadhi za mshahara (salary slip) atakaporudi Dar es Salaam.


Rais alilazimika kufanya hivyo kufuatia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), kumpa changamoto ya kutaja mshahara wake, baada ya kueleza nia ya serikali yake kupunguza mishahara ya watumishi wa mashirika na taasisi zake kutoka Sh. milioni 40 hadi milioni 15.


Iwapo Rais mstaafu Kikwete, alikuwa analipwa kiasi hicho, kwa mujibu wa sheria, kwa sasa analipwa asilimia 80 ya mshahara huo ambayo ni Sh. milioni 7.6 ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani.


Hivi karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vilinukuu taarifa iliyotolewa Julai, mwaka jana na mtandao wa Africa Review ulioandika kuwa Rais Kikwete wakati akiwa madarakani alikuwa akishika nafasi ya tano miongoni mwa marais 38 wa Afrika kwa kulipwa mshahara mnono wa Dola 16,000 za Marekani (sawa na Sh. milioni 34 wakati huo).


Taarifa hizo zilikanushwa vikali na Ikulu, lakini hakukuwa na ufafanuzi wa mshahara halisi anaopokea Rais kwa wakati huo.


Kwa mujibu wa Katiba ibara ya 43 (1), Rais atalipwa mshahara na malipo mengineyo na atakapostaafu, atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo, posho, kadiri itakavyoamuliwa na Bunge na mshahara, malipo hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho, vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya serikali na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara hiyo.


Ibara ndogo ya pili inasema mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba.

Haya hapa Magazeti Ya Tanzania Yalichoandika leo Jumatano Ya,April 06,2016 Kwenye habariza kitaifa kimataifa udaku michezo na stori kali

April 6 2016naanza kwa nakuletea habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye ,habari za kitaifa,kimataifa Michezo na udaku na stori nyingine kali ili ujue kilichojiri duniani.. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook/tanzaniampya sasa blog,  pia kwenye twitter @tanzaniampysasa.

Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono afariki usingizini

 Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono Meghan Wren
Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono Amber Rayne amefariki nyumbani kwake mjini Los Angeles ,maafisa wamethibitisha.

Magufuli kuzuru Rwanda ziara ya kwanza nje tyaangu achaguliwe.

Magufuli

Hiyo itakuwa ziara ya kwanza ya Magufuli nje ya Tanzania tangu Oktoba
Rais wa Tanznia John Magufuli amepangiwa kufanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi hiyo tangu kuingia
 

Gallery

Popular Posts

About Us