KINGAZI BLOG: 07/11/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, July 11, 2016

INDIA NA TANZANIA ZAINGIA MKATABA WA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI.

 

Serikali ya India na Tanzania zimesaini mikataba ya miradi ya maendeleo katika sekta za maji, kilimo, viwanda, teknolojia ya habari na mawasiliano na afya katika kuimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili ili kusaidia wananchi wake. 


Mikataba hiyo imesainiwa jana, wakati Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi alipokuakifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Mikataba wa kwanza uliosainiwa inahusisha mradi wa kusambaza maji katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam. 


Aidha, mkataba wa pili unahusisha mradi wa kusambaza maji Zanzibar ambao unatarajiwa kugharimu dola za kimarekani milioni 92 ambapo mradi huo unatarajiwa kufikia miji 17 nchini na mkataba mwingine utahusisha mafunzo ya ufundi yatakayosaidia kuzalisha wataalamu mbalimbali. 


“Lengo letu ni kusaidiana na kuimarisha mahusianao yetu katika kukuza uchumi na kutengeneza fursa mpya za ajira kwa wananchi wetu” alisema Waziri Modi. 


Waziri Modi aliongeza kuwa Serikali ya India itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa biashara na hatimaye kukuza uchumi wa nchi hizo. 


Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alisema Serikali India imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania hasa katika masuala ya maendeleo ambapo imeweza kuwekeza nchini kiasi shilingi za Kimarekani dola bilioni 2.4 na kuzalisha ajira 54,176. 


Baadhi ya misaada iliyotolewa na Serikali ya India ni pamoja na mashine ya vipimo vya ugonjwa wa kansa katika hospitali ya Bugando, itakayosaidia wakazi wa kanda ya ziwa na nchi nzima kwa ujumla pamoja na kuongeza na kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika la viwanda vidogo vigodo la India kushirikiana na Tanzania katika kukuza viwanda vidogo na vya kati nchini. 


Katika masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano, Serikali hiyo imeahidi kuleta wataalamu wao nchini Tanzania kwa lengo la kutengeneza program mbalimbali ili kuisaidia Tanzania katika masuala ya ulinzi wa mitandao pamoja na kutengeneza namna bora za ukusanyaji wa mapato ya nchi. 


Katika masuala ya viwanda, Serikali ya India imeahidi kuanzisha viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu zitakazotibu magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria, figo na kisukari, ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa tiba vitakavyotumika katika hospitali mbalimbali nchini kwa lengo la kupunguza gharama ya kununua vifaa hivyo nje ya nchi. 


Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa nchi ya India ina uhitaji mkubwa wa mazao ya kilimo hasa jamii ya kunde hivyo akawataka wakulima kutumia fursa hiyo kuzalisha mazao hayo kwa wingi. 


“India inauhitaji wa tani 200 za mazao jamii ya kunde, wakulima mnatakiwa kuzalisha mazao hayo kwa wingi kwa vile tayari kuna soko la uhakika, na tutahakikisha madalali hawatakuwepo ili mkulima asikandamizwe” alisema Rais Magufuli. 


Katika sekta ya uwekezaji nchini, India ni nchi ya tatu kwa uwekezaji Tanzania ikifuatiwa na Uingereza pamoja na China

KIONGOZI WA ISIS AKIRI KWAMBA WANAFADHILIWA NA UTAWALA WA OBAMA

Kiongozi wa ISIS kwa jina Yousef al-Salafi kutoka Pakistan amekubali kwamba kundi lao la ISIS linafadhiliwa na Marekani, kutoka utawala wa Obama. Habari hii ilikuja kutoka serikali ya Pakistani mara baada ya kuhojiana na Yousef na kupokea taarifa hii.
Chanzo kilichofanya uchunguzi wa siri kilisema:
Wakati wa uchunguzi,Yousaf al Salafi alibainika kuwa alikuwa akipata fedha kutoka Marekani- kuendesha hiki kikundi nchini Pakistan na kuwaajiri vijana wengi kwenda kupigana nchini Syria.
Chanzo kimoja kinasema kuwa Yousaf al Salafi amekiri mwenyewe kuwa mshirika-akisema yeye ni imam-alikuwa akilipwa na Marekani kuwaajiri vijana wengi hili kujiunga na ISIS kwa kuwapa $600.
Chanzo hiki pia kimesema:
Marekani imekuwa ikilaani shughuli za IS lakini kwa bahati mbaya imeshindwa kujizuia kuwafadhili.Marekani inawatumia IS kwa maslahi yake binafsi na imejaribu kukishambulia kikundi hiki kilichopo Iraq ila imeshindwa kabisa kuzuia maasi yanayofanywa na kikundi hiki nchini Syria.
Utawala wa Obama kuwafadhili ISIS, sio kitu cha kushangaza, Hebu tujikumbushe kwamba utawala wa Obama umekataa kuiunga mkono Misri katika uharibifu uliofanywa na ISIS, hata hivyo inafanya kazi na Uturuki ambao ni moja ya waunga mkono wakubwa wa ISIS.Pia tusisahau ya kuwa Marekani inawasaidia FSA na inaendelea kuvifadhili vikundi vya jihad ili kupigana na serikali ya Assad, mapigano yanayowahusisha waislamu tu, na hatimaye hili Uturuki iweze kutawala Mashariki ya Kati.
Kweli duniani kwa sasa inatawaliwa na shetani, na wengi kati ya watu wenye nguvu duniani wanaingiliwa na mapepo,wanavyofanya vitu kwa upande wao wanajiona wapo sahihi, na kwa kiasi kikubwa wanakubaliana na maovu yote yanayoiandma dunia.
Kuanzia madawa ya kulevya, magaidi, mauaji ya watoto wasio na hatia, hadi agenda ya mashoga, uovu tunaouona kwa sasa machoni petu unawezeshwa zaidi na watu waovu waliopewa nguvu na umma, wakijifanya wema wamevaa suti na wana tabasamu zuri.
Watu wengi wanafikiria ugaidi ni uovu pekee mbaya, ila ukweli ni kwamba watu wengi wenye ushetani ndani yao wanafanya matukio mabaya sana nyuma ya pazia, wakielekeza kwa siri, na wana nguvu maana wapo madarakani.
Hebu tukumbuke kwamba George Bush ambaye alimtoa Saddam madarakani, aliyekuwa anawakandamiza jihad na kuwalinda wakristo, kitu ambacho Bush alifanya ni kutengeneza mazingira kwa ISIS kuvamia mashariki ya kati na kusababisha matatizo makubwa na machafuko yaliyogharimu maisha mengi ya wasio na hatia.
Ukweli unabaki kwamba Marekani inasaidia mateso yote wanayopata Wakristo katika Mashariki ya Kati, na lengo lake kubwa ni kuwatumia wanajihadi: kuharibu ukristo wote mashariki ya kati.
Huyu kamanda wa ISIS ambaye yupo nchini Pakistan, ambapo anafanya kazi kuunda sharia state katika nchi ya Pakistan,ambayo utaleta uharibifu mkubwa wa ukristo nchini humo.
Inatupasa wote wenye mapenzi ya dhati na utu wa binadamu kutoa sauti zetu juu ya vitendo viovu wanavyofanyiwa watu wasio na hatia yeyote duniani. Kuna idadi kubwa ya watu wanauliwa na wanateswa kijinsia na wengine wanauzwa kwa ajili ya maslahi ya wale waovu.

VIDEO :MASANJA MKANDAMIZAJI AMVISHA PETE MCHUMBA WAKE

Miongoni mwa vitu vinavyozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na picha zinazomuonyesha Masanja Mkandamizaji akimvisha pete msichana anaedaiwa kuwa mchumba wake,kwenye picha hizo Masanja na mchumba wake huyo wanaonekana 

ALICHOANDIKA MAMA YAKE DIAMOND PLATINUMZ KUHUSU WEMA SEPETU


Mtu wangu wa nguvu najua mitandao ya kijamii ina nguvu sana siku hizi, jumapili ya July 10 2016 mama mzazi wa msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz amempost Wema Sepetu ambaye alikuwa ni girlfriend wa zamani wa Diamond Platnumz.

Picha aliyopost mama Diamond
kendrah_michaelUzalendo kwanza..umependeza sanaa mamy akee
Najua ni kipindi kirefu kimepita toka toka Diamond Platnumz na Wema waachane, tokaDiamond na Wema waachane ni kipindi kirefu kimepita na watanzania hawakuona upande wa Diamond wakimzungumzia Wema, lakini sasa hivi imekuwa sio ishu tena kwaWema kumpost mama Diamond na yeye kupostiwa na mama Diamond.

Picha aliyopost Romy Jons
Baada ya mama Diamond kupost alifuatia Romy Jons ambaye ni kaka yake naDiamond Platnumz, hiyo inaonesha kuwa upande wa Diamond Platnumz na Wema Sepetu hakuna tatizo kama ambavyo baadhi ya watu walikuwa wanaweza kuhisi.

TAZAMA PICHA ZA GAUNI LA MAMA DIAMOND PLATNUMZ UTADHANI NI MDADA




Hatimaye!! Ureno yatwaa ubingwa wa Ulaya, Euro 2016


 Timu ya taifa ya Ureno imetwaa ubingwa michuano ya Ulaya, Euro 2016, kwa kuwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika dakika za ziada kwenye mchezo wa fainali mjini Paris.

Goli la ushindi lilifungwa na Eder katika dakika ya 110, na kupeleka kilio na huzuni kwa mashabiki wa Ufaransa waliofurika kwenye uwanja wa Stade de France.


Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Ureno. Hii ni mara ya kwanza Ureno kushinda michuano mikubwa.
Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano bila ya mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo aliyetoka kutokana na kupata jeraha la goti katika kipindi cha kwanza.

Ufaransa ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini hawakuweza kuzitumia vyema nafasi walizopata.

RC PAUL MAKONDA AANDIKA HII KUHUSU ZARI THE BOSS LADY




MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 11KWENYE HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA NA MICHEZO



 

GIGY MONEY aamua kuachia picha hizi za nusu utupu mtandaoni hebu jionee




Bella, Wema, Idris Walivyofunika Katika Black Tie









































Usiku wa kuamkia leo, staa wa Bongo Muvi, Wema Abraham Sepetu pamoja na mwandani wake, Idris Sultan waliiongoza shoo ya Black Tie iliyokuwa maalum kwa King Of The Best Melodies, Christian Bella iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa King Solomoni, Kinondoni jijini Dar.

Katika shoo iliyohudhuriwa na mashabiki kibao, Bella alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 10 tangu aingie kwenye muziki nchini ambapo aliungwa mkono na mashabiki na mastaa kibao wa muziki wa Dansi, Bongo Fleva pamoja na Bongo Muvi wakiongozwa na Irene Uwoya, JB, Steve Nyerere, Shilole, Jacqueline Wolper, Linah, Barnaba, Faiza Ally, Odama na wengine kibao.

Shoo hiyo iliyoandaliwa na rafiki wa karibu na Wema aitwaye Muna (Muna Logistic), ilianza mida ya saa nne za usiku kwa burudani kutoka kwa msanii Nandy na baada ya hapo alifuatiwa Linex kisha Linah na kumalizia kwa Barnaba ambaye aliwakumbusha mashabiki Wimbo wa Barua aliouimba zamani na Linah.

Ulipofika muda wa saa nane kasoro, Bella aliingia jukwaani na kufunika ambapo alipiga nyimbo zake zote kali kuanzia yapo wapi mapenzi, Nagharamia na nyingine kibao.

Baada ya Bella kufanya shoo ya kwanza, alimpisha Wema na Idris ambao kwa mara ya kwanza walipanda na kutambulisha waandaaji wa shoo hiyo.

“Tunawapongeza Muna Logistic lakini pia nimpongeze Bella kwani ndiye msanii pekee aliyeweza kutamba kwa muda mrefu bila kuchuja.

“Bella ameaandaliwa CD, DVD za muziki wake tangu alipoanza na kufikisha hiyo miaka 10,” alisema Wema Sepetu akiitikiwa na Idris.

Kilichofuta baada ya hapo, Walifungua shampeni spesho (za makaratasi ya kung’ara) ambazo zilipendezesha ukumbi wote na kulipukwa kwa furaha.

Baada ya kushuka kwa Wema na Idris, MC mwingine aliyekuwa akiongoza shoo hiyo, Gardner G. Habash aliruhusu shoo kuendelea kwa Bella ambapo kivutio kikubwa kilikuwa pale alipopanda na kuanza kuimba Wimbo wa Nani Kama Mama huku akitaja jina la msanii mmojammoja ambaye ameguswa na wimbo huo kuja kutoa chochote na baada ya hapo kilichofuatiwa ni mvua ya hela kutoka kwa mastaa kibao wakiongozwa na Alawi Junior.

Mbali na shoo hiyo, kivutio kingine kilikuwa ‘red carpet’ ambayo ilikuwa kitofauti na iliyoongozwa na baadhi ya mastaa wakiwemo Miss Tanzania, Lilian Kamazima.

Imeandaliwa na Andrew Carlos na Musa Mateja/GPL

 

Gallery

Popular Posts

About Us