KINGAZI BLOG: 07/06/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, July 06, 2016

EXCLUSIVE: Wema Sepetu kaongea kuhusu Diamond kumpost Instagram jana

July 5, 2016 mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz aliingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kupost kwenye Instagram kuhusu watu kujitokeza kwa wingi kwenye show ambayo imeandaliwa na mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu pamoja na Christian Bella na Idris.
AyoTV ilimpata Wema na ameyasema haya >>>Watu wamekuwa wakiitumia hii beef yetu kujipatia followers hasa kwenye mitandao yao kwasababu mtu anaweza akatokea sehemu yoyote na kuanza kunitukana mimi au kumtukana Naseeb akajipatia followers wa kutosha, kuna muda mimi nilikuwa naogopa kuimba wimbo wa Diamond unapopigwa naogopa hata kucheza’
Nikisikia nyimbo za Naseeb siwezi kuimba inanibidi nikaze lakini mwisho wa siku najikomoa mimi mwenyewe nikikaa kwenye gari nitaimba kama utakuwa unakumbuka nilivyoimba mara ya kwanza watu wakashangaa wakawa wanajiuliza maswali mengi sana, kwasasa hatuko kwenye mapenzi lakini tunasaidiana kazi kuonesha uzalendo’


MILLARD AYO

Mtandao unaowaunganisha wapenzi wa Kiislamu wadukuliwa((HACKED)


Image copyrightBBC
Image captionMtandao wa kuwaunganisha Waislamu wanaopendana
Maelezo ya kibinafsi ya takriban wanachama 150,000 wa mtandao unaowaunganisha wapenzi wa Kiislamu umewekwa wazi mtandaoni.
Zaidi ya ujumbe 700,000 za kibinafsi kati ya wanachama zimefichuliwa.
Ujumbe katika mtandao huo ulisema: ''Tumejulishwa kuhusu udukuzi na tunaurekebisha mtandao wetu kwa lengo la kuimarisha usalama wake''.
Ujumbe uliofichuliwa ulihusisha habari za siri kama vile iwapo mwanachama angependa kuwa na wake wengi.
Udukuzi huo ulibainiwa na mtafiti wa maswala ya kiusalama Troy Hunt ambaye anamiliki mtandao wa maswala ya usalama wa mitandaoni.
Image copyrightBBC
Image captionMtandao wa Waislamu
Maelezo kuhusu waajiri wa wanachama,akaunti zao za Skype na anwani zao za kuingia mtandao kulingana na mtandao wa teknolojia Motherboar.
Ukurusa wa kuwaunganisha waislamu wapendanao katika facebook ulielezea mtandao huo kuwa :Wasio katika ndoa,waliotalakiana,walio katika ndoa,''Ujumbe mmoja uliofichuliwa ulisema: Nataka kukuoa-iwapo unakubali nikutumie picha na maelezo yangu''.

MAAAJABU!!!!!!Mwanamke kujifungua 'mjukuu wake'


Mwanamke ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi mahakanani na kuruhusiwa kufanya hivyo.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 60 alikuwa amekatazwa kupeleka mayai ya bintiye kwenye kliniki moja nchini Marekani hali iliyosababisha akate rufaa.
Bintiye ambaye aliaga dunia mwaka 2011, anaripotiwa kumuambia mamake amzalie watoto wake. Lakini mamake alishindwa katika kesi mwaka uliopita.
Hata hiyo aliruhusiwa kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufaa mjini London mbele ya jopo la majaji watatu.
Mwaka 2014 halmashauri inayohusika na mayai ya uzazi, ilisema kuwa mayai hayo hayangetolewa mjini London, kwa sababu bintiye hakuwa ametoa idhini kamili kabla ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 28.
Lakini kwenye kesi ya sasa mawakili waliawaambia majaji kuwa, mwanamke huyo alikuwa anataka kutimiza matakwa ya bintiye ya kuzaa mtoto akitumia mayai yake na kisha amlee mtoto huyo.

Lionel Messi ahukumiwa kufungwa jela


Image copyrightGETTY
Mchezaji nyota wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kupatikana na makosa ya kutumia ulaghai wakati wa ulipaji ushuru, vyombo vya habari nchini Uhispania vinaripoti.
Babake, Jorge Messi, pia amehukumiwa kufungwa jela kwa kuilaghai Uhispania €4.1m (£3.2m; $4.6m) kati ya 2007 na 2009.
Wakati wa kesi, waendesha mashtaka walisema maeneo salama yenye kinga dhidi ya ushuru Belize na Uruguay yaliyumiwa kuficha mapato kutokana na uuzaji wa haki za picha za mchezaji huyo.
Lakini Messi amesema hakufahamu lolote kuhusu masuala yake ya kifedha.
Wawili hao hata hivyo hawatarajiwi kufungwa jela.
Chini ya mfumo wa haki nchini Uhispania, mtu anaweza kutumikia kifungo chochote kilicho chini ya miaka miwili nje ya gereza.
Messi na babake pia wanaweza kukata rufaa katika Mahakama ya Juu nchini humo.

BBC SOURCE

Diamond akiri kumkubali Wema Sepetu

MKALI wa Bongo hivi sasa ,na Rais wa label ya WBC Diamond Platnumz mapema hivi leo ameonyesha kuzika rasmi tofauti zake na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu,ambapo katika tukio lisilo la kawaida Daimond amepost ujumbe wa kushow Support tukio linalofanywa na Mlimbwende huyo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006.

Kufuatia tukio hilo mashabiki wa Staa huyo nguli Afrika Mashariki kwa sasa wamempongeza Baba Tiffa kwa kitendo hiko ikizingatiwa kuwa wawili hao walikuwa katika kile kilichozungumziwa kuwa ni 'mgomo baridi wa kampani'.
Hata hivyo hii ni kama Diamond anajaribu kulipa fadhila kwa Wema ,kwani kipindi ambacho Diamond alikuwa akiwania tuzo za BET ,Wema alionyesha kumuunga mkono Staa huyo pamoja na kwamba hakuweza kufanya vizuri katika tuzo hizo

MAGAZETI YA LEO JUMATANO 06/07/2016 KWENYE HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO NA UDAKU.

Eid Mubarak!!karibu tunakuletea uchambuzi wa magazeti ya Leo kwenye habari za kitaifa kimataifa na michezo,usisahau kutufollow kupitia twitter na face book @kingazi blog
















 

Gallery

Popular Posts

About Us