Gabo Zigamba ndiyo mrithi wa Kanumba? | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, April 23, 2016

Gabo Zigamba ndiyo mrithi wa Kanumba?


Inawezekana si mara yako ya kwanza kusikia jina hili la Gabo Zigamba katika tasnia ya filamu nchini, wazazi wake walimpa jina la Salim Ahmed.
Msanii Gabo Zigamba
Muigizaji huyu kadili siku zinavyozidi kwenda anazidi kupenya masikioni mwa watu wengi na kuzidi kuonyesha uwezo wake katika uigizaji kiasi cha baadhi ya mashabiki kudai kuwa huyu ndiye mrithi wa Steven Kanumba katika tasnia hiyo kutokana
na uwezo wake katika kazi hiyo.
Wiki iliyopita tuliweka swali katika ukurasa wa Facebook wa East Africa Radio tukiwauliza mashabiki, kwa sasa Tanzania ni msanii gani wa filamu ambaye anafanya vizuri na sifa nyingi zilitolewa kwa Gabo Zigambwa huku wengine wakisema kwa sasa wamerudisha mapenzi yao kutazama kazi za filamu za nyumbani kutokana na uwezo wa msanii huyo kwani wanadai baada ya kifo cha Kanumba Bongo movie ni kama ilipoteza mwelekeo.
Sifa nyingi zilisema kuwa msanii huyo ana uwezo mkubwa sana katika kuuva uhalisia katika kazi zake huku wengine wakidai pia anaweza kufaa kila sehemu na akaitendea haki, lakini pia ilinibidi nifanye utafiti katika mabanda ambayo yanakodishwa na kuuzwa kwa Cd za kibongo bado watu hao waliniambia kuwa kazi ambazo msanii huyo yupo huwa zinauzika na kukodishwa sana jambo ambalo linaonyesha kuwa anakubalika sana na wapenzi wa filamu za kibongo.
Watu ambalimbali waliweza kumuelezea kwa namna tofauti tofauti kama ambavyo wewe mwenyewe unaweza kushuhudia hapa.
'Mimi kiukweli Gabo ndiyo anakonga moyo wangu napo muona yupo anacheza filamu nafurahi na barikiwa na yeye". Cemola Emmanuel
"Gabo yuko vizuri, Ray sioni uhalisia kwenye movie zake na ananichefua zaidi anapokariri neno la nitakutumbua na pumbavu! Kila movie analitumia".- Yustina Masungwa
"Jamani watanzania tuache uongo kitu kikiwa kizuri tuseme, Gabo namba moja na Niva wa pili yani huyo Ray hata JB hamfikii kwa sasa Ray maneno yanajirudia tumechoka".- Mamu Raja
"Mr Gabo anaigiza kwa hisia zote tena anakaribia kuwa kama kanumba, mfano movie yake ile ambayo mke wake alikufa kisha akaenda na nesi kumzalisha ni shida". -Stella Yona
Katika zaidi ya Comment 2000 ambazo watu waliweza kuchangia mada ile watu wengi walikuwa wakimpa sifa za kutosha Gabo Zigamba na kuonyesha ni jinsi gani anakubalika na mashabiki kuliko hata majina ya watu wengine maarufu na wakongwe katika tasnia ambao kwa mujibu wa mashabiki wanadai kuwa uwezo wao hauwezi kufanana na uwezo wa msanii huyo jambo ambalo mashabiki wenyewe wanaonyesha kuwa huenda Gabo Zigamba kama ataendelea na moto huo huo na kuongeza jitihada na kutojisahau anaweza kuvaa viatu vya marehemu Steve Kanumba katika uigizaji.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us