Mbio za Mwenge Zazinduliwa rasmi Mkoani Morogoro | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, April 18, 2016

Mbio za Mwenge Zazinduliwa rasmi Mkoani Morogoro


MOROGORO


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo atawasha Mwenge wa Uhuru na kuzindua rasmi mbio zake ili kukimbizwa katika halmashauri za wilaya na Manispaa zipatazo 179 za mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Uzinduzi huo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambao utatanguliwa na shamrashamra za halaiki kutoka kwa vijana zaidi ya 1,000 na vikundi vya utamaduni kutoka wilaya za Morogoro na nje ya mkoa huo.MWENGEKatika uzinduzi huo, viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na vyama vya siasa wamealikwa kushiriki wakiwemo pia mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Miongoni mwa mawaziri ambao hadi jana walikuwa tayari wamewasili mkoani hapa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Sera, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mouldine Castico.

Mawaziri hao jana waliungana na Makamu wa Rais kutembelea mradi wa vijana wajasiriamali wa mafundi seremala eneo la Mtaa wa Betero, Kata ya Sabasaba, Manispaa ya Morogoro. Kaulimbiu za Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni “Vijana ni Nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na Kuwezeshwa.”

Baada ya kuwashwa leo, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kuhitimishwa wilayani Gairo ambako Aprili 25, mwaka huu utakabidhiwa mpakani mwa wilaya hiyo na Kilindi ya Mkoa wa Tanga ili kuendelea na mbio zake.

Kwa mujibu wa ratiba ya mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu, utakimbizwa katika Halmashauri na Manispaa zipatazo 179 na kilele cha mbio hizo ni Oktoba 14, mwaka huu katika Mkoa wa Simiyu

.DOWNLOAD APP YETU YA TANZANIAMPYASASA HAPA

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us