Msanii TUNDA MAN apata AJALI mbaya ya gari Mkoani Iringa.Habari za Kifo na Majeruhi soma Hapa. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, April 17, 2016

Msanii TUNDA MAN apata AJALI mbaya ya gari Mkoani Iringa.Habari za Kifo na Majeruhi soma Hapa.


Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakua umekutana na taarifa inayomhusisha Tunda Man kupata ajali  akiwa Mkoani iringa Asubuhi ya April 17 chanzo cha habari kimempata Tunda Man mwenyewe na amekubali kutuelezea.


Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema
‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki‘

Tunda Man anamalizia kwa kusema
‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.

chanzo;Millard ayo.com

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us