Wema ambwaga Idris sultan | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, April 14, 2016

Wema ambwaga Idris sultan


Habari ya mtoto mzuri Wema Sepetu ‘Madam’ kumwagana na mpenzi wake, Idris Sultan si ngeni masikioni mwa wapenda ubuyu, imetapakaa kwenye mitandao ya kijamii lakini chanzo chetu imenasa sababu kubwa inayodaiwa kusababisha penzi hilo kuvunjika, twende pamoja.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wawili hao waliripotiwa kumwagana rasmi ambapo haikubainika mara moja sababu.

Iliposambaa habari hiyo, mapaparazi wetu waliingia kazini kuchimba zaidi ubuyu huo ambapo walifanikiwa kuzungumza na mmoja wa marafiki wa Wema ambaye alieleza siri ya wawili hao kumwagana.
“Kilichomfanya Wema amwagane na Idris si kingine ni shilingi milioni 98. Unajua Madam anadaiwa fedha hizo ili alikomboe lile gari lake (Range Rover Evoque) linaloshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Sasa akamuomba Idris amlipie, jamaa akazingua. Hapo ndipo penye sababu kubwa iliyomfanya Wema amaindi hadi wakamwagana na Idris,” alisema shosti huyo wa Wema.
idriss sultanaIdris Sultan.
IDRIS ADAIWA KUFULIA
Akaendelea: “Nasikia Idris kwa sasa amefulia. Zile shilingi milioni 500 alizoshinda kwenye Shindano la Big Brother (Hotshot 2014) zote zimeyeyuka. Ameshindwa kumhudumia Madam, Wema ameona isiwe tabu, bora amuweke pembeni aangalie ustaarabu mwingine.”

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us