PAUL Makonda Azitaka Benki zimwambie Waliokuwa Wanapokea Mishahara Hewa | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, May 22, 2016

PAUL Makonda Azitaka Benki zimwambie Waliokuwa Wanapokea Mishahara Hewa

Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda amezitaka benki nchini zishirikiane na serikali ili kubaini akaunti zilizokuwa zikiingiziwa mishahara hewa pamoja na kuwabaini wote waliohusika katika malipo hayo.

Makonda akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amezitaka bank 6 zikiwemo NBC, CRDB, NMB, CDB na zingine kutokana na swala la watumishi hewa waisaidie serikali ya mkoa wa Dar kufanya mambo matatu.

1) Kusimamisha matumizi ya akaunti za watumishi hewa mpaka pesa hizo zitakaporudishwa

2) Kuwataja watu wanaochukua pesa kupitia account hizo ambazo zimefunguliwa kwenye benki zao na watumishi wanaojulikana ni hewa ili polisi wachukue hatua pamoja na kufikishwa mahakamani.

3) Kama pesa hizo hazijachukuliwa maana yake ziko bank kwa sababu hiyo makonda amezitaka bank hizo kurejesha pesa za wananchi.

Makonda amezitaka benki hizo kukamilishwa mambo hayo ndani ya siku 21 na amezipatia benki hizo majina na namba zote za akaunti za watumishi waliyokuwa wananufaika na mfumo huo na amesema itasaidia pia kwa watumishi wa mabenki ambao siyo waaminifu.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us