Ben Pol Afunguka 'Muungano wa Diamond Platnumz na Rich Mavoko na WCB | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, June 14, 2016

Ben Pol Afunguka 'Muungano wa Diamond Platnumz na Rich Mavoko na WCB


Mkali wa wimbo ‘Moyo Mashine’, Ben Pol amefunguka na kuzungumzia hatua ya Diamond Platnumz kumsani msanii kubwa kama Rich Mavoko katika label yake WCB.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Ben Pol amesema hatua ya Diamond kuamua kumsaini Rich Mavoko katika label ya WCB, itafungua njia kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.

Ni vizuri sisi kwa sisi tukaaminiana na kufanya kolabo kwenye kazi,” alisema Ben Pol. “Diamond ni mpiganaji na Mavoko ni mtu ambaye ana kipaji na mjanja mjanja, kwa hiyo muungano wao unaweza kuleta mapinduzi makubwa katika muziki,”

Pia muimbaji huyo amewataka wale wasanii wenye uwezo wa kuwasaidia wenzao wasisite, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbele zaidi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us