Wezi wa Umeme Waendelea Kukamatwa | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, July 30, 2016

Wezi wa Umeme Waendelea Kukamatwa

Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Kinondoni limeendelea kuwakamata wananchi wanaotumia umeme wa wizi kujiunganishia umeme kinyume cha sheria pamoja na kuwekewa mita za Luku na Vishoka ambao siyo watumishi wa Shirika hilo.

Katika eneo la Mbezi jijini Dar es salaam, Mfanyabiashara wa Chakula Mariam Mjema amejikuta matatani baada ya kubainika kuwa mita ya Luku aliyowekewa ilikuwa ya wizi na haina kumbukumbu Tanesco, huku umeme aliowekewa ukipitishwa moja kwa moja kutoka katika nguzo ambapo ametumia umeme huo kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kulipia.

Akijitetea mbele ya mbele ya maafisa wa Tanesco na polisi waliofika eneo hilo,Mfanyabiashara huyo amedai kuwa vijana waliojitambulisha kuwa mafundi kutoka Tanesco walifika na kumfungia mita hiyo ya Luku na kuwalipa bila kupewa risiti.

Akizungumza baada ya kubaini wizi huo huo Afisa wa Tanesco mkoa wa kinondoni Injinia Marsel Antony amewatahadharisha wananchi kuwa macho dhidi ya Vishoka na huduma zote za mita za luku pamoja na kuunganishiwa Umeme zinapatikana katika ofisi za Tanesco na sio mitaani.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us