London: Wateja wala chakula wakiwa watupu mgahawani | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, August 17, 2016

London: Wateja wala chakula wakiwa watupu mgahawani

 Katika hali isiyokuwa ya kawaida mgahawa mmoja  jijini London Uingereza umechukua chati ya aina yake kwakuwa na huduma ya kipekee ambapo wateja wake hula  vyakula mbalimbali wakiwa utupu.

Mradi wa kujenga Mgahawa huo wa Bunyadi ulitangazwa na kampuni ya Lollipop Aprili 19 mwaka 2016 na kufunguliwa rasmi tarehe 11 Juni 2016 chini ya mwanzilishi wake Seb Lyall pamoja na timu yake.

Mgahawa huo wa Bunyadi upo kusini mwa mji wa London katika vitongoji vya Elephant na Castle ,una uwezo wa kupokea wateja takribani 42 kwa wakati mmoja na hadi sasa taarifa kutoka mji huo zinasema kuwa takribani watu 42,000 tayari wameweka oda ya kula katika mgahawa huo.

 “Naamini kuwa watu wanahaki ya kupata nafasi ya kufurahi bila vizuizi vyovyote kama rangi bandia, umeme, kemikali, simu za mkononi, na hata nguo kama wakitaka,wazo langu kuu ni ukombozi wa kweli” Alisema Lyall

Lyall pia anahusika na bar mbili za Owl Bar na Shoreditch’s Breaking Bad cocktail bar zenye utata mkubwa jijini London.Kampuni yake pia inajulikana kwa kuwa nyuma ya ugunduzi wa programu za simu kama Locappy na Hoot London ambazo ni maarufu sana katika jiji la London.




google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us