Serikali yatangaza Kiama kwa Majambazi | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, August 28, 2016

Serikali yatangaza Kiama kwa Majambazi

Serikali imesema imejipanga vilivyo kuhakikisha inawalinda raia na mali zao na kwamba watakao bainika kujihusisha ama kuunga mkono vitendo vya uhalifu ukiwemo ujambazi pamoja na kulibeza jeshi la polisi, watachukuliwa hatua kali.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na maafisa wa jeshi la polisi ,uhamiaji,magereza na vyombo vingine vya ulinzi na usalama usalama,katika mkutano uliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya polisi Moshi mkoani Kilimanjaro nakusema kuwa serikali haita fumbia macho uhalifu

Aidha Waziri Nchemba amelipongeza jeshi la polisi kwa kufanya kazi kwa weledi huku akilitaka lishirikiane na jamii kuzidisha juhudi za ulinzi kwenye maeneo ya pipakai, ili kuthibiti mtandao wa wahamiaji haramu ,magendo ,pamoja na ule wa uingizaji wa madawa ya kulevya nchini .

Pia Waziri Nchemba,katoa angalizo  kwa vyombo vya ulinzi na usalama kushiriki vilivyo katika kufanikisha zoezi la uandikishaji vitambuklisha vya uraia

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us