DK SHEIN AMTEUA BALOZI SEIF ALI IDD KUWA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 29, 2016

DK SHEIN AMTEUA BALOZI SEIF ALI IDD KUWA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR



Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa visiwa hivyo.

Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk Shein amemteua Balozi Idd ambaye alikuwa na wadhifa huo hata kipindi kilichopita.

Uteuzi wa Balozi Idd aliyezaliwa Februari 23, mwaka 1942, ulianza jana ikiwa ni siku nne tangu kuapishwa kwa Shein kuwa Rais wa Zanzibar.

Balozi Idd anakuwa mtu wa pili kuteuliwa na Dk Shein baada ya kuteuliwa kwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said mwishoni mwa wiki.

Dk Shein sasa atakuwa na wakati mgumu wa ama kumteua au kutomteua Makamu wa Kwanza wa Rais ili kukidhi matakwa ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani hakuna chama cha upinzani kilichokidhi vigezo vya kushirikishwa katika kuunda Serikali.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us