WATU 6 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI KATIKA MLIMA IPOGOLO-MKOANI IRINGA, 38 WAJERUHIWA | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 29, 2016

WATU 6 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI KATIKA MLIMA IPOGOLO-MKOANI IRINGA, 38 WAJERUHIWA



Watu sita wamefariki dunia katika ajali iliyotokea katika Mlima Ipogolo baada ya Basi la Lupondije linalofanya safari zake kati ya Iringa na Mwanza kupinduka baada ya mfumo wa breki kushindwa kufanya kazi. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema Dereva wa basi hilo ambalo hufanya safari zake kati ya Iringa na Mwanza alilazimisha kupita na abiria wote wakiwemo waliopaswa kushuka kituo kikuu cha mabasi Iringa ili kuwahi moja ya mabasi yaendayo Mbeya kutokea Dar es Salaam ili afaulishe abiria waliokuwa wanaelekea mkoani Mbeya. 


Abiria wanasema ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva kwani basi hilo lilimshinda na kupinduka.

Katika ajali hiyo jumla ya watu 38 wamejeruhiwa na baadhi yao kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa ambapo 11 kati yao wametibiwa na kuruhusiwa.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us