MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2016/2017. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, March 16, 2016

MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2016/2017.

MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2016/2017.

 
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yani Online Central Admission System (CAS), umefunguliwa rasmi tarehe 4 Machi, 2016, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada, Stashahada na Shahada kwa mwaka wa masomo 2016/17. Mfumo utajumuisha kozi zifuatazo;
1. Astashahada na Stashahada
2. Shahada za Elimu ya Juu

Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo;
1. Biashara na Utalii, mfano; Uhasibu, Meneja rasilimali watu, Wanyama pori, Mipango.
2. Ualimu.
3  Sayansi shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya mawasiliano, Usanifu majengo, Mifugo.
4. Afya, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi

Sifa za muombaji
1. Astashahada na Stashahada: Ufaulu wa alama D kwa masomo manne (4) ya mtihani wa kidato kidato cha nne
2. Shahada: Ufaulu wa GPA ya 2.7 kwa dipoma au mbadala pamoja na Ufaulu wa alama D kwa masomo manne (4) ya mtihani wa kidato kidato cha nne
NB: Sifa kwa kozi mahsusi ziko kwenye mwongozo wa kozi (Guidebook) ulioko kwenye mfumo.
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo;
1. Kwa eneo la Afya ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=
3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Ualimu, ada ni Tshs 30,000/=, muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
4. Kwa waombaji wa Shahada za Elimu ya juu, ada ya maombi ni Tshs 50,000/=

Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 31/05/2016.BONYEZA LINK HII KUJAZA FORM YA MAOMBI

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us