Trump asema huenda fujo zikazuka Marekani | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, March 16, 2016

Trump asema huenda fujo zikazuka Marekani


 
TrumpTrump ameshindwa katika mchujo jimbo la Ohio
Mfanyabiashara tajiri Marekani Donald Trump, amesema anafikiri kutatokea fujo iwapo ataongoza kwa wajumbe kisha chama chake cha Republican kitakosa kumuidhinisha awanie urais.

Bw Trump alishinda mchujo katika majimbo matatu zaidi, likiwemo jimbo la Florida mnamo Jumanne, ingawa alishindwa katika jimbo jingine muhimu la Ohio.
Hatua yake ya kushindwa Ohio huenda ikawawezesha wahafidhina wadhibiti wa chama cha Republican, ambao hawajafurahishwa na mtazamo wake, kumpendekeza mgombea mwingine kwenye mkutano mkuu wa kuidhinisha wagombea Julai.
 
TrumpMfuasi wa Donald Trump
Hayo yakijiri, Bw Trump amesema hatashiriki mdahalo katika runinga ya Fox News wiki ijayo akisema ametoshena na midahalo.
Katika chama cha Democratic, Hillary Clinton ameimarisha uongozi wake na kumshinda mpinzani wake wa pekee Bernie Sanders katika majimbo manne yaliyofanya mchujo Jumanne.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us