Uliye naye ni mtu sahihi kwako au umebugi? | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, March 25, 2016

Uliye naye ni mtu sahihi kwako au umebugi?

Image result for love couple imagesHakuna jambo linalowasumbua watu wengi katika uhusiano wa kimapenzi kama kumtambua mwenzi sahihi. Upo msemo maarufu mitaani kwamba ni bora ukosee mambo mengine yote lakini siyo
kukosea kumchagua mwenzi wa maisha yako! Swali la msingi, utajuaje kama huyo unayeishi naye, awe mke, mume, mchumba au mpenzi ni mtu sahihi?

Pengine nikuulize hata wewe msomaji wangu, unajuaje kama mwenzi wako unayeishi naye au uliyenaye ni mtu sahihi kwako? Una uhakika gani kwamba maisha yako ukiwa naye yatakuwa mazuri na hatakuja kuuvunja moyo wako? Huenda wengi wakakosa majibu zaidi ya kuishia tu kusema: ni mtu sahihi kwa sababu nampenda au ananipenda.

Hata hivyo, upendo pekee hautoshi kukufanya uamini kwamba huyo uliyenaye ni mtu sahihi kwa sababu upendo kama zilivyo hisia nyingine, kuna wakati huongezeka na kuna wakati hupungua au kuisha kabisa kwa hiyo kama unampima mwenzi wako kwa kigezo hicho, ipo siku utahisi kwamba pengine hukufanya uamuzi sahihi.

UTAMJUAJE KAMA NI SAHIHI?
Mtihani mkubwa ni namna ya kugundua kwamba huyo unayeishi naye ni chaguo sahihi katika maisha yako. Yapo mambo mengi unayoweza kuyatumia kumpima mwenzi wako lakini katika makala haya, tutazungumzia mambo manne ya msingi.

UNARIDHIKA UKIWA NAYE?
Jambo kubwa na la msingi linaloweza kukuonesha kwamba upo na mtu sahihi katika maisha yako ni kuridhika. Kuridhika ninakokuzungumzia hapa, ni ile hali ya moyo wako kujihisi kama unapata kila unachokihitaji na huna sababu ya kufikiria kuwa na mtu mwingine.
Kuridhika ninakomaanisha hapa, si lazima mtu awe na uwezo wa kukupa magari, majumba au vitu vya thamani kubwa, hapana. Namaanisha ile hali ya kuridhika kuanzia kihisia, kimawazo, kimapenzi na kimaisha kwa jumla.

Hujawahi kuona watu wanaishi maisha ya kimaskini lakini wana furaha, wanapendana, wanaheshimiana na kudumu? Ni kwa sababu kila mmoja ameridhika na mwenzake. Hujawahi pia kuona wake wa matajiri wanatoka kimapenzi na mahausiboi au vijana wa mitaani? Ni kwa sababu hawajaridhika kwenye maisha wanayoishi, hata kama wanapata kila kitu.
Wakati mwingine, baadhi ya watu hujaribu kufananisha uhusiano waliopo na waliowahi kuishi nao (ex), si makosa kulinganisha lakini isiwe kwa lengo la kubomoa.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us