Odinga ampigia saluti magufuli | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, April 04, 2016

Odinga ampigia saluti magufuli

Odinga

 Bw Odinga amekuwa kaskazini magharibi mwa Tanzania kwa siku tatu
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amesema ana imani Rais wa Tanzania John Magufuli ataisaidia Tanzania kukabiliana na changamoto zinazoikabili.
Bw Odinga amerejea nchini Kenya baada ya kumaliza mapumziko ya siku tatu eneo la Lubambangwe, wilaya ya Chato mkoani Geita, ambako alimtembelea Rais Magufuli ambaye pia yupo mapumzikoni.
Akizungumza katika uwanja wa michezo wa shule ya Sekondari ya Chato kabla ya kuabiri helikopta, Bw Odinga amesema ana imani kuwa Rais Magufuli ataisaidia Tanzania kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo umaskini unaowakabili wananchi wake.
"Lakini mimi najua yeye mwenyewe ana maono, anaona mbele na anajua yale ambayo yanatakiwa yafanyike ili Tanzania iinuke, itoke katika hali ya ufukara na kuwa katika hali ya maendeleo zaidi," amesema Bw Odinga kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Tanzania.
Bw Odinga, ambaye kwa sasa ni kiongozi wa mrengo wa upinzani Kenya, amekuwa rafiki wa karibu wa Dkt Magufuli.
Urafiki wao ulikolea zaidi wawili hao walipokuwa mawaziri wa ujenzi na barabara.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us