Hizi ni njia Tatu zinazoweza Kusaidia Mahusiano yako Kudumu Kwa Muda Mrefu... | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, July 14, 2016

Hizi ni njia Tatu zinazoweza Kusaidia Mahusiano yako Kudumu Kwa Muda Mrefu...

Mahusiano mengi yamekuwa yakivunjika kwa kushindwa kudumu kwa muda mrefu kutokana na kila mtu kumchoka mwenzake. Unaweza kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu na kamwe usichoke kumwona au kutaka zaidi kutoka kwa mpenzi wako.

Hizi ni njia tatu zinazoweza kusaidia mahusiano yako kudumu kwa muda mrefu:

Geuza mtazamo wa mapenzi

Unapaswa kutumia kila nafasi unayoipata kufanya mapenzi kama nafasi ya kumuonyesha kitu kipya mpenzi wake – Mwisho utagundua kitu kutoka kwa mpenzi wako huyo!

Jitahidi kusoma na kujifunza njia mpya kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako hali itakayopelekea kumlinda mpenzi wako asitoke nje ya mahusiano yenu.

Watu wengi wamezoea kuwa mwanaume ndio kiongozi wa kila kitu, hali iliyopelekea mpaka wanawake wengi hawezi kumuambia mtu wake kuhusu kufanya ‘tendo’ mpaka mwanaume ndio aanze kusema. Hilo kwenye mapenzi ni kitu ambacho kinapaswa kuwekwa kando ili kuleta furaha kwenye mapenzi yenu.

Tafuta ushauri

Kuna mbinu nyingi ambazo wapenzi hudhani wanazijua, lakini ni njia moja ya kuhakikisha kuwa mapenzi yananoga kila siku ni kutafuta mbinu mpya na za kipekee.

Wapenzi wengi wamekuwa waoga kuomba ushauri kama kuna matatizo ndani ya mahusiano yao, hali inayopelekea mtu huvumilia matatizo hayo mpaka mwisho wake huamua kulisaliti penzi lake kwa kutafuta furaha kwa mtu mwingine.

Kwenye mapenzi siyo kila rafiki wala mtu wako wa karibu anaweza kukupa ushauri mzuri utakaokufaa – Kuna wengine watakushauri vibaya ukajutia maamuzi yako hapo mbeleni. Unaweza kuwafuata watu waliodumu kwenye mahusiano kwa muda mrefu wakiwa na furaha na kuweza kuomba ushauri kujua wamefanyaje mpaka kufikia hapo ili uweze kufikia malengo na mpenzi wako.

Jua vitu anavyovipenda/ havipendi mpenzi wako

Unapaswa kuvijua vitu ambavyo havipendi mpenzi wako ili kujiepusha na kumkwaza mara kwa mara ili hata ikitokea hivyo ujue kwa wakati huo yupo kwenye ‘mood’ gani.

Aidha wapenzi wengi wamekuwa hawa fahamu sehemu za wapenzi wao zinazowasisimua na kupandisha raha au kumfikisha ‘kileleni’. Hali hiyo imepelekea wapenzi wengi kushindwa kudumu kwa muda mrefu kwenye mahusiano yao.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us