HEBU ONA PICHA ZOTE UKWELI KUHUSU MAPAMBANO YA POLISI NA MAJAMBAZI JANA HUKO VIKINDU | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, August 27, 2016

HEBU ONA PICHA ZOTE UKWELI KUHUSU MAPAMBANO YA POLISI NA MAJAMBAZI JANA HUKO VIKINDU


Eneo la Mtaa wa Vikindu Mashariki mkoani Pwani kwenye nyumba ya mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Mzee Manitu paligeuka uwanja wa mapambano baada ya polisi kuizingira nyumba hiyo na kupiga risasi nyingi hewani wakati wakimtaka jambazi anayetuhumiwa kufanya mauaji ya katika tukio la kuuawa askari polisi wanne waliokuwa wakibadilishana lindo kwenye Benki ya CRDB Tawi la Mbande wialayani Temeke jijini Dar. Katika tukio hilo Afisa wa Polisi mwenye cheo cha ASP Thomas Njuki wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi ameuawa.

Baada ya jambazi huyo kumuua askari, jeshi la polisi liliongeza nguvu eneo hilo na kupiga mabomu na risasi nyingi hewani zilisababisha taharuki katika eneo hilo na kusababisha kila mmoja aseme lake.

Mapaparazi wetu baada ya kufika eneo hilo walitaka kuzungumzia na maofisa wa polisi waliokuwa eneo hilo akiwemo, RPC wa Pwani, Bonaventura Mushongi, Gilles na Kamishna Mwandamizi wa Jeshi hilo, Liberatus Sabas lakini wote walisema hawawezi kuongea chochote mpaka wapate ruhusa kutoka ngazi za juu kwa kuwa tukio hilo si la Kimkoa bali ni la Kitaifa.

Licha ya viongozi hao kukataa kuzungumza, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili ambaye alikuwa bega kwa bega na askari hao alisema kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wanaume 7 ambapo walikutwa wanaume 3 na wanawake 3 ambapo mwanaume mmoja aliyetajwa kumuua Afisa huyo wa Polisi alitoroka pamoja na silaha yake.

Hakuna Jambazi yeyote aliyeuawa katika tukio hilo zaidi ya afisa huyo wa polisi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili
Angalia picha
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/ ISSA MNALLY /GPL.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us