UKWELI KUHUSU MSANII BELLE9 KUJIUNGA NA WCB(SOMA HAPA) | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, August 27, 2016

UKWELI KUHUSU MSANII BELLE9 KUJIUNGA NA WCB(SOMA HAPA)

Kumekuwa na tetesi nyingi kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha msaani wa bongo fleva Belle 9 kusajiliwa kwenye lebo kubwa ya muziki wa bongo fleva Tanzania,WCB ianyomilikiwa na Diamond Platnumz.
Tetesi hizo ziliibuka baada ya kuonekana kwa kipande cha video zikumuonyesha Belle 9 akiimba pamoja na Diamond wimbo wa ‘kidogo’ kwa live band katika studio za lebo hiyo.Alipoulizwa kwa upande juu ya kujiunga na lebo hiyo ,Belle 9 alikuwa na haya ya kusema.
“Me ni msanii ambaye niko huru kukutana na wasanii wenzangu,na kama kuna mtu amefanya kitu kizuri ni vyema kumsapoti.Mimi binafsi nilikwenda tu kuitembelea ile studio,pia nilikwenda kuangalia bendi,maana mshikaji anajiandaa kufanya live band,Alichokifanya mshikaji ni kitu kizuri kwa maendeleo ya muziki wetu na mimi nilivutiwa nacho,lakini waandishi wanapoandika habari wanaangalia upande wao tu” alifunguka Belle anayetamba na kibao chake cha BMS (bunger,movie&selfie).

source: Tizneez

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us