9, wajitosa uspika Zanzibar. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, March 24, 2016

9, wajitosa uspika Zanzibar.


 Image result for majengo ya bunge  zanzibar

VITA ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar imepamba moto, huku mchuano mkali ukionekana kuwa kati ya Spika aliyemaliza muda wake, Pandu Ameir Kificho, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa (UVCCM) na Mbunge wa Jimbo la Donge, Sadifa Juma Hamis na Naibu Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Hamis Silima.

 

Akizungumza na waandishi wa habari hii jana Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya Kamati Maalumu Zanzibar Waride Jabu, alisema waliojitokeza kuomba nafasi hiyo ni tisa.

 

Wengine mbali na wanaochuana vikali ni Hakimu Mstaafu, Janeth Sekiola, David Mwakanjuki, Zubeir Ali Maulid, Mohamed Ali Ahmed, Mahamoud Mohamed Mussa na Abdallah Waziri Ramadhan.

 

"Majina haya ndiyo ya waliojitokeza kuwania nafasi hiyo, uamuzi wa mwisho utatolewa na Kamati Kuu ya (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwenye kikao kitakachofanyika kesho (leo, Machi 24)," alisema Jabu.

 

Jabu alisema haijalishi kama majina yatakayoteuliwa ni mawili, matatu ama manne, lakini kikao hicho ndicho kitatoa uamuzi.

 

Kificho yeye anagombea nafasi hiyo akiwa ni Spika wa kwanza wa Baraza la Wawakilishi tangu kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us