Dayna: AY na Prezzo wameniponza. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, March 24, 2016

Dayna: AY na Prezzo wameniponza.




dayna
MSANII wa Bongo Fleva, Diana Nyange ‘Dayna’, amesema kilichosababisha wakaachana na mchumba wake ni wivu wa mapenzi uliotokana na picha aliyopiga na wasanii wawili wa Kenya, Wahu na Prezzo pamoja na Mtanzania, Ambwene Yessaya ‘AY’.

Dayna anasema picha hiyo alipiga na wasanii hao kabla hajawa maarufu wala kujihusisha na muziki kwa kiasi kikubwa hivyo hiyo ilikuwa sehemu ya kutafuta marafiki wa kumsaidia kimuziki.
“Kutokana na picha hiyo mchumba wangu huyo alihisi kwamba mmoja wa wasanii hao labda natoka naye kimapenzi hivyo akawa hataki nipige picha na wasanii na nisijihusishe tena na masuala ya kimuziki.
“Muziki ni kitu ninachokipenda sana katika maisha yangu hapo nikaona wivu umezidi kwa mwezangu ambaye tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kike mwenye miaka 10, tukaamua kuachana nami nikaendelea na muziki wangu hadi leo bila mchumba, mpenzi wala nini na maisha yanaenda,” alijieleza mrembo huyo.
Dayna alianza kujulikana katika muziki mwaka 2008 baada ya kuimba wimbo wa ‘Mafungu ya Nyanya’ na msanii aliyewika katika kampeni ya urais na wabunge mwaka 2005, Marlow, kisha akatoa ‘Nivute kwako’ na sasa anatamba na wimbo wa ‘Ungejua’.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us