Bomba la Mafuta Kuokoa Zaidi ya Shilingi Trilioni moja | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, March 31, 2016

Bomba la Mafuta Kuokoa Zaidi ya Shilingi Trilioni moja

 
Dar es Salaam. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesema Uganda itachagua kupitishia mradi wake wa bomba la mafuta Tanzania kwa sababu ni nafuu kwa Dola 500 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1 trilioni), ikilinganishwa na ujenzi huo ukifanywa Kenya.
 
TPDC imetoa kauli hiyo huku kukiwa na maono tofauti juu ya ujenzi wa mradi huo, ambao unagombewa kati ya Tanzania na Kenya ambazo zina bandari zinakazofanikisha usafirishaji mafuta kutoka Uganda kwenda soko la dunia.
 
Akihojiwa katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Kituo cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk James Mataragio alisema anashukuru hivi sasa Watanzania wengi wanauona mradi huo kuwa ni suala la kitaifa, hivyo kuupa msukumo unaostahili.
Akionyesha sababu za Tanzania kupewa nafasi kubwa kushinda mradi huo dhidi ya Kenya, ambayo ilikuwa na nafasi hiyo tangu mwanzo wa upembuzi wa mradi huo, Dk Mataragio alibainisha miradi ya Tazama (Bomba la mafuta kati ya Tanzania na Zambia), Songosongo, Mnazi Bay na bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam.
 
Alisema miradi hiyo imetoa uzoefu wa kampeni za uelewa juu ya miradi, kutwaa ardhi kutoka kwa wananchi kwa utaratibu mzuri na kulipa fidia ya mashamba na mali zilizomo kwenye maeneo yanayopitiwa na mradi husika.
“Kwenye miradi tuliyoitekeleza hakuna malalamiko kutoka kwa wananchi. Hakuna aliyepunjwa, hivi sasa asilimia 70 ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na gesi. Haya ni mafanikio ya miradi iliyotekelezwa, kukamilika kwa bomba hili pia kutakuwa na faida kubwa hasa ajira kwa wananchi,” alisema.
Aliwataka Watanzania, kila mmoja kwa nafasi yake kushawishi na kuuvutia mradi huu na kubainisha faida nyingine zitakazofuata baada ya ujenzi wa mradi kuwa, ni ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano na gesi na kuongezeka kwa wawekezaji.
 
Kutokana na ushawishi unaoendelea kati ya Tanzania na Kenya, Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kufanya ziara nchini Ufaransa kuanzia Jumatato wiki ijayo.
Rais Kenyatta anatazamiwa kutumia ziara hiyo kushawishi Kampuni ya Total ambayo inahusika kwenye ujenzi wa mradi huo kulegeza msimamo wake, ili itumie Bandari ya Lamu kusafirisha mafuta hayo. Kenya inaituhumu Tanzania kwamba tangu awali ilishindwa kushiriki upembuzi yakinifu uliofanywa Bandari ya Mombasa.
 
Mradi huo ambao utaanza kutekelezwa mwakani na kuchukua miezi 36 kabla haujakamilika unaweza kujengwa njia tatu zilizopo. Kwanza ni kutoka Hoima mpaka Bandari ya Mombasa, au ile ya Hoima mpaka Bandari ya Lamu, zote za nchini Kenya. Ya tatu ni Hoima mpaka Bandari ya Tanga
 

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us