EgyptAir: Abiria apiga selfie na mtekaji wa ndege ya misri. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, March 31, 2016

EgyptAir: Abiria apiga selfie na mtekaji wa ndege ya misri.


Selfie ya Egyptair
Mtu aliyepiga picha na mtekaji wa ndege ya kampuni ya EgyptAir aliyevalia mkanda bandia wa mlipuaji wa kujitolea muhanga amesema kuwa alitaka kuuona vizuri ukanda huo.

Picha hiyo ya Ben Innes ,akitabasamu karibu na mtekaji wake katika ndege hiyo ya EgyptAir imesambazwa katika mitandao ya kijamii.
Bwana Innes anayeishi Aberdeen pia aliliambia gazeti la Jumapili la Sun kwamba alitaka kuonyesha tabasamu mbele ya shida.
Alisema kuwa picha hiyo iliochukuliwa na mfanyikazi mmoja wa ndege hiyo ilikuwa ''selfie bora zaidi''.
Ndege hiyo ilikuwa ikibeba abiria 55,ikiwemo raia 26 wa kigeni waliotoka Alexandria kueleka Cairo.
Wengi wa wale waliokuwa wameabiri ndege hiyo waliwachiliwa baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Lanarca lakini mtekaji huyo aliwazuia watu saba kabla ya kisa hicho kukamilika kwa amani.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us