Alichokisema ANNE KILANGO MALECELA baada ya kufutwa kazi na JPM. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, April 12, 2016

Alichokisema ANNE KILANGO MALECELA baada ya kufutwa kazi na JPM.

Anna Kilango
Leo taarifa ambayo imetrend vya kutosha kwa muda mfupi, ni kuhusu Rais wa J.M wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama Anne Kilango Malecela katika nafasi hiyo.


Mwanasiasa huyu Mkongwe amekumbwa na Panga hili baada ya kutoa taarifa hadharani kuwa, Mkoa wa Shinyanga haukuwa na watumishi hewa.

Kauli ambayo ilikinzana na tume rasmi ya uchunguzi iliyotumwa mkoani humo, ambapo iligundua watumishi hewa 45 na bado uchunguzi Zaidi unaendelea.

Akiongea na kituo cha radio cha Times Fm,Kilango amedai kuwa hana taarifa juu ya utenguzi wa nafasi hiyo kutoka kwa aliyemteua.

“Jamani Mimi sina taarifa sipendi kukizungumzia maana yake sijaambiwa na aliyeniteua, sina la kukwambia.” Alisema na kukata simu.

Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.
SOURCE:SWAHILI NEWS

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us