App ya simu ya Taliban yatolewa sokoni | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, April 05, 2016

App ya simu ya Taliban yatolewa sokoni


Taliban
Image captionWapiganaji wa Taliban wamekuwa wakipigana Afghanistan na Pakistan
Alemarah, programu inayotumiwa katika simu za Android iliyoundwa na kundi la wapiganaji wa Taliban imeondolewa kwenye
soko la programu la Google, Play Store.
App hiyo iliyozinduliwa tarehe 1 Aprili, miongoni mwa mengine, ilikuwa na taarifa rasmi na video kutoka kwa kundi hilo la Kiislamu kwa lugha ya Pashto.
Kundi hilo limesema kumetokea “hitilafu za kiufundi” baada ya app hiyo kutoweka.
Hata hivyo BBC imefahamu kwamba app hiyo imeondolewa kwa sababu inakiuka kanuni na sera za Google zinazokataa uchochezi.
App hiyo iligunduliwa na shirika la Marekani la Site Intel Group linalofuatilia shughuli za makundi ya kijihadi.
Google imekataa kuzungumzia app hiyo binafsi lakini ikasema kupitia taarifa kuwa: “Sera zetu zimeundwa kuridhisha wateja wetu na watu wanaotengeneza app. Ndio maana huwa twatoa apps zinazokiuka sera hizi kutoka kwenye Google Play."
Msemaji wa kundi la Taliban alikuwa ameambia Bloomberg kwamba app hiyo ilikuwa “sehemu ya juhudi za kiteknolojia za kufikia watu zaidi duniani.”
CHANZO;BBC  SWAHILI

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us